Wakati CCM wanaona kabisa jinsi ambavyo hakuna uwanja sawa wa kufanya siasa, harakati zote za kisiasa ni za Nini?

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Kwa kuwa nimejizoesha kufanya tafakuri tunduizi katika mambo yangu mengi, hapa nyuma nimeanza kujiuliza, harakati, mikakati, na nguvu yote wanayotumia CCM ni ya nini?

Mimi ninapoona uwanja wa kufanya siasa vile ulivyo, hakuna kabisa haja ya kusumbuka kujijenga na harakati nyingi wanazofanya maana ushindi ni wao.

1) wao ndo wanaamua Kasi yako ya kufanya siasa iweje ( kumbuka Zanzibar jinsi ambavyo mgombea wa ACT alikuwa keshaondolewa kimbinu) Sasa kwa kuwa wao ndo regulator wa mazingira ya kisiasa, nguvu zote hizi na harakati ni za nini? fulana, ngoma, kusafirisha watu mikutanoni nk vyote ni kwa ajili gani?

2) Vyombo vya Dola polisi, na vingine vinavyoandaa michakato ya ushindi wa CCM vyote vinacheza muziki wao. CCM wakisema tumetukanwa, kesho wapinzani, ambao tunadhani ndiyo washindani wa CCM, wananyimwa kibali Cha kufanya mikutano au wanazifanya siasa kwenye mazingira ya kusimamiwa kunakoondoa uhuru wa kuzifanya hata hizo siasa zenyewe.

3)Government machineries zote zinakuwa professional tu wakati CCM hawajaingiza mguu mahala, ikiwemo na tume ya uchaguzi.

Niambieni katika mazingira haya , jitahada na harakati zote ni za nini wakati fika wanajua wana Kila uwezo wa kushinda inapofika kwenye uchaguzi?

Hivi wanashindana na nani? Hawa wapinzani ambao wamebanwa Kila mahali kwa mifumo na wakati mwingine hila zikiwemo?

Nashauri pesa wanayotumia kujitangaza sana hivi, mikakati ya Kila siku ya kutafuta ushindi kana kwamba kweli wanashindana, waachane nazo.

Maana wanajua na wanafahamu kwamba Kila kitu hapa ndani kinawabeba. Iwe tume, polisi, wakurugenzi, msajiri wa vyama vya siasa, na hata wapinzani uchwara, wote wako nyuma yao. Kama ni hivi, harakati zote hizi ni za nini? ( why spend your resources in vanity?)

Kama mazingira ya kisiasa yamewafunga wenzenu namna hii, si mngepumzika tu. Hiyo pesa Sasa ya kujiharisha kuwa chama Cha kawaida Cha siasa mngewapelekea wananchi maendeleo.

Kwangu Mimi haya ni masumbwi ambayo bondia mmoja( CCM) anajua kabisa, siku ya mpambano mwenzangu( UPINZANI) atakuwa kafungwa mikono yote miwili na kamba. Sasa mazoezi yote haya ya kujiandaa kwa pambano ni ya nini?

Naomba dhamiri ziwasute kidogo CCM. Kama kweli mnataka kufanya siasa, achieni na wenzenu wafanye hizo siasa kama ninyi, achilieni raia watoe maoni yao kikamilifu, achieni vyombo vya dola viwe dola kweli na msikimbie huko kwa msaada .

Mkishinda katika mazingira hayo, mna haki ya kutamba kuwa chama dume. Mkitamba Sasa ni chama dume, kimemshinda dume gani mwingine kwa haki?

Let's apply the law of proportion. Harakati ziendane na upinzani halisi, ulioachiliwa ( not tactfully bound)na siyo kutamba na kutumia nguvu nyingi wakati hakuna equal proportion kwenye kufanya siasa.

Keep your energy and resources my ruling party, don't lose it for no good reasons.
 
Back
Top Bottom