NDOTO YA LOWASSA KUWA RAIS KUPITIA UPINZANI ITAKUWA SAWA NA KUINGIA PEPONI KWA IMANI ZA KISHIRIKINA.
Hadi kufikia maamuzi ya kamati kuu ya (CC-NEC) ndani ya chama cha mapinduzi kukata jina la Edward lowassa ni dhahili kabisa hawakukurupuka, walitathimini madhara na faida ya kumuengua ndugu lowassa, walitathimini uwezekano wa yeye kukihama chama endapo atakatwa na wakajiandaa vilivyo kukabiliana naye,
MIZIZI iliyo simikwa na MWINYI,MKAPA NA KIKWETE haiwezi kung'olewa na vyama dhaifu vya upinzani tulivyo navyo Tanzania, CCM ina siri nyingi nzito za lowassa, akithubutu kuhama ndo kajimaliza mwenyewe, kutokana na nguvu iliyopo nyuma ya mgombea wa CCM ni ngumu kwa Lowassa kushinda Urais hata kama kura zingepigwa nyumbani kwake tu,
HATA KAMA UWE UNAPESA KIASI GANI HUWEZI SHINDANA NA MWENYE DOLA, kuwa kinyume na mwenye dola ni sawa nakuingia mgogoro na nafsi yako mwenyewe, wanaomshauri lowassa ahame CCM wanampoteza kabisa, atafilisika zaidi ya mrema, Lowassa akithubutu kuhamia upinzani hawezi kupambana na mgombea yeyote wa CCM hata awe WEMA SEPETU,hii ni kutokana ngome kubwa iliyopo.
Lowassa anachotakiwa kufanya ni atulie tu aendelee kula pensheni siasa baasi!