GOT season ya mwisho ndio imekuja kuharibu sijui nini kiliwakuta hawa watu aisee... nadhani ni vile waliitengeneza series mtu asiweze kutabiri lolote lijalo. Night king alikufa kihovyo haakutendewa haki kabisa hatukuona role ya mafunzo aliyopata arya kwenye vita ya mwisho.
Lakini tukiondoa S8 GOT inabaki kua series bora kuanzia uigizaji Hadi uandishi na realistic..LOTR ni fairly fantasy vitu vya kufikirika zaidi ila GOT kuna uhalisia.
Binafsi naona pambano la LOTR kwenye return of the king (Battle of Minas Tirrith?) Inazidiwa na Battle of the Bastard. Ile battle ni balaa hadi mtazamaji mwenyewe unakua unafeel kama upo vitani pia..
Batle zingine bora ni
- Batle of Hardhome
- Batle of Mereena
- Battle of Castle Black