Power G
JF-Expert Member
- Apr 20, 2011
- 3,884
- 1,200
Hili kundi likitoswa kwenye uteuzi wa mgombea urais 2015 linaenda ADC, na hapo ndipo patachimbika. CDM watachukua nchi kiulaini kama wanamsukuma mlevi.Membe,magufuli,mwakyembe,6 ndo kaburi la ccm
Hili kundi likitoswa kwenye uteuzi wa mgombea urais 2015 linaenda ADC, na hapo ndipo patachimbika. CDM watachukua nchi kiulaini kama wanamsukuma mlevi.Membe,magufuli,mwakyembe,6 ndo kaburi la ccm
Umaarufu wa scandal za kifisadi hauna tija kwa taifa!
Anashangaza sana maana kampeni za udiwani si level yake.Huyu fisadi na yeye sasa ameanza kuweweseka baada ya kusikia kuna makundi mengine ya urais ndani ya ccm yameanza kujipambannua. Atulie anyolewe
binafsi simkubali mtu huyu kama ni dhambi MUNGU anisamehe, lakini inavyoonekana ccm hawana mtu mwingine zaidi yake kama wanabisha wamtaje ( kibaya zaidi wanachoangalia zaidi ni fedha zake ndizo wanazozifikiria )
anangufu kwa kuwa ana mali ambazo sisi wadanganyika hatujawahi hata kuhoji amezipataje.
lakini naamini MUNGU atafanya kitu siamini kama ataendelea kutuacha tunyanyasike.
Subirini kichapo Makuyuni..
Mbona umaarufu wake haukumusaidia Mkwewe Sioyi Sumary kule Arumeru!
Tatizo la Tanzania ukiwa FISADI ukuwa "MAARUFU" badala ya kuwa BEHIND BARS! Maajabu ya Tanzania hayatakaa yaishe kama CCM itaendelea kututawala.
Kwani yeye amechochea vurugu? Yeye ni mwizi tu wa Richmond na hao anaowasema wao ni vurugu sasa kichaa na mwendawazimu lao mojaDuh!hata wewe........kuna mtu alikuwa anaombewa na kutolewa pepo kanisani na kati kati ya wale waombaji alikuwepo dada mmoja naye akikemea kwa sauti ya juu ndipo yule pepo alimgeukia na kumuuliza hata wewe unanikemea.......nashangazwa na lowasa badala ya kujitakatisha ananyooshea wenzake vidole.....toa boriti kwanza ndani ya jicho lako mzee.
Anashangaza sana maana kampeni za udiwani si level yake.
lowassa: Sina shaka na umaarufu wangu .
Jumanne, mei 28, 2013 03:41 na eliya mbonea, monduli
.
Mbunge wa monduli na waziri mkuu mstaafu, edward lowassa, amesema hana shaka na umaarufu wake monduli wala tanzania kwa ujumla. Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana wakati akifungua kampeni za udiwani wa kata ya makuyuni huku akikishangaa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kwa kupeleka mgombea wake katika kata hiyo.
eti hawa wanathubutu kujinadi na kujigamba kushinda udiwani monduli ya lowassa wakisema watapata kura kwa asilimia 90 jamani haya ni kweli, alihoji lowassa na kuongeza:
ndugu zangu sina shaka na umaarufu wangu monduli wala tanzania.
katika mkutano huo, aliwaambia wananchi kwamba anahitaji kuona wakikiadhibu chadema kwa kukipa pigo ambalo hawajawahi kulipata mahali popote nchini.
ndugu zangu atakayewapa kura hawa chadema wana wa makuyuni atakuwa amenichoma kisu mimi, naomba msiwape kura hata moja, naomba muwafundishe adabu, alisema lowassa.
Akikishambulia chama hicho kwa kutumia helikopta katika kata hiyo, alisema siku zote vita vya kiafrika vinapiganwa kwa kutumia askari wa miguu na si helikopita.
Alisema ccm inatumia askari wa miguu kuhakikisha inashinda vita vyake, hivyo haitatishika na helikopita hiyo.
Alikirushia kombora chama hicho kwa kukitaka kisimame hadharani na kujipapanua kama hakihusiki na vurugu
zinazoendelea nchini.
Alisema kama kweli hakihusiki na vurugu zilizopo nchini basi viongozi hao wanapaswa kujihoji ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki.
nawaomba hawa chadema wajihoji ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki na vurugu hizi, je wanaifanyia nchi yetu mema au mabaya, alihoji lowassa.
Wewe na tembo dentist mlitakiwa muwe kwenye concentration camp. Umaarufu wa wizi?