Lt. Gen Abrahaman Amir Shimbo kustaafu kesho

Lt. Gen Abrahaman Amir Shimbo kustaafu kesho

kumbe ukiiba trilioni 4 ndo unakuwa muadilifu? Kazi ipo kwa tusiokuwa na mianya za kupiga hizo hela hatutakuwa waadilifu.

Tuache uongo tufikiri:

Twendeni taratibu sh. trilioni 4 ni bajeti ya Wizara nzima ya ulinzi kwa miaka zaidi ya minne. Sasa tuje kwenye mantiki Je, Lt gen Shimbo aliiba bajeti yote ya wizara ya ulinzi kwa kipidi chote hicho? Kwamba hakuna wanajeshi kulipwa mishahara, Wafanyakazi wizarani kulipwa mishahara.....wala magari kutembea kwa kipindi chote hicho.

Hebu tuwe tunafkiria kidogo tu. Inawezekana kuna alichochukua, lakini trilioni 4 kama inavyosemwa na watu kwangu a big no!
 
Sawa,aende akale pension ya matrioni aliyo jichotea.Hivi invisible alipotezea wapi hiyo thread jamaani?
 
Tuache uongo tufikiri: Twendeni taratibu sh. trilioni 4 ni bajeti ya Wizara nzima ya ulinzi kwa miaka zaidi ya minne. Sasa tuje kwenye mantiki Je, Lt gen Shimbo aliiba bajeti yote ya wizara ya ulinzi kwa kipidi chote hicho? Kwamba hakuna wanajeshi kulipwa mishahara, Wafanyakazi wizarani kulipwa mishahara.....wala magari kutembea kwa kipindi chote hicho. Hebu tuwe tunafkiria kidogo tu. Inawezekana kuna alichochukua, lakini trilioni 4 kama inavyosemwa na watu kwangu a big no!
...................na zile wazoweka Uswisi ni % ngapi ya bajeti ya Tz? kwani mishahara serikalini ilikuwa hailipwi na magari ya serikali yamepaki?
 
Plato wewe uu mgeni na izo trillion za shimbo dig deep utajagundua ukweli kwenye thread za hayo matrillion
 
Hawa wote tutakwenda nao sawa mwaka 2015 mara baada ya CDM kushika dola
 
...................na zile wazoweka Uswisi ni % ngapi ya bajeti ya Tz? kwani mishahara serikalini ilikuwa hailipwi na magari ya serikali yamepaki?

Inakisiwa zilizowekwa Uswis ni kama Bilioni 390 ambayo haifiki hata robo ya bajeti ya Tanzania ya Trilioni 11. Fikiri tena kama ana trilioni 4 maana yake ana mara 10 ya pesa za watanzania zilizoko Uswis!! Au kwa lugha rahisi ni zaidi ya pesa zote zilizofichwa Uswis na Waafrika mashariki!!

Au labda hufahamu tofauti ya Trilioni na Bilioni.......Tuanzie hapo!
??
 
Mwenzake Mkapa analia Wastaafu wamesahauliwa! Ngoja sasa na yeye aende huko akaonje joto ya jiwe. Kama Mkapa analia, sembuse yeye?

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com

Mkwe.re si alikuwa na biff na mzee nkapa, ndio maana alikuwa anampa adhabu kiaina, sometimes ku nutroliz ilibidi mkapa awe anapanda majukwaani kujidhalilisha, ili tu amfuraishe baba riz....
 
kumbe ukiiba trilioni 4 ndo unakuwa muadilifu? Kazi ipo kwa tusiokuwa na mianya za kupiga hizo hela hatutakuwa waadilifu.

kuna ushahidi..? thread ilifichwa sababu wakuu wa jf walishindwa kuthibitisha
 
YANGESOMEKA MAGAZETI HIVI,KATI YA MAFISADI WALIOJILIMBIKIZA FEDHA USWIS NI KATI YA HUYU SHIMBO

Ni kati ya mafisadi wasiopungua 50 walioorodheshwa ktk mtandao fulani wa kijamii!
Halafu eti anastaafishwa! Serikali yetu jamani? Ni zaidi ya tuijuavyo ila hakika mwisho wao mafisadi waja! Na watajiju!

tungekuwa na serikali magazeti ya kesho kutwa yangeandika hivi " Shimbo afikishwa mahakamani kwa ufisadi wa kutisha, anyimwa mdhamana"
 
platozoom

Wewe unamtetea kwa lipi, au ni shemeji mtu? kwani hujui kuwa Shimbo yumo katika ile list ya 30 billionaires of TZ, ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa ni mabilioni ambayo ameyaficha uswisi, kutokana na dili alizozifanya, ikiwemo Meremeta?! Sasa tunaanza kupata picha kuwa aliamua kujikusanyia mapesa hayo ayatumie wakati wa kustaafu.

Lakini ushauri wa bure ninaompa, ni bora pesa zetu hizo akaamua kuturejeshea nchini, lakini akiamua kakaidi ushauri huu, kwa mkakati unaoandaliwa, ashishangae, badala ya kustaafu kwa amani, akajikuta anapandishwa kizimbani Kisutu!!
 
Last edited by a moderator:
Heri akitoe maana alikuwa akitumiwa na Kikwete kuutisha upinzani. Hana lolote la kujivunia zaidi ya kuacha wingu zito juu ya usafi wake. Ni mmojawapo wa mafisadi tuliowalea na kuwafuga kwenye taasisi yetu nyeti. Nenda Shimbo na utokomee bila kugeuka nyuma. Laiti angefikishwa mahakamani ili haki itendeke. Lakini nani wa kumfikisha nani mahakamani wakati wote ni ngedere kwenye shamba la mahindi tena la bibi aitwaye Tanzia?
 
Hautapita muda mrefu tutasikia kateuliwa kuwa mwenyekiti wa board! Years of looting lakini bado atapata pension!
 
Inakisiwa zilizowekwa Uswis ni kama Bilioni 390 ambayo haifiki hata robo ya bajeti ya Tanzania ya Trilioni 11. Fikiri tena kama ana trilioni 4 maana yake ana mara 10 ya pesa za watanzania zilizoko Uswis!! Au kwa lugha rahisi ni zaidi ya pesa zote zilizofichwa Uswis na Waafrika mashariki!!

Au labda hufahamu tofauti ya Trilioni na Bilioni.......Tuanzie hapo!
??
Whether it is trillions or billions,it doesn't matter. issue hapa, kama pesa hizo ameziweka kwa kificho, bila BoT, kutoa kibali cha uwekaji wa pesa hizo, maana yake ni kuwa hizo ni pesa chafu, ambazo, zinahalalisha yeye apandishwe kizimbani mahakamani, kujibu mashtaka ya kujipatia pesa kwa njia ya ufisadi!!
 
Back
Top Bottom