Lowassa, Sumaye wamponza Mhariri wa Gazeti la Nipashe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa, Sumaye wamponza Mhariri wa Gazeti la Nipashe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUA GAMBA, May 8, 2011.

 1. M

  MVUA GAMBA Senior Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wana Jf kuna taarifa za bila kuwa na shaka Muhariri Mkuu wa Gazeti la Nipashe Jumapili Mama Flora Wingia na Muhariri wa Habari Bi Bandawe wamesimamishwa kazi kwa Kosa la Kuandika Story jumapili iliyopita inayohusu Tuhuma zilizotolewa Na Mchungaji Mtikila Dhidi ya RIDHWAN KIKWETE,wamesimamishwa kazi kwa kosa hilo.

  Kosa la Pili ni kuandika Maoni juu ya Urais 2015 kuwa ni kati ya Lowasa na Sumaye ndani ya CCM,mambo haya mawili yamemuudhi sana Mwenye mali na wao kusimamishwa kazi siku ya IJUMAA maamuzi haya yalifanyika bila kufanyika kikao chochote cha Kinidhamu kujadili kama wamekiuka maadili ya uandishi ama kama wamekiuka sheria za chombo chao za habari.

  My opinion barua zao zimesema hivo wazi najiuliza kosa la muandishi ama muhariri nini hapo kwani mtikila alituhumu wazi na kila chombo kiliandika,kuhusu maoni yale ni maoni ya muhariri na si siri tena CCM kuwa sasa inakabiliwa na Vurugu zinazotokana na URAIS wa 2015 ,wanahabari kama wananyanyasika hivi huyu mama Wingia amefanya kazi zaidi ya miaka 10 ni FOUNDER wa Gazeti la nipashe sisi waandishi wadogo tuna Future gani hapa nani yuko salama,wanahabari tuungane kupinga hili ni uonevu.
   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  kumbe huyo mzee naye gamba, duh na kelele zote zile na mafisadi papa tena muda wa taarifa ya habari.
  kama ni kweli basi huu ni muda wa kuanzisha trade union zinazoeleweka. kutetea wafanyakazi

   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  source ,ok weka hizo barua mkuu
   
 4. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Mhmmm ndiyo wamiliki wetu hao wa vyombo vya habari
   
 5. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  watafute kazi sehemu nyingine au waende kortini
   
 6. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  pata habari kamili na utupe source na copy za barua zao za kuachishwa kazi ili hii habari iwe na mantiki
   
 7. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  achakupenda maandamano kuliko akili zako ww mbona mlimfukuza hausgel wenu alipokataa kukuletea chai chumbani nani kakushutumu?
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Duh! barua ni personal labda ameonyeshwa tu, aombe aka-scan, aiweke humu, aliyeonyesha si atajua nani katoa taarifa. Yeye ndio source

  This is too much sasa!


  wakaombe kazi sehemu nyingine..10 years experience is gold they can not miss job anywhere!

  Mjifunze jamani kazi za watu na malengo yao, Mengi ni CCM damu, ni fisadi mzuri tu, lakini watanzania kama kawa wamepumbazwa!

  Mwisho please, please waandishi wa habari hamna umoja, kwa sababu ya waajiri wenu wenye malengo tofauti......

  hama hiyo fani haraka..siku hizi kusema mwandishi wa habari nchi hii ni kujiaibisha, hakuna investigative journalism
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  hawajamjua bado nani mchawi......acha kwanza watifuetifue,end of the day wakishamjua,kutakuwa kushakucha!!
   
 10. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Off point
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Ndo uhuru wa kutoa mawazo huo bongo, yaani usiseme lililoko moyoni wanakubana dunia nzima. Iko siku!
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,295
  Trophy Points: 280

  MVUA GAMBA, poleni kwa hayo yaliwakuta Bandawe na Wingia.

  Historia ni kujifunza mambo yalitokea hapo kale, ili kulinganisha na yanayotokea sasa kwa lengo la kupiga hesabu ya yale yatakayo kuja kutokea siku za usoni.

  Kwa sisi wa zamani, tunakumbuka jinsi Mushi alivyoondoshwa ukurugenzi wa itv na kupewa subordinate wake, sambamba na jinsi Vumi alivyoondoshwa na kupewa Mshana, hivyo hiki kinachotokea sio cha kushangaza ni cha kawaida sana hapo.

  Kwa mliousoma ule waraka wa Sakina Datoo, alioshaeleza kila kitu, hivyo hakuna jipya hapa.

  Nyinyi wanahabari wadogo hapo bado mna future nzuri ya kuwa wakubwa ndio mkutane na hayo. Kuhusu usalama, hakuna usalama sekta nzima ya habari achilia hapo.
  Wanahabari muungane na nani kuupinga huo uonevu dhidi ya nani, anzisheni ya kwenu vinginevyo kwa kuajiriwa piga ua galagaza, lazima mnyanyasike na kuonewa!, jiungeni ya safu yetu sisi ma freelancer!.
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kumbe magamba ni wengi kiasi hicho...
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,295
  Trophy Points: 280
  Waberoya, wewe unathubutu kumuita Mhe. huyu 'ni fisadi mzuri tu'?!, haya wewe subiria, sikuulizi kuthibitisha kauli yako, bali nasubiria jinsi watakavyo kushukia!

  Ni kweli waandishi hatuna umoja, ila sio kweli kuwa mwandishi wa habari siku hizi, ni kujiabisha, na sio kweli kuwa hakuna investigative journalism, ipo ila ina magazeti yake, na hata bila hiyo investigative journalism kuwepo, bado journalism ni fani adhimu!.
   
 15. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Mzee kumbe nae ni mmoja wao hao wenye Magamba! Ukimuona anaongea utadhani ni mtu mtaratibu na mnyenyekevu kwa watu kumbe nae ndi walewale. Hatari hakuna mahali pa kuponea
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Watu muache kushabikia kitu ambacho hamkifahamu. Huyu mhariri pamoja na huyo Bandawe na kikundi cha wahariri kadhaa walikuwa na mkutano uliodumu mpaka usiku wa manane pale Ubungo Plaza na ajenda ilikuwa ni kutengeneza utaratibu wa kuwasafisha watuhumiwa wa ufisadi na baada ya kufanya kikao hicho na kukubaliana, walipewa mshiko wa nguvu ambao hata ulipofuatiliwa, wengine walikutwa nao kwenye akaunti zao wakiwa wame-deposit siku hiyo hiyo. Mzee Mengi kama mmiliki wa vyombo vya habari amabvyo hapendi viingie katika upuuzi huo wa kugeuza ukweli kuwa uongo kwa vipande thelethini vya fedha akafanya uchunguzi na hatimaye kuwachukulia hatua tena baada ya wenyewe kukiri kuhudhuria mkutano huo. Kwa suala hili la kukiuka misingi ya utumishi na makubaliano ya ajira, ni nani angesamehe, tena vyombo vyako kusafisha na kuwaimbia mapambio mafisadi tena mahasimu wako?

  Mimi nadhani miaka yao mingi ya utumishi ilitakiwa iwafundishe uadilifu na siyo kutumia nafasi ya kukubalika na kuaminiwa kwao kupotosha umma. Mambo haya si mageni kwa wamiliki wa vyombo kwani hata ukiuliza akina Mwakitwange, Tagalile na akina Kwayu waliondokaje Habari Corporation? Mbona hakuna aliyepaza sauti? Mzee Mengi anastahili kupongezwa kwa kuondoa mbegu mbaya hata kama watu hao walikuwa na weledi wa hali ya juu katika uandishi wao.

  Lakini hata tukidhani kwamba kosa ni kuandika habari za Mtikila (ambayo si kweli), kuna ubaya gani kwa mmiliki kumuwajibisha mwandishi anayeandika habari ambazo huko mbeleni zitasababisha madai ya kashfa yanayoweza kukiweka chombo cha habari na mmiliki matatani? Kwa vyovyote vile atakayekwazwa na habari hizo hawezi kumshtaki Mtikila ambaye ni mchovu na hana heshima mbele ya jamii zaidi ya kuwa ni jeshi la kukodiwa. Bingo ingetafutwa kwa watu wanaomiliki vyombo kama Mzee Mengi. Na hii ndiyo maana wenyewe wamekauka kau! Wanajua dhambi zao.
   
 17. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MVUA GAMBA!

  Join Date : 13th April 2011
  Posts : 58
  Thanks
  0
  Thanked 12 Times in 7 Posts
  Rep Power : 21

  :A S-baby:
   
 18. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni hivyo bora watupishe
   
 19. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Poleni kwa hayo, mi si mwandishi but sipendi upotoshwaji wa taarifa unaofanywa kwa makusudi na waandishi wa Tz hasa kwa sababu ya njaa na kupenda mlungula kupita kiasi kwa maana hiyo nakosa iman wapi nisimame kat ya hawa waandish na bos wao. Who is right!
   
 20. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  who is right or wrong doesn't matter, the issue here is je mwajiri amefuata taratibu za ajira na usimamishwaji au kufukuzwa kazi kwa waajiriwa? Je tuhuma walizopewa zilikuwa sahihi? On the other hand je waandishi walifanya kazi kadri ya ethics za taaluma yao? If yes then they can always file the complaints if any to the court. That's my opinion. Tusisahau pia kuwa taaluma ya uandishi kwa kiasi kikubwa inasumbuliwa na njaa
   
Loading...