LOWASSA Vs CCM: CCM Wakati Ni Sasa Wa Maamuzi Magumu ya Kusuka au Kunyoa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LOWASSA Vs CCM: CCM Wakati Ni Sasa Wa Maamuzi Magumu ya Kusuka au Kunyoa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Nov 26, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Well, sasa umefika wakati wa Serikali ya CCM kuamua moja either kumuachia Lowassa Serikali, au kuridhisha Katiba na kuwa Serikali halali iliyochaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri. I mean what has gone wrong na hili taifa? Kila kukicha it is Lowassa and Lowassa, and Lowassa and Lowassa! What is wrong na CCM? I mean how much money does this man has ambazo toka tumeanza kumsikia akizitumia ku-manipulate our politics haziiishi tu na wala hazithibitiwi na Serikali on uhalali wake?

  - CCM ifike mahali sasa tuambiane ukweli, kama we can't stop this man basi tumuachie hiii Serikali kuliko hizi never ending Dramas behind the Scene, WHY? Who is this man? Huku US kuna wakati kulikuwa na Mafia John Gotti, na yeye aliizidia sana Serikali mpaka Rais Clinton, akaamua uamuzi mgumu na kumfunga kwa kuizunguka Sheria, ili kuirudishia heshima na Legitimacy Serikali, Serikali ya CCM inaanza kukosa Legitimacy kwa sababu ya this one man, basi ifike mahali ikubali kushindwa na kumpa anachokitaka yaani URAIS, maana hii sasa imekua kero isiyokwisha na inakimaliza chama mwisho itamaliza hata taifa!


  MUCH RESPECT PEOPLEs!


  William @...NYC, USA: Mutuz Le Baharia!
   
 2. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,401
  Likes Received: 1,525
  Trophy Points: 280
  ....kwani ni nani hasa wanaoteswa na kivuli cha Lowassa, tunaimbishwa huu wimbo Lowassa! Lowassa! kila kukicha, Lowassa ni Fisadi, sawa tunaaminishwa hivyo, kisa Richmond, Lakini sakata linavyokwenda linaonyesha mkuu wa kaya naye yumo, anajua kila kitu, kwa nini tusimwambie aige na hili la kuachia ngazi aachie wengine wachape kazi???? hatuna sababu ya kumwogopa Lowassa, tunaomwogopa ni kwa ajili ya umaskini wa mawazo yetu,
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Willam usipate shida, JK na Lowasa ni chanda na pete. Kidogo walitaka kuachana katika sakata la Richmond lakini kwa hali ilivyo ni wazi JK ameshindwa kuhimili vishindo vya Lowasa.
  Muasisi wa kujivua gamba ni mwenyekiti lakini ameshindwa kulivua gamba hilo hali inayopelekea nadharia hiyo kuwa ngumu kama atomic phsysics vile!!!!!
  Kitakacho mzuia kushika urais Lowasa ni nguvu ya wananchi pekee na siyo CCM. Hili linatachagizwa na kuvurunda kwa JK urais 2015. Hasira za wananchi zitakuwa kubwa juu ya serikali ya kisaliti ambapo kufika 2015;

  1.0 Mfumuko wa bei utakuwa mkubwa hali itayoongeza makali ya maisha
  2.0 Ukosefu wa ajira utaongezeka mara dufu na kufanya vijana waichukie serikali yao kupindukia
  3.0 Serikali kushindwa kusimamia baadhi ya mambo muhimu na kuibuka kwa ufisadi mkubwa utakopelekea kuundwa kwa tume nyingi kama za akina Jairo
  4.0 Nyota ya upinzani kuzidi kung'aa kutokana na umahiri wa kujenga hoja na kuonyesha tumaini jipya kwa wananchi

  Ni kipindi hicho ndg Lowasa atakapojaribu bahati yake na kukumbana na nguvu kubwa ya umma itakayokuwa imemkataa na kuwa mwisho wake kisiasa kwani CCM wameshindwa kumdhibiti.
  We inafikia mahali kusema kumfukuza mtu kunaweza kuua chama!!!! Je akifa ina maana na chama kimekufa? Basi huyo anaweza kuwa ndiye mungu wa CCM!!!!
   
 4. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,401
  Likes Received: 1,525
  Trophy Points: 280
  .............................................................
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu mimi nadhani udhaifu wa JK kiuongozi uliotokana na kuingia madarakani kwa "fedha chafu" ndiyo kiini cha tatizo. Walewale waliompa JK uraisi ndiyo hao wanaplay behind the scenes kum-promote Lowassa. Na sasa EL amemuweka JK kwenye zone ya kuonekana defensive akiongelea lolote kuhusu ufisadi wa Lowassa. JK is being defeated by his own records.

  Lakini pia huu utaratibu wa kitanzania wa kutomkosoa na kumuonya "mkubwa" ndiyo unaoi-cost CCM sasa hivi na taifa kwa ujumla. Hawa hawa wanaompigia makofi na vigelegele JK leo utawaona watakavyoanza kumponda watakapokuwa wanawania uraisi 2015. They will start pretending wako pamoja na ss wananchi, JK did nothing (kama vile wao hawakuwemo).
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Mkiwaruhusu waingie ikulu hawa vijana wawili watawasumbua sana" By JK NYERERE.
  Hasie sikia la mguu, uvunjika guu, Nyerere aliposema Kikwete bado mdogo 1995 hakumaanisha umri, kwani Nyerere alichukua Tanganyika akiwa na umri mdogo wa zaidi aliokuwa nao Kikwete wakati anaomba kuwa mgombea wa CCM mwaka 1995.

  Kinachoendelea sasa hivi ni laana ya kutomsikiliza yule mzee na kupima kwa makini pale aliposema ikulu sio sehemu ya kukimbilia ni mzigo mzito, sasa hawa wanaoitaka ikulu kwa gharama yoyote wana miradi yao wanayotaka kufanya pale.
  Na kuanzia leo sipendi unafki wa kumtaja Lowasa bila Kikwete kuhusika, Kikwete ndio gamba namba moja ndani ya CCM na nini yeye ndio ameikisha nchi hii hapa ilipo. huyu ni Rahisi na sio Rais.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mimi nafikiri unaposema kuwa anatumia pesa ku manipulate na unapomfananisha na mafia John Gotti
  hapo panahitaji zaidi ufafanuzi...na kueleweshana.....

  sio wote tunaoujua kwa uhakika habari hizo..
  wengi tunasikia sikia tu....give us more details...
   
 8. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  tia chaka Lowassa hana mpango wala nini. Nalog off
   
 9. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu Willy,
  Heshima sana kaka.
  Waswahili wana usemi usemao "zimwi likujualo halikuli likakwisha" Kinachoitesa ccm na Bongoland yetu ni hila za urais wa Kikwete zilijojengwa na pesa na ubaguzi wa matabaka ya watu ndani ya ccm tangu pale kura zilipogoma kutosha na mzee Mkapa kuchukua Uongozi. Recently rafiki yako Nape alibeba bango nchi nzima akipigia kelele usafi wa chama, mkuu wa kaya akasikika akisema yale anayosema Nape ni ya chama, leo kageukwa na yuko kwenye hatari ya kumwagwa. I don't expect anything good from ccm,
   
 10. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Ingekuwa Jambo jema kama mkuu wa kaya angedhibitisha kwenye KHK kuwa hawajui Richmond na wala hakupigiwa simu na wala hakujua serikali yake inafanyanini kutatua tatizo la umeme. Vinginevyo Mkuu wa Kaya ndio tatizo kama anashimdwa kuchukua maamuzi magumu ikiwa ni pamoja na kupisha kama ameshindwa.
   
 11. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Humo ndani hamna wa kumgusa Lowassa hata mmoja, mkuru mwenyewe anaonekana mpole kwa lowassa maana anajuwa akiongea tu au kufanya jambo lolote basi kila kitu kitaharibika humo ndani, kwa ujumla huyo jamaa ni kama ameishika CCM kwa kiwango kikubwa sana....
   
 12. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ccm hawana uwezo wa kumuwajibisha Lowasa kwani tatizo ni Kikwete,ushindani wa kugombea urais ndani ya ccm 2005
  ulikua mkubwa kiasi kwamba Kikwete kwa uwezo wake asingeshinda, mtandao wa swaiba wake yaani Lowasa ndiyo uliomweka Kikwete madarakani kwa makubaliano kwamba baada jk afuate el, hvyo kumuondoa el ccm ni ngumu sana kwani el ule mtandao wake bado ni mkali sana,wajumbe karibu wote wa vikao vya maamuzi ndani ya ccm ni mtandao wake,dogo Nape angejua haya asingekua anabweka hovyo.
   
 13. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Huna unalojuwa.
  uwepo wako hauna faida yoyote.
  Ni sawa na Nyusi ktk mwili wa Binadamu.
   
 14. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wana JF, nimekuwa nikilisema hili mara kwa mara (fuatilia posting zangu za nyuma kuhusu Lowasa) kwamba Lowasa hakupewa muda wa kujieleza mbele ya tume ya akina Mwakyembe. Kila mtuhumiwa aliitwa kujieleza mbele ya tume na wengine walifuatwa mpaka America, lakini cha kushangaza zaidi Lowasa hakuitwa wala kupigiwa simu na tume husika na wakati ofisi ya Lowasa haikuwa mbali na ofisi ya tume husika.

  Lowasa kama angeitwa mbele ya tume basi haya anayoyasema leo ndani ya vikao vya CCM angeliyasema mbele ya tume na ukweli ungelijulikana mapema sana. Na pia ikumbukwe kwamba katika ripoti Mwakyembe alisema kuna mengine hawezi kuyasema kwa kuifichia siri serikali. Alikuwa na maana gani kusema hivyo wakati sisi walipa tumetoa pesa zetu ili uchunguzi wa kina ufanywe na tupewe ukweli bila kuficha?. Ninarudia kusema na nitarudia kusema kwamba Lowasa alionewa, hakutendewa haki, alifanywa mbuzi wa kafara.
   
 15. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu Willy, this is now becoming a tragedy.

  Wananchi wa TZ hatuwezi kuwa na Rais aliyechaguliwa, halafu mtu mwingine nje ya katiba akacontrol serikali ( CCM ni chama Tawala, so kucontrol CCM ni kucontrol Serikali).

  Vyombo vya usalama hii ndio kazi yao kubwa kuprevent, lakini wao wanahangaika na Chadema. Rais hawezi kudharaulishwa halafu mkategemea serikali kurun. Sasa ukiwa kwenye position ya power, halafu fisadi Lowassa anataka mchongo kama ilivyo kawaida yake, utafanya nini?? Unajua yeye ana nguvu kuliko Rais, HELL NO, THIS HAS TO STOP NOW.

  Sasa huyu mtu anatudharau wananchi wote, kama ana nguvu za kumdharau JK kwenye NEC mbele ya wajumbe wote, hii ni KASHFA kubwa.

  JK, please tuondolee huu upuuzi, ebu safisha watu wote wanaompa huyu mtu kichwa walioko serikali na kwenye chama, anza na DPP Feleshi, halafu weka mtu atakaye anza na kumpa Fisadi Lowassa kesi mbalimbali za ufisadi, awe busy huko mahakamani ili hii Futile ndoto ya urais iishe na nchi tudeal na mambo mengine ya maendeleo. ENOUGH IS ENOUGH.
   
 16. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Issue hapa siyo Lowassa vs CCM, ni Lowassa vs Kikwete.
  1. Lowassa ametuambia kwamba hiyo Richmond inayotaka kutumiwa ili kumhukumu siyo yeye bali ni JK. Kwa hiyo kumhukumu yeye ni kumwonea.
  2. Ikumbukwe kwamba JK na EL wameshatuambia kwamba ni marafiki. Huo urafiki ndio ulipelekea waachiane ugombea 2005. Lakini kwa makubaliano gani? Simply say: "Nenda wewe (JK) sasa hivi (2005), ukimaliza nakuja mimi (EL) 2015.
  3. Tatizo linakuja kwamba JK ametaka kutumia skendo yake, ambayo iliyomfunya EL kujiuzulu U-PM ili kumlinda rafiki yake asiumbuke, JK ametaka kuitumia hiyo hiyo ili kumtwanga nayo rafiki yake na kumpiga pembeni. ndo maana kumekuwa na tetesi kwamba mkulu ameanza kupigia ndogo ndogo watu wengine kuelekea 2015.
  4. Lowassa is using all the means he has to fight back.
  Tutaendelea kuona mengi huko mbele tuendako.
   
 17. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  All in all Finally Honorable Lowassa atakuwa amiri jeshi mkuu wa taifa hili...

  Tuseme inshaalah
   
 18. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  manywele ni choli sana wampe nafasi ya kugombea uraisi tuipige puuu ccm mazima, ppls.... power....
   
 19. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Nimetoka kumjibu mwenzio mmoja aliyekurupuka na kudai kuwa Muheshimiwa Lowassa ni fisadi, mwizi, na upuuzi mwengine kuwa atafute mawakili kisha wakamshtaki....na sio kuja kuleta porojo zenu hapa wakati njia husika za kumshughulikia mtu mwenye sifa hizo mnazompa mnazijuwa.
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Siku moja nimesafiri na mama mkimbizi kutoka Sierra Leone kwenye metro. Nilizungumza naye kuhusu hali nchini mwao ambako waasi wa kundi la RUF walikuwa wakiwakata raia mikono, masikio na viungo vinginevyo vya mwili. Nikamwuliza, je, unadhani suluhu ya tatizo la Sierra Leone ni nini? Akajibu, ni kuwaachia waasi wachukue serikali. Angalau wataacha kukata watu mikono. Naona na sisi Tanzania tumeshafikia hali hiyo. Lowassa, kwa kutuibia na kutajirika kwa kutumia migongo yetu, hivi leo hana tofauti na waasi wa RUF. Kwa Watanzania waliokata tamaa watasema kwamba njia pekee ni kumwachia Lowassa uongozi wa nchi. Lakini kwa Watanzania wenye matumaini, nikiwemo mimi, tunasema kuwa Lowassa hatufai. Hafai kuwa kiongozi wa Tanzania inayoelekea karne ya 21. Ameiba vya kutosha, amedhulumu vya kutosha abaki na mali zake lakini hafai kuwa kiongozi wa nchi. Tanzania deserves better.
   
Loading...