Lubuva: Matokeo yabandikwe nje ya kituo husika!

Lubuva: Matokeo yabandikwe nje ya kituo husika!

TeamLowassa

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2013
Posts
1,495
Reaction score
937
Jaji Lubuva amesema ameagiza kwa mujibu wa taratibu, kura zipigwe, zihesabiwe na matokeo yabandikwe nje ya kituo husika

Chanzo: Jamhuri

==============================

UKAWA tufanye haya kujihakikishia ushindi:

1. Tupige kura na kulinda kura zetu hadi matokeo yatoke kwenye kituo husika; then matokeo hayo yaende kwenye Tallying Centre ya UKAWA
==============================

2. 'UKAWA TALLYING CENTRE' iwepo mbali ya ile ya NEC. Ili kuwe na uhakika kwamba matokeo yanyotumwa na wakurugenzi kwenda NEC ni sawa na yaliyopo kwenye Tallying Centre ambayo ni mkusanyiko wa matokeo ya kura zote kutoka kwenye vituo husika.

Tallying Centre ikikosekana, bao la mkono linatuhusu! Ulinzi wa kura ukikosekana, bao la mkono linatuhusu!

==============================

HIZI MBINU MBILI NDIO ZILIZOMUOKOA JOHN MNYIKA VINGINENVYO UBUNGE WAKE INGALIKUWA HISTORIA
 
Anaendelea kusema baada ya hapo wasimamizi wa uchaguzi watatakiwa wapokee matokeo kutoka kwenye vituo vyote kwa ajili ya kujumlisha kura na kuwatangaza washindi(udiwani na ubunge)

Matokeo ya kura zote(udiwani, ubunge na urais) yatabandikwa!
 
Hivi kura za rais zihesabiwe vituoni kutakuwa na tatizo gani?
 
Kura za rais pia zibandikwe vituoni tujue nani ni nani. Sio kusafirisha matokeo mpaka Dar tena vyama vya Ukawa vinatakiwa Jambo hili viwe na msimamo usioyumba kuhusu kura.

Mgombea wa Ukawa pia anatakiwa awe anawaambia watu kuwa kura zetu tutazilinda kwa njia zote kuliko kusema nipeni kura nyingi hata wakiiba nyingi zitabaki kwetu, hii inawavunja munkari wapiga kura.
 
huwezi kukiuka sheria kwa matakwa ya vyama
 
huwezi kukiuka sheria kwa matakwa ya vyama

Kura za rais pia ni vizuri zihesabiwe kituoni na matokeo yake yabandikwe kituoni. Huko mbele ibaki kazi ya kujumlisha tu! Kwenye kata ipatikane jumla ya kura za rais kwenye kata hiyo na ibandikwe kwenye ofisi ya kata. Kwenye jimbo ipatikane jumla ya kura za rais kwenye jimbo hilo na ibandikwe kwenye ofisi ya jimbo. Kazi ya hatua ya juu iwe ni kujumlisha tu kura za majimbo mbali mbali. Huu ndiyo utaratibu mzuri ambao utaepusha hisia za uchakachuaji wa matokeo! Naomba NEC izingatie ushauri huu!
 
hata za urais ni hvyo na kila jimbo litatangaza kura za urais baadae yanapelekwa nec
 
Kwani kuna shida gani na za urais zikitangazwa pale pale. Poa sie tutamsaidia kutangaza za majibo yote na kujumlisha wenyewe.
 
Kura za Rais nazo zinabandikwa kituoni. Wanachokataa NEC ambacho mimi sikubaliani nacho ni kwamba huruhusiwi kujumlisha kura za Rais kutoka vituo mbali mbali na kutangaza.

Ila kubandika, mbona hata 2010 walibandika ?

Kwa hiyo hapo sioni chochote alichoagiza, amekumbushia tu utaratibu wa siku zote ambao hata 2010 ulikuwepo

Kura za rais pia zibandikwe vituoni tujue nani ni nani. Sio kusafirisha matokeo mpaka Dar tena vyama vya Ukawa vinatakiwa Jambo hili viwe na msimamo usioyumba kuhusu kura.

Mgombea wa Ukawa pia anatakiwa awe anawaambia watu kuwa kura zetu tutazilinda kwa njia zote kuliko kusema nipeni kura nyingi hata wakiiba nyingi zitabaki kwetu, hii inawavunja munkari wapiga kura.
 
Tunataka hadi kura za uraisi zihesabiwe na zibandikwe vituoni!

Huo ndio utaratibu kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi. Kinachotakiwa ili kura zisiibiwe ni kuhakikisha kila kituo kinakuwa na mawakala ambao 'hawadanganyiki' na kuwa na tallying centre (mbali na ile ya NEC) kwa ajili ya kujumlisha kura za urais kama walivyofanya Nigeria. Yote haya yanawezekana ni kujipanga tu.
 
Naona lugha staa leo trh 01 wadau kunani?
 
Hayo ya rais wanaende kuyaombea dua!maana wasijefikiri wanajamba kumbe wamejinyea kabisa
 
Back
Top Bottom