Lowassa: Wakining'oa NEC nitaeleza ukweli kuhusu Richmond

EL alisema wakimwaga mboga yeye atamwaga ugali. Aliahidi wakimuvua gamba yeye atawaonyesha watanzania mahali alipo BALALI. Hii ndio mimi naisubiri kwa hamu.
Hivi kumbe ni kweli alisema ataonyesha mahali Balali alipo?

Mimi nilidhani ni porojo tu za humu,kumbe kweli?

Basi ngoa nisubirie...
 
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima

Hana ukweli wowote anaoujua huyu mzee,anamtumia kibanda na gazeti lake kutishia nyau!angekua nao huo ukweli angeusema huko makanisani anako tanga tanga!
 
Kwa upande mwingine kama ni kweli EL alitolewa kafara,na wao wakamvua gamba,basi ana haki ya kumwaga mboga bila wasi wasi wowote ule.

Na hili ni ukweli endapo CCM na serikali yake walijuwa kuwa kama EL asingejiuzulu,basi mtafauruku mkubwa ungewakumba.

Naamini kabisa EL kumwaga mboga is a fair game...

Si log off wala nini!
 
hivi aseme na JK kwa kuwa rafiki yake amebanwakatibu wake na rafiki yake amebanwa atakosa yeye?
 
Ndicho nilichowambia Mkandara hicho,EL kashikilia kwenye kamali...Kutachimbika kama ni kweli,trust me!

Mwakyembe around or not,someone still holds the wild cards.

Kumbuka kulikuwepo na ripoti mbili na Mwakyembe aliitoa ile ya kumchafua EL...

Sio ya kumchafua lowassa utamchafua vipi mtu aliyechafuka tayari,aliitoa ile ya ukweli akaachana na ileya kupikwa,game hilo akalistukia yule mama aliyegombea ubunge kule arusha kwa tiketi ya ccm uchaguzu uliopita jina lake limenitoka,yule mama ni mtu wa lowassa ile mbaya,ndio akaenda kumstua mwanaume wao wa shoka lowassa kwamba ile ripoti ya kupikwa haitasomwa tena,mwakyembe kaamua kusoma ile ya ukweli,ndio lowassa kwa hasira akaona anazungukwa akaamua kuachia ngazi bila "kupima"
 
kama anaujua ukweli kwann acseme ukweli muda ule ilipojulikana?alikua anaficha nn?
Alijitoa mhanga kumlinda mkulu, kutokana na hilo ndiyo maana mkulu hana ubavu wa kumgusa Lowasa hata siku moja.
 
Sio ya kumchafua lowassa utamchafua vipi mtu aliyechafuka tayari,aliitoa ile ya ukweli akaachana na ileya kupikwa,game hilo akalistukia yule mama aliyegombea ubunge kule arusha kwa tiketi ya ccm uchaguzu uliopita jina lake limenitoka,yule mama ni mtu wa lowassa ile mbaya,ndio akaenda kumstua mwanaume wao wa shoka lowassa kwamba ile ripoti ya kupikwa haitasomwa tena,mwakyembe kaamua kusoma ile ya ukweli,ndio lowassa kwa hasira akaona anazungukwa akaamua kuachia ngazi bila "kupima"
Kama wote "walioga" kwenye tope la ufisadi, then ni kwanini yeye tu ndo achafuke?

Una uhakika kwa ukweli kabisa kuwa yeye peke yake ndiye resonsible for RICHMOND?
 
Tatizo ni uongozi wote wa CCM umeoza kuanzia kwa JK. Lowassa hawezi kutishia uhai wa CCM na wakabaki wanamuangalia tu, hapa lazima ujue kuwa uongozi wa juu ulishiriki kukamilisha huo wizi. Hata sielewi Magamba wanatumia vigezo gani kuonyesha Lowassa amechafuka wakati chama chote kimechafuka kuanzia kwa JK?

Itakuwa jambo jema kama JK ataamua kujiuzuru pamoja na uongozi wake, kisha kianze upya ukiwa na viongozi wengine wapya. Nafikiri hapo anaweza kujenga taswira yake na ya chama chake kuonyesha kuwa wanafanya mageuzi na si porojo za Magomeni kwa Macheni.
 
KIGUGUMIZI CHA CCM KUJIVUA GAMBA DODOMA INA UJUMBE KWAMBA HIYO SARATANI IMESAMBAA MNO MWILINI HADI IKULU KIASI KWAMBA HATA PA KUWEZA KUKATA ILI MGONJWA AENDELEE KUISHI JAPO KWA MATUMAINI HMNA

Wingi wa mafisadi ndani ya CCM kama ambavyo wengine wanavyodai hapa hata siku moja haiwezi fisadi aliyekamatwa tayari na wananchi dhambi zake zikayeyuka tu eti kwa sababu ni kosa lililotendwa na wana CCM wengi sana, hapana!!

Hata kama zaidi ya theluthi tatu ya wana CCM wangetuhumiwa kuwa ni mafisadi, na kiukweli ndivyo hali halisi inavyoonyesha siku zote katikaa vitabu vyeusi mikononi mwetu wananchi juu yao, lakini HILO PEKEE kamwe haliondoi ukweli kwamba zoezi la kuvua gamba ndani ya chama hicho lazima ianzie mahala na kila faili kupitiwa kwa wakati wake.

Kwa msingi huo, kama ambavyo CCM lenyewe tu lilivyojitokeza na kukiri kuchukizwa na gamba kati kati yake na kuanza kujikana kujisafish na tatizo hilo sugu ili KIWEZE KUPENDEKA TENA nchini, hadi hivi sasa macho yote ni kusubiri kitu gani kinachotokea kwa kufunuliwa kwa faili zao akina
Mafisadi waliokubuhu - Chenge na Edward Lowassa huko Dodoma.

Lakini kwa bahati mbaya sana CCM ikifanyia mzaha swala la Ufisadi na mafisadi huko kwenye kikao cha huko basi sote tuhesabu tu kwamba hilo ndilo litakalokua sanda na jeneza la kisiasa nchini.

Hili la Lowassa kulialia eti kwa nini asulubiwe WAKATI YEYE ALITUKWAPULIA WANANCHI SI KWA FAIDA YA FAMILIA YAKE BALI NI KULE KULITUNISHA DHANA ILE ILE YA 'MASLAHI YA CHAMA' ndio kwanza limeongezea kuchafua mambo zaidi kwa CCMmpaka dakika hii na CHADEMA sasa kuonekana kuwa ni wakweli kupindukia juu ya tuhuma zote juu hawa magamba.

Ndio, nasema mpaka hapo tu ni kwamba amefanya kesi yake iwe mbaya zaidi na wala sidhani kama hiyo CCM anayodai kuifaidisha na wizi huo kweli wWATAMWACHI JAPO KA-KIPENYO kwenda kusema nje kile anachokiita yeye UKWELI WOTE JUU YA UFISADI WA RICHMOND alias DOWANS au kwa jina lingine SI-MBIONI.
 
Siri yenyewe anayotaka kutwambia ni kuwa Richmond = Kikwete. Kwa hiyo kumvua gamba kwa kutumia Richmond ni kumtoa kafara.
 
kama angekuwa mwizi saa hizi angeshasahaulika kile kinachomfanya aendelee kuwa Lowasa hadi leo ndicho kinachoniaminisha yeye si mwizi bali kule kuachia kwake uwaziri mkuu kulikuwa kwa kujitolea tu. Alijitolea kuumia yeye ili wengine hata kama ni. wachache wapone. Binafsi ninamheshiimu kwa hilo.

Nyie wengine mnaugua ugonjwa wa LOWASANIOSISS akikosekana hali yenu inakuwa mbaya ndio wote mafisadi nyie,kwani nyerer alikuwa mjinga?
 
Lowasa bana, anazeeka vibaya sana; anatuambia kuwa anasiri kubwa ya ukweli wa Richmon, na anajua kuwa tunachokifaham sisi Watanzania wa kawaida kuhusu Richmond ni uwongo wa maksudi!

Kwa kitendo chake cha kuwaficha watanganyika ajue ni kushiriki uhalifu! Tukilegeza kamba huyu jamaa atakuja kuwa raisi wa Tanganyika Miaka michache ijayo, na nina hakika ataendeleza siasa na utendaji wa kulindana kimakundi kama anavyofanya Mkweere! Simwamini hata kidogo huyu mzee.

yaliyomtokea mwakyembe ni matokeo ya kutudanganya na kutuficha watanzania. Tunashindwa kumwombea apone maana alipewa dhamana ya kuchunguza uovu wa richmond akatuficha mengine kuilinda serekali yatamkuta tu hata huyo lowasa
 
Kama ni kweli then alishiriki wizi na yeye ni mwizi miongoni mwa wezi wa nchi hii na amekuwa akiiba kushirikiana na wezi.
Hata hivyo, siku zote hata rafikiye ambaye hawakukutana barabarani nafahamu kuwa naye ni mwizi tu na mchora ramani za wizi pia.
 
If that is the case. Here is my free consultancy to EL. Keep quiet, fight for that post quietly. Discipline them when you get there, or keep quiet if you wont get there.
 
Alikuwa wapi siku zote kueleza hilo?? Huu nao ni upuuzi. Sio mzalendo ni mchumia tumbo,
...........naam, single kama ya Mh. Mwakyembe kwamba nikirudi nitafyatuka kila kitu; sasa hawa watu nani ana ukweli? wabongo kwa unafiki bwana
 
Hawawezi,na wakija humu,watajibu posti ambayo iko nje kabisa ya mjdala ili kuonyesha sura tu na kuingiza siku,basi.
.........ni kweli, siku mkuu wa kaya akiongea na wazee(sijui safari hii watakuwa wa wapi), utakimbia upupu wa post zao!!!!!
 
Back
Top Bottom