Lubuva: Matokeo yabandikwe nje ya kituo husika!

Lubuva: Matokeo yabandikwe nje ya kituo husika!

Kura za Rais nazo zinabandikwa kituoni. Wanachokataa NEC ambacho mimi sikubaliani nacho ni kwamba huruhusiwi kujumlisha kura za Rais kutoka vituo mbali mbali na kutangaza.

Ila kubandika, mbona hata 2010 walibandika ?

Kwa hiyo hapo sioni chochote alichoagiza, amekumbushia tu utaratibu wa siku zote ambao hata 2010 ulikuwepo

Vizuri
Kama kura zote mpaka za Rais zitabandikwa itakua vyema sababu tutakua tumeiona picha mapema kabla ya kupelekwa Makao Makuu ya Nec ili kumtangaza mshindi.

Kinachotakiwa Vyama vya Ukawa Viwaandae Mawakala ambao ni Halisi sio Pandikizi wa Vyama vingine.

Ambao hawatakubali chochote kifanyike nje ya Utaratibu.

Tanzania Mpya inakuja.
 
Huo ndio utaratibu kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi. Kinachotakiwa ili kura zisiibiwe ni kuhakikisha kila kituo kinakuwa na mawakala ambao 'hawadanganyiki' na kuwa na tallying centre (mbali na ile ya NEC) kwa ajili ya kujumlisha kura za urais kama walivyofanya Nigeria. Yote haya yanawezekana ni kujipanga tu.

Sawa hata 2010 chadema walikuwa na jumla ya kura za Dr Slaa na siyo zile zilizotangazwa na tume na katiba ya sasa na sheria za uchaguzi haziruhusu kuzitangaza au kuzihoji popote au kwenye mahakama yoyote. Hapo ndipo katiba ya mzee Warioba itakapoondoa hiyo kasoro. Kwa sasa tukubali chochote watakachotangaza.
 
Kura za rais pia ni vizuri zihesabiwe kituoni na matokeo yake yabandikwe kituoni. Huko mbele ibaki kazi ya kujumlisha tu! Kwenye kata ipatikane jumla ya kura za rais kwenye kata hiyo na ibandikwe kwenye ofisi ya kata. Kwenye jimbo ipatikane jumla ya kura za rais kwenye jimbo hilo na ibandikwe kwenye ofisi ya jimbo. Kazi ya hatua ya juu iwe ni kujumlisha tu kura za majimbo mbali mbali. Huu ndiyo utaratibu mzuri ambao utaepusha hisia za uchakachuaji wa matokeo! Naomba NEC izingatie ushauri huu!
Tume izingatie ili kuondoa maneno.
 
hata za urais ni hvyo na kila jimbo litatangaza kura za urais baadae yanapelekwa nec

Ili Lubuva akwepe kuiingiza nchi katika sintofahamu hiyo ndiyo tu suluhisho, kwenye kila kituo matokeo yote matatu yabandikwe.
 
Ili Lubuva akwepe kuiingiza nchi katika sintofahamu hiyo ndiyo tu suluhisho, kwenye kila kituo matokeo yote matatu yabandikwe.

Bila hivyo upande wowote utakaoshindwa utakuwa na hisia za kuibiwa kura za urais na inaweza ikachochea machafuko. Lazima uwazi uwepo kwanini uwazi unaogopwa? Tume isipozingatia ushauri huu wasishangae wakijikuta wako mikononi mwa ICC!!!!
 
Kura za Rais nazo zinabandikwa kituoni. Wanachokataa NEC ambacho mimi sikubaliani nacho ni kwamba huruhusiwi kujumlisha kura za Rais kutoka vituo mbali mbali na kutangaza.

Ila kubandika, mbona hata 2010 walibandika ?

Kwa hiyo hapo sioni chochote alichoagiza, amekumbushia tu utaratibu wa siku zote ambao hata 2010 ulikuwepo

Hata mie.nakumbuka yalibandikwa,hivi kuna shida gani kujumlisha
 
Hata mie.nakumbuka yalibandikwa,hivi kuna shida gani kujumlisha

Shida ni kuwa kukiwa na tofauti kati ya zilizobandikwa na zitakazotangazwa na tume hakuna fursa ya kukata rufaa popote. Ni kukubali goli la mkono kwani hakuna jinsi.
 
Kwani kuna shida gani na za urais zikitangazwa pale pale. Poa sie tutamsaidia kutangaza za majibo yote na kujumlisha wenyewe.

Huruhusiwi kadri ya sharia ya Takwimu
 
Shida ni kuwa kukiwa na tofauti kati ya zilizobandikwa na zitakazotangazwa na tume hakuna fursa ya kukata rufaa popote. Ni kukubali goli la mkono kwani hakuna jinsi.

Ndio shida...Hii sharia ilitakiwa irekebishwe muda mrefu....Ni kandamizi....Yaani unaweza kua umeshinda ukaambiwa Umeshindwa and nothing happens
 
mbona zinahesabiwa hapo hapo vituoni jamani. Lubuva hajasema lolote jipya. Kura zinahesabiwa na kutangazwa kituoni. Ndio sheria hiyo.

Nasikia mfumo huu mya wa BVR kura za uRais zitatangazwa makao makui pekee.
 
Sawa hata 2010 chadema walikuwa na jumla ya kura za Dr Slaa na siyo zile zilizotangazwa na tume na katiba ya sasa na sheria za uchaguzi haziruhusu kuzitangaza au kuzihoji popote au kwenye mahakama yoyote. Hapo ndipo katiba ya mzee Warioba itakapoondoa hiyo kasoro. Kwa sasa tukubali chochote watakachotangaza.

Hii ni moja ya concern yangu kwa wana Ukawa.
Kilele cha nguvu zote ni kuhesabu na kutangaza matokeo ya urais.
Ukawa wakilegea hapa, imekula kwao.
 
Lubuva ameamua liwalo na liwe! safi sana.
 
IWE KTK MFUMO HUU:
***********************
URAIS
******
A--------1267
B--------2769
C-------1273
D-------7768

UBUNGE
*********
A------1223
B-------6788
C------2888
D------8888

UDIWANI
*********
A
B
C
C
*********************************
**********************************
HUU NDIYO MFUMO AMBAO UNGESTAHILI KUTUMIWA
ii
 
Back
Top Bottom