Ludovick Utoh: Serikali iongeze uwajibikaji, kiwango cha upotevu wa rasilimali kwa mwa 2021 ni mara mbili ya mwaka 2020

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Katika Kongamano la Uthibit na Tathmini linalofanyika jijini Dodoma, Aliyekuwa CAG Ludovick Utoh ametoa wito kwa serikali kuongeza uwajibikaji ili kupunguza kiwango cha upotevu wa rasilimali ambao umekuwa ukiripotiwa na CAG.

Ludovick amesema kiwango kilichopotea kwa mwaka wa fedha 2020/21 ni mara mbili ya kiwango kilichopotea mwaka 2019/20. Amesema hiyo sio alama nzuri. Ameitaka serikali itengeneza bodi ya udhibiti ili kudhibiti.

Amesema Uwajibikaji ni suala la muda na inabidi lianzia kwa watu, ili kudhibiti rasilimali za umma. Aidha watunga sera wametakiwa kuripoti masuala hasi na chanya ili kuongeza uwazi na kutoa picha kamili kwa wananchi.

Badala ya kuendelea kufanya ukaguzi, amesema CAG awe anafanya Tathmini na Udhibiti ili wahasibu waweze kuongezewa uwajibikaji.
 
Back
Top Bottom