Lt Col Alexander Nyirenda (RIP)

Wakulu Jf ni kisima cha maarifa na kila habari iliyofichwa itapatikana hapa najua!
Tuweke historia sawa kuhusu huyu kamanda mzalendo

Alikuwa ni mwafrika wa kwanza kuattend kozi ya uofisa wajeshi kule Sandhurst college UK akapata commission ya malkia kuwa second lieutenant mwafrika ktk jeshi la KAR. Kafanya kazi zake vizuri hadi tumepata uhuru, akapandisha mwenge juu ya mlima Kilimanjaro na bendera. Baada ya uhuru alikuwa ofisa mzalendo pekee kwa jeshi liloachwa na waingereza likiitwa Tanganyika Rifles. Huenda angekuwa chief of defence forces lakini kama kawaida yetu chuki fitina na majungu alijikuta anakumbwa na adhabu za rais baada ya maasi ya 1964 yaliyoanzisha jwtz akihusiahwa na kuhusika na uasi. Hapo ikawa mwisho wa ndoto na mipango yake ya maisha mzalendo huyu. Mwl Nyerere(Rip) alizungukwa na watu wenyw fitna na majungu na hakusita kuchukua hatua pale tu aliposikia hata rumours za watu wake wa usalama. Hivyo haikujulikana alienda wapi ni kwamba aliondolewa jeshini na ikawa ndo mwisho wake akaja kusikiaka tena publicly wakati anaumwa hadi alipopoteza maisha yake.

Haya pia yalimkuta Gen Mirisho Sarakikya aliyepewa ukuu wa jw baada ya kuundwa upya naye hakudumu walimpenda mwanzoni haikupita muda majungu yakaanza hatmaye Nyerere akampeleka ubalozini Nairobi alipoishi miaka mingi bila kukumbukwa hadi kastaafu ndo kwa aibu kubwa Mkapa akampa ujenerali wakati wa sherehe za miaka 40 ya jwtz ili asijisikie vibaya kuhudhuria na apate maslahi km cdf mstaafu kwani wenzie wanakula kuku tu!

Haya jamani jukwaa lipo wazi tuweke sawa kumbukumbu kwa vizazi vijavyo, hata jwtz hakufai kwa majungu na ubabaishaji hatujapata vita tu ya kutia msukosuko ndo mngejua kama mna jeshi au ni siasa za kina Nchimbi. Hawa ni wachache wapo wengi sana walioharibiwa kwa vile wapo smart tu. Wasio na elimu ndo majenerali na makanali wasomi wanapigwa vita sana huko.
 
Du, mzee wangu Mzuzu wewe inaelekea ulichelewa kidogo kufika hapa jamvini. Swala la General Nyirenda (in fact siyo Lt. Col. bali ni Brig. Gen.) lilishajadiliwa hapa kikaoni kwa kina sana pamoja na lile na Gen. Sarakikya. Hukuitaji kuanzisha thread nyingine kuhusu jambo hilli, ni afadhali ungetafuta discussion za huko nyuma na kuzifufua kama uliona lazima kusudi watu waunganishe kwa urahisi.

Huenda ni kweli kuwa maasi ya 1964 na mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea Nigeria ya mwaka 1966 yaliyofanywa na Gen Gowon (ambaye alisoma na Gen. Nyirenda kule Sandhurst) vilichangia sana kumfanya Nyerere amwondoe Nyirenda kutoka jeshini na kumpeleka kwenye diplomatic corps. Vile vile huenda njama za mapinduzi za mwaka 1972 zilizofanywa na maofisa wa jeshi wasomi wa kimeru pia zilichangia kumfanya Nyerere amwondoe Sarakikya jeshini na kumweka kwenye diplomatic corps. Lakini sidhani kama ni lazima turudie mijadala hii ambayo tulishafanya siku za nyuma. Mijadala hiyo inapataika kwenye linki zifuatazo hapa chini.

(a) Nyerere kama mtu na utawala wake

(b) Lawama kwa Nyerere

(c) Historia ya taifa hili kadri tunavyoweza kukumbuka

(d) Maombolezo ya Kifo cha General Nyirenda
 
Fitna na majungu? Kumbuka hizo ndizo enzi ambazo akina Col. Menguistu, Gen. Siad Barre, Gen. Gowon, Col. Gadaffi, Col. Jerry Rawlings, Gen. Amin, Gen. Nguema, Sajenti Doe, na watemi wengine wa kijeshi walifanya vitu vyao na kuvuruga nchi zao. Si afadhali na Nyerere alikuwa anawapeleka ubalozini..
 
Ok nashukuru sana ngoja nikajichotee elimu iliyopo huko mkuu!
 
Tatizo letu tunataka kuishi na kusubiri wale wenye historia yetu vichwani mwao wafe ndio tuanze kuuliza!
 
Fitna na majungu? Kumbuka hizo ndizo enzi ambazo akina Col. Menguistu, Gen. Siad Barre, Gen. Gowon, Col. Gadaffi, Col. Jerry Rawlings, Gen. Amin, Gen. Nguema, Sajenti Doe, na watemi wengine wa kijeshi walifanya vitu vyao na kuvuruga nchi zao. Si afadhali na Nyerere alikuwa anawapeleka ubalozini..

Unajua bwana,

Miaka hiyo ya sitini hadi sabini ilitokea kama staili kwa viongozi wa kijeshi kujichukulia madaraka ya kiserikali. Sasa ukizingatia kuwa mfumo wa utawala wetu ulikuwa bado mchanga sana, kulikuwa na lazima kwa viongozi wa kiserikali kuwa makini sana dhidi viongozi wa kijeshi. Kwa hilo nadhani Nyerere alikuwa smart sana kwa vile ndiye alikuwa kiongozi wa kwanza Afrika kuvunja jeshi lake katika Brigade zinazojitegemea na mwishoni kuwa na divisheni zinazojitegemea. Ku-decentralizze uongozi wa jeshi kuliisadia sana Tanzania kuwa imara dhidi ya mapinduzi ya kijeshi.
 
ndo maana hawa jamaa tunawajengea golf courses, na wakistaafu tunawapa uwenyeviti wa board nyeti ili wasinuse mapinduzi
 
Yah kwa muundo wajeshi uliopo sasa hakuna wanaoweza kupanga mapinduzi wakafanikiwa namkubali mwl kwa hilo. Kuanzia elimu wanyopata maafisa na askari hadi hifadhi ya silaha ni ngumu na gharama kubwa kuvikutanisha pamoja. Stoo za mabomu na risasi zipo mali sana na mashine za kupigia kiasi ambacho anayeorganize labda aje na yake yote. Mahusiano kati ya commands pia utata! Mabomu ya mbagala kwa mfano mashine za kupigia zipo Dodoma na Arusha. Ndege chache zipo Moro mabomu Mtwara etc vikosini ni Smg na Sar na risasi za guard tu! Huyu ni Nyerere alifanya. Elimu ilikuwa standard nzuri ya kimataifa hadi 1984 wakati wa plan nyingine ya mapinduzi. Baada ya hapo ikafanyika dilution kubwa na leo capt wa Tz hata kuongea kiingereza na coplo wa Kenya hajui. Huwezi kumlinganisha hata na robo ya ufahamu aliokuwa nao Capt Tamim, Capt Hatty McGhee au Lt Rwechungura by then!
 
ndo maana hawa jamaa tunawajengea golf courses, na wakistaafu tunawapa uwenyeviti wa board nyeti ili wasinuse mapinduzi

Kwa sasa hamna mwanajeshi mwenye kiwango hicho mkuu! Wanalialia tu hata ndo maana mafisadi hawana waiwasi kwa lolote na hata serikali haijali kwa vile hamna jeshi na kila siku wanasema ni siri
Usiri ni kuficha udhaifu wa jeshi lenyewe!
 
Wakulu Jf ni kisima cha maarifa na kila habari iliyofichwa itapatikana hapa najua!
Tuweke historia sawa kuhusu huyu kamanda mzalendo. Hivyo haikujulikana alienda wapi ni kwamba aliondolewa jeshini na ikawa ndo mwisho wake akaja kusikiaka tena publicly wakati anaumwa hadi alipopoteza maisha yake.

- Mkuu Mzuzu heshima mbele sana, ninamkumbuka sana Marehemu Nyirenda, ninajua tu kwamba alikuwa akiishi tena kwa maisha ya kifahari sana kule Lusaka, Zambia huku watoto wake wakisoma shule UK.

- Nikiwa Lusaka kwa safari zangu za kawaida nimekutana naye sana na kuongea naye sana one on one akiwa hai, na hata kuembelea sana nyumbani kwake Lusaka, maeneo ya Kabwata Estate, niliwahi kumuuliza kulikoni yeye kuishi kule na sio Tanzania, hakuwa very interested na the subject ingawa alisema machache sana kuhusiana na siasa zake na Mwalimu hii ilikuwa ni in the early 80s,

- Ingawa nilikuwa mdogo kiumri, lakini my conclusion ni kwamba whatever the arrangement za yeye kuishi kule at the time, alionekana kuwa na maisha mazuri sana na ya kifahari sana kulinganisha na karibu viongozi wote wa Tanzania then including hata Mwalimu mwenyewe, lakini one thing sikuelewa ni kwamba why he was very much at home arround viongozi wa juu wa Zambia ambao siku zote walikuwa wakim-treat with very high respect, hilo tu ni swali moja sikuweza kupata jibu, why?

- Sikumsikia tena, mpaka hapa majuzi alipokuwa akikaribia mwisho wa maisha yake, I was shocked kusikia kwamba hata alikuwa akiishi Tanzania tena kwenye maisha ya kiwango cha chini, personal nilisikitishwa sana, sasa kinachosikitisha zaidi ni habari nyingi sana ambazo zinawahusu hawa viongozi wa wakati ule, ni vigumu sana kujua ipi ni ya ukweli na ipi ni uongo. Niliwahi kumuuliza Marehemu Mzee Chiume, ambaye ninaamini sana kwamba walikuwa very close, lakini my conclusion ni kwamba tatizo la Kambona, litakua ndilo lile lile la Nyirenda kwa sababu walikuwa one people.

Haya pia yalimkuta Gen Mirisho Sarakikya aliyepewa ukuu wa jw baada ya kuundwa upya naye hakudumu walimpenda mwanzoni haikupita muda majungu yakaanza hatmaye Nyerere akampeleka ubalozini Nairobi alipoishi miaka mingi bila kukumbukwa

- Gen. Sarakikya, kwanza alihamishiwa kwenye wizara ya utamaduni na michezo, baadaye akahamishiwa ubalozi wetu Lagos, na baadye Addis, kabla ya kuletwa Nairobi, ambako ndiko alikomalizia na kustaafu, ninaamini kuwa wanajeshi ambao walianza kuwa a threat kwa utawala wa Mwalimu, akaamua kuwahamishia nje, nao ni yeye (Gen. Sarakikya), Major Gen. Mayunga(Zaire), na Brigedier Mwakalindile (Mozambique) the then rising star huko JWTZ ambako aliondoka na cheo cha Chief of Staff,

- Whatever the case, ninaamini hawa wali-benefit sana personally na kupelekwa huko nje, maana kuacha Mayunga, hawa wengine walitajirika sana na hasa Gen. Sarakikya, ambaye kwa sasa ni majority owner wa Azania Bank, na mjumbe wa bodi nyingi sana nchini, kwa hiyo kama kweli kisiasa walikuwa ni maadui wa Mwalimu, basi kuna something about him hatuambiwi ukweli, kwa sababu unawapaje maadui zako nafasi za kwenda kujitajirisha binafsi, tena kwa mgongo wa ile ile serikali unayoiongoza? Especially with a lot of info mjini kwamba walikuwa wanataka kumpindua Mwalimu?

I mean Mkuu Mzuzu, samahani sana huo ni mchango wangu mdogo on the subject.

Respect.

FMEs!
 
Wakulu Jf ni kisima cha maarifa na kila habari iliyofichwa itapatikana hapa najua!
Tuweke historia sawa kuhusu huyu kamanda mzalendo

Alikuwa ni mwafrika wa kwanza kuattend kozi ya uofisa wajeshi kule Sandhurst college UK akapata commission ya malkia kuwa second lieutenant mwafrika ktk jeshi la KAR. Kafanya kazi zake vizuri hadi tumepata uhuru, akapandisha mwenge juu ya mlima Kilimanjaro na bendera. Baada ya uhuru alikuwa ofisa mzalendo pekee kwa jeshi liloachwa na waingereza likiitwa Tanganyika Rifles. Huenda angekuwa chief of defence forces lakini kama kawaida yetu chuki fitina na majungu alijikuta anakumbwa na adhabu za rais baada ya maasi ya 1964 yaliyoanzisha jwtz akihusiahwa na kuhusika na uasi. Hapo ikawa mwisho wa ndoto na mipango yake ya maisha mzalendo huyu. Mwl Nyerere(Rip) alizungukwa na watu wenyw fitna na majungu na hakusita kuchukua hatua pale tu aliposikia hata rumours za watu wake wa usalama. Hivyo haikujulikana alienda wapi ni kwamba aliondolewa jeshini na ikawa ndo mwisho wake akaja kusikiaka tena publicly wakati anaumwa hadi alipopoteza maisha yake.

Haya pia yalimkuta Gen Mirisho Sarakikya aliyepewa ukuu wa jw baada ya kuundwa upya naye hakudumu walimpenda mwanzoni haikupita muda majungu yakaanza hatmaye Nyerere akampeleka ubalozini Nairobi alipoishi miaka mingi bila kukumbukwa hadi kastaafu ndo kwa aibu kubwa Mkapa akampa ujenerali wakati wa sherehe za miaka 40 ya jwtz ili asijisikie vibaya kuhudhuria na apate maslahi km cdf mstaafu kwani wenzie wanakula kuku tu!

Haya jamani jukwaa lipo wazi tuweke sawa kumbukumbu kwa vizazi vijavyo, hata jwtz hakufai kwa majungu na ubabaishaji hatujapata vita tu ya kutia msukosuko ndo mngejua kama mna jeshi au ni siasa za kina Nchimbi. Hawa ni wachache wapo wengi sana walioharibiwa kwa vile wapo smart tu. Wasio na elimu ndo majenerali na makanali wasomi wanapigwa vita sana huko.
Kipindi kirefu baada ya uhuru jeshi letu liliipamba historia ya Tanzania. Kwa makusudi naona watu wanataka kufanya kama ile kazi waliyotolea jasho na damu ndugu zetu hawa haikuwa na thamani. Tuanze kuwapa heshima wanayostahili tuachane na uzushi
 
Blaza wa mdingi wangu naye alipigwa kibano hadi kuachia ngazi jeshini kwa vile alisoma Israel. Lakini wale walo mbana wako wapi leo?
Watu wamevuruga nchi kiasi kwamba sijui wajukuu zao watapata raha gani?!
 
Mimi binafsi nilikuwa napenda kuiomba JF ipitishe petition ya kumwomba Rais wa Tanzania awapandishe vyeo makamanda wote wa Jeshi waliotoa michango mikubwa ya kijeshi kwa taifa hili wawe majenerali kamili baada ya kustaafu hata kama hawakufikia ngazi hiyo wakiwa jeshini. Hii isijali kama wako hai au wameshafariki. Kufanya hivyo kutasaidia kuwaweka wasomi wetu wa mambo ya jeshi kama vile General Nyirenda aliyesoma Military Science kule Sundhurst kuwa katika ngazi moja na General Twalipo ambaye hakusoma Military Science popote pale ila alikuwa msiri mkubwa sana wa Nyerere.

Kuna wengi ambao kulingana na muundo wa jeshi wakati ule wasingeweza kuvuka viwango vya luteni kanali lakini leo hii kwa madaraka yale yale wangekuwa ni majenerali.

Watu kama General Kotta (baba yake Faraja Kotta) ambaye alisomea mambo ya mizinga kwa kina sana kule Kanada na Israel na akaongoza kikamilifu kikosi chetu cha mizinga wakati wa vita ya nduli Amini, na e General Herman Lupogo aliyepanga plan ya vita ile tangu A to Z wakati akiwa kanali watakuwa generali kamili.

Kuna majenarali nusu wengi ambao inabidi tuwatunze kwa kuwafanya majenerali kamili kwa matendo yao yaliyoturudishia heshima yetu kwa namna moja ama nyingine wakati ule: Mayunga, Marwa, Walden, Kotta (my hero), Kiwelu, Lupogo, na wengineo.
 
FMES,
Kabla ya Mwalimu kumwondoa Sarakikya jeshini alimwita pale Msasani na kumwambia kama anakitaka hicho kiti ambacho Mwalimu alikuwa amekilalia basi awaombe raia wa Tanzania na si kufanya njama za mapinduziya kijeshi. Kwa hiyo naaamini kabisa kuwa zile njama za 1972 alihusika kabisa.
 
Mimi binafsi nilikuwa napenda kuiomba JF ipitishe petition ya kumwomba Rais wa Tanzania awapandishe vyeo makamanda wote wa Jeshi waliotoa michango mikubwa ya kijeshi kwa taifa hili wawe majenerali kamili baada ya kustaafu hata kama hawakufikia ngazi hiyo wakiwa jeshini. Hii isijali kama wako hai au wameshafariki. Kufanya hivyo kutasaidia kuwaweka wasomi wetu wa mambo ya jeshi kama vile General Nyirenda aliyesoma Military Science kule Sundhurst kuwa katika ngazi moja na General Twalipo ambaye hakusoma Military Science popote pale ila alikuwa msiri mkubwa sana wa Nyerere.

Kuna wengi ambao kulingana na muundo wa jeshi wakati ule wasingeweza kuvuka viwango vya luteni kanali lakini leo hii kwa madaraka yale yale wangekuwa ni majenerali.

Watu kama General Kotta (baba yake Faraja Kotta) ambaye alisomea mambo ya mizinga kwa kina sana kule Kanada na Israel na akaongoza kikamilifu kikosi chetu cha mizinga wakati wa vita ya nduli Amini, na e General Herman Lupogo aliyepanga plan ya vita ile tangu A to Z wakati akiwa kanali watakuwa generali kamili.

Kuna majenarali nusu wengi ambao inabidi tuwatunze kwa kuwafanya majenerali kamili kwa matendo yao yaliyoturudishia heshima yetu kwa namna moja ama nyingine wakati ule: Mayunga, Marwa, Walden, Kotta (my hero), Kiwelu, Lupogo, na wengineo.

Hawa watu wanaharibu makusudi kwa kutafuta maslahi binafsi sijui vizazi vinavyokuja vitajifunza nini kutoka kizazi hiki. Hakuna kumbukumbu inayotunzwa na watu wanahribu hata nyaraka kupoteza ushahidi baada ya kufanya mambo ya kifisadi
 
Tusilaumu tusichokifahamu vizuri!Huyu Nyerere tunayemlaumu kwa kutompa ujenerali sarakikya ni huyu huyu aliyempandisha cheo kutoka ukapteni mpaka ubrigedia jenerali!tafakari kwanza!pili na mimi ni kati ya watu niliokuwa namuonea huruma sana nyirenda ila ukifatilia kiundani utajua tu jamaa alikuwa na tatizo!ebu tujiulize je ni kwa nini nyerere amteue sarakikya kuwa CDF kutoka ukapteni na sio nyirenda ambaye alikuwa kapteni by then kama sarakikya tena na ujiko kibao wa kupandisha mwenge mlima siku ya uhuru?jibu la karibu linapatikana katikati ya uasi wa mwaka 1964!Nyerere alipokuwa mafichoni na kambona alipojitolea kuzungumza na wanajeshi waasi;waliamua kubadilisha uongozi wa jeshi uliokuwa chini ya brigedia mwingereza na ndipo ilipoamuliwa ipite kura kati ya nani ataongoza jeshi na ndipo kati ya majina yaliyopita la nyirenda nalo liliinuliwa ila kwa mshangao lilipingwa vikali kwa tuhuma kuwa nyiranda ni wa kujisikia na mbinafsi!tuyaache ya uasi ila si siri kuwa nyirenda pamoja na usomi na sifa pia alikuwa mbinafsi na hakuwa wa kuaminika sio tu ya serikali hata wanajeshi wenzake hawakumpenda!fuatilia hata mazishi yake sidhani hata kulikuwa na ujumbe kutoka jeshini!kwa kifupi jamaa aliharibu na walishamtema!mbona wanajeshi wengi tu wamekufa na heshima zao!pia kuna waastafu mpaka leo wana sauti jwtz kwa kiwango cha kutisha kwa ajili ya heshima tuu waliyonayo huko!tusilaumu sana ila huko ndani wenyewe wanajua kwa nini ni hivi kwa nini ni vile!
 
Mzuzu,

..kitabu cha maasi ya 1964 kinawazungumzia maofisa wetu kama Sarakikya,Nyirenda,Kavana,Kashmiri etc na kuelezea nini kilitokea wakati ule.

..nakumbuka kusoma kwamba askari waasi walimfanyia fujo Captain Nyirenda na kumdhihaki kwa mambo mbalimbali. kama sijakosea askari waasi walimpakia ktk gari yeye na maofisa waingereza na kuwatishia kuwarudisha 'kwao.'

..Nyirenda aliendelea na utumishi jeshini hata baada ya maasi na alipanda ngazi mpaka kufikia cheo cha Luteni Kanali.

..yapo mahojiano aliyoyafanya miaka ya karibu na kifo chake ambapo anadai aliomba mwenyewe kuondoka jeshini kwasababu za kibinafsi. nadhani alidai wako ambao waliendelea kuyakuza yale yaliyomtokea wakati wa maasi ya 1964.

..RAISI MWINYI, KWA KUTAMBUA MCHANGO WA ALEXANDER GWEBE NYIRENDA, ALIMPANDISHA CHEO TOKA LT.COL KUWA BRIG.GENERAL.

NB:

..waasi wa 1964 'walimteua' Lt.Kavana kuwa Mkuu wa Majeshi na kumpachika cheo cha Brigadier.

..baadaye Kavana aliteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Chief of Staff/Mnadhimu Mkuu wa kwanza wa JWTZ akiwa na cheo cha Major. wakati huo CDF alikuwa ni Mirisho Sarakikya akiwa na cheo cha Brigadier.

..the highest non british officers wakati wa maasi ya 1964 walikuwa ni Capt.Kashmiri na Capt.Mirisho Hagai Sarakikya.

..wahusika wa maasi ya 1964 walipelekwa mahakamani na kuhukumiwa vifungo.
 
Back
Top Bottom