Lowassa, Sumaye wamponza Mhariri wa Gazeti la Nipashe

Kama ni kweli walifukuzwa kazi sbb ya kupokea rushwa kwa ajili ya kuwasafisha mafisadi mimi mnampa pongezi bwana Mengi kwa kuwa mstari wa mbele kupigana vita ya ufisadi u aosababisha maumivu hasa kwa sisi wananchi wa hali ya chini.
 
Mengi amechukukia labda kwa ajili ya Sumaye lakini sio Lowasa. lakini hata hivyo si nasikia Mengi ananyanyasa sana watumishi tofauti na anavyojifanya kutoa misaada kwa watu wasiojiweza, lakini kumbe ni kafara tu (Free mansory)
 
Huyu Mzee kumbe nae ni mmoja wao hao wenye Magamba! Ukimuona anaongea utadhani ni mtu mtaratibu na mnyenyekevu kwa watu kumbe nae ndi walewale. Hatari hakuna mahali pa kuponea

Pamoja na kwamba mtoa mada hajatoa source ya kueleweka nashawishika kuikubali hii habari kutokana na yale niliyaona jana kwenye taarifa ya hbr ya 2 usiku ya ITV. Msoma habari alikuwa akisoma habari kuhusu Chadema akamweka Mbowe kidogo then ikaja habari kuhusu Dr. Slaa na "huyo anayeishi kimjinimjini" ni kama vile walitaka kumweka Slaa then wakagundua kwamba ni kosa wakaipotezea hiyo hbr na kuweka tangazo. ITV big shame on you!
 
Watu muache kushabikia kitu ambacho hamkifahamu. Huyu mhariri pamoja na huyo Bandawe na kikundi cha wahariri kadhaa walikuwa na mkutano uliodumu mpaka usiku wa manane pale Ubungo Plaza na ajenda ilikuwa ni kutengeneza utaratibu wa kuwasafisha watuhumiwa wa ufisadi na baada ya kufanya kikao hicho na kukubaliana, walipewa mshiko wa nguvu ambao hata ulipofuatiliwa, wengine walikutwa nao kwenye akaunti zao wakiwa wame-deposit siku hiyo hiyo. Mzee Mengi kama mmiliki wa vyombo vya habari amabvyo hapendi viingie katika upuuzi huo wa kugeuza ukweli kuwa uongo kwa vipande thelethini vya fedha akafanya uchunguzi na hatimaye kuwachukulia hatua tena baada ya wenyewe kukiri kuhudhuria mkutano huo. Kwa suala hili la kukiuka misingi ya utumishi na makubaliano ya ajira, ni nani angesamehe, tena vyombo vyako kusafisha na kuwaimbia mapambio mafisadi tena mahasimu wako?

Mimi nadhani miaka yao mingi ya utumishi ilitakiwa iwafundishe uadilifu na siyo kutumia nafasi ya kukubalika na kuaminiwa kwao kupotosha umma. Mambo haya si mageni kwa wamiliki wa vyombo kwani hata ukiuliza akina Mwakitwange, Tagalile na akina Kwayu waliondokaje Habari Corporation? Mbona hakuna aliyepaza sauti? Mzee Mengi anastahili kupongezwa kwa kuondoa mbegu mbaya hata kama watu hao walikuwa na weledi wa hali ya juu katika uandishi wao.

Lakini hata tukidhani kwamba kosa ni kuandika habari za Mtikila (ambayo si kweli), kuna ubaya gani kwa mmiliki kumuwajibisha mwandishi anayeandika habari ambazo huko mbeleni zitasababisha madai ya kashfa yanayoweza kukiweka chombo cha habari na mmiliki matatani? Kwa vyovyote vile atakayekwazwa na habari hizo hawezi kumshtaki Mtikila ambaye ni mchovu na hana heshima mbele ya jamii zaidi ya kuwa ni jeshi la kukodiwa. Bingo ingetafutwa kwa watu wanaomiliki vyombo kama Mzee Mengi. Na hii ndiyo maana wenyewe wamekauka kau! Wanajua dhambi zao.
Mbopo, nakushukuru kwa ufafanuzi na kukunga mkono watu wasishabikie vitu wasivyo fahamu.
Pamoja na ufafanuzi wako, hoja yangu inabaki pale pale kuwa hayo yaliyo wakuta ni ya kawaida hapo!.
Mifano ya Mushi, Urasa, Sakina etc inatosha ku determine trend.

Naamin hata kina Kwayu na Mshana hili wanalijua na watakuwa mamesha jiandaa kisaikolojia kwa zamu zao!.
 
kumbe huyo mzee naye gamba, duh na kelele zote zile na mafisadi papa tena muda wa taarifa ya habari.
kama ni kweli basi huu ni muda wa kuanzisha trade union zinazoeleweka. kutetea wafanyakazi

Mlisha ambiwa nae ni fisadi nyangumi mkabisha mmeona sasa!!
 
Mlisha ambiwa nae ni fisadi nyangumi mkabisha mmeona sasa!!

Hivi una-determine mtu kuwa fisadi nyangumi or otherwise kwa kuchukua hatua dhidi ya kile ambacho yeye anadhani ni kwenda kinyume na philosophy ya uendeshaji wa biashara yake? Watu waelewe kwamba huyu jamaa amechukua hatua dhidi ya ufisadi na kama mmiliki wa vyombo hivi na mwajiri ana haki ya kufanya hivyo, bila kujali watu watasema nini. Mimi nashangaa kuona watu wanashangilia kuona watu wanatumia kalamu zao kuendeleza uovu na kutukuza ufisadi na hatimaye kuipotsha jamii na kuonyesha kwamba watu hao (mafisadi) wanaonewa kumbe wamewekwa sawa ili kufanya upotoshaji. Katika hili Mengi anastahili sifa kwa uzalendo wake.

Hao akina Datoo, Mushi na Urassa ni case tofauti na pengine watu wametoa uamuzi ama kwa kuzingatia hisia au kwa kusikiliza maelezo ya upande mmoja. Hili suala la kulipwa mishahara midogo au kuchelewesha mishahara ni la kawaida sana. Infact kule Habari Corporation hali ni mbaya zaidi pamoja na kwamba mmiliki wake ni fisadi anayekwapua mabilioni kila kona ya hazina yetu.

Ukweli unabaki kwamba waandishi wale wamejichumia janga wao wenyewe na sharti janga hilo walile na mafisadi waliowaingiza mkenge huo. Impunity has no place in our society any more!
 
achakupenda maandamano kuliko akili zako ww mbona mlimfukuza hausgel wenu alipokataa kukuletea chai chumbani nani kakushutumu?

Hapa nashindwa kucconect thread hii na comment ya huyu mwenzetu, mwenye uwezo wa kuchambua kiswahili vizuri labda atusaidie huyu mwenzetu ana hoja ipi kwenye thread hii?
 
..............................................................................................

Mjifunze jamani kazi za watu na malengo yao, Mengi ni CCM damu, ni fisadi mzuri tu, lakini watanzania kama kawa wamepumbazwa!........................................................................................................

That is it!
 
Pamoja na kwamba mtoa mada hajatoa source ya kueleweka nashawishika kuikubali hii habari kutokana na yale niliyaona jana kwenye taarifa ya hbr ya 2 usiku ya ITV. Msoma habari alikuwa akisoma habari kuhusu Chadema akamweka Mbowe kidogo then ikaja habari kuhusu Dr. Slaa na "huyo anayeishi kimjinimjini" ni kama vile walitaka kumweka Slaa then wakagundua kwamba ni kosa wakaipotezea hiyo hbr na kuweka tangazo. ITV big shame on you!

Hiyo ni speculation. Hata hivyo hana obligation ya kutangaza kitu ambacho asingependa kitangazwe kwa sababu afterall yeye ni mmiliki binafsi wa kituo cha TV. Hata hivyo, CDM hudhani kwamba TV au magazeti yanayowatangaza wao ndiyo mahiri au ni ya kizalendo lakini mbona kuna upotoshaji wa kupitiliza katika Tanzania Daima na ndiyo gazeti hilo ambalo sasa limegauka kuwa mdomo wa mafisadi na bado CDM iko kimya? Na ajabu ni kwamba mafisadi hao hao waliodai mwaka mmoja uliopita kwamba Mengi ni mwanachama wa CDM. Huoni kwamba kuna ajenda hapo?
 
Watu muache kushabikia kitu ambacho hamkifahamu. Huyu mhariri pamoja na huyo Bandawe na kikundi cha wahariri kadhaa walikuwa na mkutano uliodumu mpaka usiku wa manane pale Ubungo Plaza na ajenda ilikuwa ni kutengeneza utaratibu wa kuwasafisha watuhumiwa wa ufisadi na baada ya kufanya kikao hicho na kukubaliana, walipewa mshiko wa nguvu ambao hata ulipofuatiliwa, wengine walikutwa nao kwenye akaunti zao wakiwa wame-deposit siku hiyo hiyo. Mzee Mengi kama mmiliki wa vyombo vya habari amabvyo hapendi viingie katika upuuzi huo wa kugeuza ukweli kuwa uongo kwa vipande thelethini vya fedha akafanya uchunguzi na hatimaye kuwachukulia hatua tena baada ya wenyewe kukiri kuhudhuria mkutano huo. Kwa suala hili la kukiuka misingi ya utumishi na makubaliano ya ajira, ni nani angesamehe, tena vyombo vyako kusafisha na kuwaimbia mapambio mafisadi tena mahasimu wako?

Mimi nadhani miaka yao mingi ya utumishi ilitakiwa iwafundishe uadilifu na siyo kutumia nafasi ya kukubalika na kuaminiwa kwao kupotosha umma. Mambo haya si mageni kwa wamiliki wa vyombo kwani hata ukiuliza akina Mwakitwange, Tagalile na akina Kwayu waliondokaje Habari Corporation? Mbona hakuna aliyepaza sauti? Mzee Mengi anastahili kupongezwa kwa kuondoa mbegu mbaya hata kama watu hao walikuwa na weledi wa hali ya juu katika uandishi wao.

Lakini hata tukidhani kwamba kosa ni kuandika habari za Mtikila (ambayo si kweli), kuna ubaya gani kwa mmiliki kumuwajibisha mwandishi anayeandika habari ambazo huko mbeleni zitasababisha madai ya kashfa yanayoweza kukiweka chombo cha habari na mmiliki matatani? Kwa vyovyote vile atakayekwazwa na habari hizo hawezi kumshtaki Mtikila ambaye ni mchovu na hana heshima mbele ya jamii zaidi ya kuwa ni jeshi la kukodiwa. Bingo ingetafutwa kwa watu wanaomiliki vyombo kama Mzee Mengi. Na hii ndiyo maana wenyewe wamekauka kau! Wanajua dhambi zao.

Khaa!!! :busu
 
Nchi imeanza kuvurugika tayar ila ccm mngeondoka vyema kuliko dalili izi maana mkianza kufukuzisha watu kwakua mnaficha maovu yenu isaidie mabadiliko yatakuepo iwe kwavi au vip ukawa ndo mshindi na si mchezo
 
Mkuu hii habari ni ya 2011. Hawa wanamama walisharudi kazini kitambo
 
Samahan mi siko nchini ila na machungu na taifa langu watu wameendela watu wana maisha mazuri si kwajili ya utajiri wao bali ni mifumo mizuri yakisiasa chama kukaa miaka 50 madarakani definitely wanaona kama inchi ni yao ndo maana wanatukana ccm hamfai, hamtufai, na hatuwaitaji tena
 
Suala la trade union litategemea kama ajira zao ni za mdomoni au za maandishi kwa maana ya employment contract.
Pili kuwa mfanyakazi wa mengi kunataka moyo sana kwa sababu yeye ndiye bosi pekee anayeingiliaga utaratibu wa kazi.
Pole sana mdau. Nadhani mda wenu wa kuhama kazi umefika.
 
Fatma Almasi Nyangasa hebu mshauri huyu Mama aje huko muanzishe Azam Gazeti.Gwiji liko huko mambo yanawezekana
 
Wana Jf kuna taarifa za bila kuwa na shaka Muhariri Mkuu wa Gazeti la Nipashe Jumapili Mama Flora Wingia na Muhariri wa Habari Bi Bandawe wamesimamishwa kazi kwa Kosa la Kuandika Story jumapili iliyopita inayohusu Tuhuma zilizotolewa Na Mchungaji Mtikila Dhidi ya RIDHWAN KIKWETE,wamesimamishwa kazi kwa kosa hilo.

Kosa la Pili ni kuandika Maoni juu ya Urais 2015 kuwa ni kati ya Lowasa na Sumaye ndani ya CCM,mambo haya mawili yamemuudhi sana Mwenye mali na wao kusimamishwa kazi siku ya IJUMAA maamuzi haya yalifanyika bila kufanyika kikao chochote cha Kinidhamu kujadili kama wamekiuka maadili ya uandishi ama kama wamekiuka sheria za chombo chao za habari.

My opinion barua zao zimesema hivo wazi najiuliza kosa la muandishi ama muhariri nini hapo kwani mtikila alituhumu wazi na kila chombo kiliandika,kuhusu maoni yale ni maoni ya muhariri na si siri tena CCM kuwa sasa inakabiliwa na Vurugu zinazotokana na URAIS wa 2015 ,wanahabari kama wananyanyasika hivi huyu mama Wingia amefanya kazi zaidi ya miaka 10 ni FOUNDER wa Gazeti la nipashe sisi waandishi wadogo tuna Future gani hapa nani yuko salama,wanahabari tuungane kupinga hili ni uonevu.
Tuache kuandika hisia ya usichokitaka, tafuta habari/undani wa jambo bila kukurupuka. Fanya uchambuzi, tulia na tafakari bila ya kuwa na mhemko. Kumbuka kufanya kazi muda mrefu haimaanishi huwezi kutenda kosa litakalo hatarisha sio tu kazi bali hata future yako, either uwe muhariri au mfanyakazi yeyote hata wa ndani....kama walikiuka maadili lazima wachukuliwe hatua otherwise tuache kulalamika lalamiko. Wangeachwa ungelalamika, wamechukuliwa hatua umelalamika......kumbuka kusimamishwa kazi ni mojawapo ya adhabu wakati uchunguzi ukiendelea.
 
Back
Top Bottom