Dkt. Mwigulu: Mifumo ya kielektroniki ni muarobaini upotevu wa mapato ya serikali

Msichoke

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
569
400
View attachment EGA18017.jpg


Matumizi sahihi na salama ya mifumo ya kieletroniki Serikalini, yametajwa kuwa suluhisho la kudumu katika kuziba mianya ya upotevu wa rasilimali za serikali ikiwemo mapato yatokanayo na vyanzo mbalimbali nchini.

Hayo yameelezwa jana jijini Dodoma na Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba, wakati akipokea na kuzindua Mfumo wa Kieletroni wa Kuratibu Ununuzi wa Mafuta Serikalini, ujulikanao kama GPSA Intergrated Management Information System’ (GIMIS), kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene.

Alisema kuwa, matumizi ya mifumo imara ya kielektroniki yanasaidia kuondoa mianya ya upotevu wa rasilimali za Serikali na kudhibiti watumishi wasio waadilifu, kwakuwa malipo yote ya serikali yatalipwa kupitia njia sahihi na salama katika taasisi husika.

“Tukifanya kazi kupitia mifumo ya kielektroniki tunapunguza makosa mengi ya kibinadamu, hivyo matumizi sahihi ya mifumo hii yatatuwezesha kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wetu ikiwa ni pamoja na eneo la ukusanyaji wa mapato mbalimbali ya serikali”, alifafanua Dkt.Mwigulu.
View attachment 10.jpg

Akieleza kuhusu mfumo huo Dkt. Mwigulu alisema kuwa, mfumo wa GIMIS unatumiwa na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), ambapo kwa sasa majukumu yote ya Wakala yanatekelezwa kupitia mfumo huo ambao umesaida kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Aidha, Dkt. Mwigulu aliielekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kuhakikisha inaunganisha mfumo wa Manunuzi Kielektroni (NeST) na mfumo wa GIMIS kwa kuwa, mfumo huo unatumiwa na Wizara, Mashirika ya Umma, Wakala, Ofisi za Mikoa na Halmashauri za Wilaya nchini katika kupata huduma za GPSA.
 
Back
Top Bottom