Lt. Gen Abrahaman Amir Shimbo kustaafu kesho

Moshe Dayan

JF-Expert Member
Feb 10, 2008
815
698
Mnadhimu mkuu wa jeshi (Chief of staff) Lt. gen Shimbo ataagwa rasmi kesho.

Kamanda huyu anastaafu kwa mujibu wa sheria za jeshi za kutimiza umri wa kustaafu baada ya kuongezewa muda wa kustaafu kipindi cha nyuma japo umri wake wa kustaafu ulishafika.

Shughuli ya kumuaga itafanyika kesho makao makuu ya jeshi, Upanga.

Ikumbukwe, alipata wadhifa wa unadhimu wa jeshi mwaka 2007 ambapo yeye na CDF Davis Mwamunyange walichukua madaraka kutoka kwa general Waitara.

Nitawajuza yatakayojiri kesho kwenye shughuli ya kumuaga huyu chief of staff.

Source: MOSHE DAYAN

mkuu umenikumbusha mbali sana huyo fisadi 2010 alizania hatostaafu, na hapa lissu katusaidia angepewa mkataba wa nyongeza na swaiba wake dhaifu... Nakumbuka hivi juu ya huyu jamaa
mashirika yanayotetea usawa wa jinsia, haki za binadamu, maendeleo ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi (femact) umetoa msimamo wa kutokubaliana na tamko lilitolewa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kile kilichodaiwa ni kuingilia shughuli za uchaguzi.

Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa tamko hilo dar es salaam leo, mkurugenzi mtendaji wa taasisi inayojihusisha na masuala ya utawala bora fordia, good govence convencer femact bw. Bubelwa kaiza alisema;

"tunashangaa kuona jeshi la wananchi wa tanzania (JWTZ) likifanyakazi za polisi wakati askari polisi wapo na inspekta jenerali wao hali hii haieleweki na nikinyume cha kanuni za msingi za utawala bora."

bw. Kaiza aliendelea kuhoji; "inakuwaje askari polisi wanaendelea kulipwa mshahara wakati kazi zao zinafanywa na wanajeshi wa jwtz?"

alisema kuwa ujumbe unaotolewa na tamko la vyombo vya usalama kuwa vimejiandaa kikamilifu kuwa vimeajindaa kupambana na mtu, watu, kikundi chama au taasisi yoyote itakayochochea kuyakataa matokeo ya uchaguzi ni kitisho cha dhahiri, sio kwa vyama vya siasa wala wagombee pekee bali dhidi ya jitihada za kujenga na kuimarisha utawala bora.

Wanaharakati hao kupitia tamko hilo walimtaka luteni jenerali abdulhaman shimbo kutambua kuwa sio wanajeshi wala silaha zinazoweza kulazimisha wananchi, vyama vya siasa na wagombea wao wakubaliane na matokeo ya chaguzi, bali unakubalika pale unapofanyika kwa kuzingatia vigezo vya msingi vya uchaguzi.

"vyombo vya ulinzi na usalama viache mara moja kuingilia mchakato wa uchaguzi kwa kuwa jambo hili linaweza kusababisha vitisho na vurugu dhidi ya wapiga kura na wananchi kwa ujumla.

Wiki iliyopita maofisa waandamizi wa jwtz na polisi walitoa tamko la kuwataka wananchi kuyakubali matokeo ya uchaguzi vinginevyo limejiandaa kukabiliana na watu waliopanga kuyapinga.

Hata hivyo alisema kuwa tamko la vyombo vya ulinzi na usalama lina agenda yake ya siri, si bure litakuwa ni jambo la kushangaza na kusikitisha sana iwapo watanzania watabaini kuwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama vimeanza kutumiwa vibaya na wanasiasa na vyama vyao kwa manufaa ya kikundi na maslahi binafsi kwa watu wachache.

Wanaharakati hao wamewataka vyama vya siasa na viongozi wao waache mara moja kujitafutia ushindi kwa kutumia mlango wa nyuma na kukubali matokeo.

Alisema kuwa uongozi wa dola sharti upatikane kupitia mashindano ya wazi kusaka ridhaa ya wananchi kidemokrasia katika uchaguzi unaokubalika kuwa huru na haki, siyo kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kutisha wapiga kura ili kujihakikishia ushindi.

Vile vile bw. Kaiza alisema kuwa wapiga kura waendelee kujibidisha kupata elimu ya mpiga kura ,kuhudhuria mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa na kusikiliza ahadi za wagombea wapembue na kuchambua kati ya pumba na mchele ili agosti 31 wafanye uamuzi wa kihistoria.

mnadhimu mkuu wa jeshi (chief of staff) lt.gen shimbo ataagwa rasmi kesho.

Kamanda huyu anastaafu kwa mujibu wa sheria za jeshi za kutimiza umri wa kustaafu baada ya kuongezewa muda wa kustaafu kipindi cha nyuma japo umri wake wa kustaafu ulishafika.

shughuli ya kumuaga itafanyika kesho makao makuu ya jeshi, upanga.

ikumbukwe, alipata wadhifa wa unadhimu wa jeshi mwaka 2007 ambapo yeye na CDF davis mwamunyange walichukua madaraka kutoka kwa general waitara.

Nitawajuza yatakayojiri kesho kwenye shughuli ya kumuaga huyu chief of staff.

Source. MOSHE DAYAN

aongezewe muda wa kustaafu kwa miaka mi3 zaidi hadi mwezi kama huu 2015 ili apate kutoa tamko la jeshi juu ya uchaguzi wa 2015. mkuu, abort mission ya kumuaga immediately.
 
Du sasa aliongezewa muda kwa sababu hakuna wanajeshi waadilifu na wenye taaluma kama ya kwake au ndo tuseme ndo kupendeleana nini
 
namtakia kustaafu kwema....
Ndomqakati wa kwenda kula bata na zile trilion 3 sasa...
Watakukomaje wadar es salamu...
 
Mzee wa Tril 4 anakwenda kugombea ubunge sasa....maana ana kila sababu ya kugombea ubunge ,pesa,kadi,na wajibu anao....ametumikia sana chama vile vile!na pia ni mwenzao!!

Arudishe pessa ya wandava wenzie na nyingine km alituibia na sie arudishe
 
Back
Top Bottom