Lowassa: Sina shaka na umaarufu wangu .

Lowassa: Sina shaka na umaarufu wangu .

Huyu mgombea wa CDM amegeuka mtu wa vurugu, mbona kwenye kura za awali akiwa CCM walimpigia kura wanachama wa CCM mpaka akaongoza kwa kuwaacha mbali wagombea wenzake wa CCM kabla jina lake halijakatwa katika ngazi ya mkoa, na ndipo akaamua kutafuta kuwatumikia wananchi kupitia chama kingine?, Au kuna ajenda nyingine imejificha ambayo haijajulikana. Vurugu zinazotumiwa na kutajwa kwenye kampeni ya Udiwani Makuyuni wilayani Monduli kwamba zinafanywa na CHADEMA mwenye ushahidi awatajie watanzania kwamba zilitokea kijiji gani wilayani Monduli, au ni kutaka kuwatisha wananchi wanaochukuliwa hawajui chochote, kama kipindi kile cha uchaguzi mkuu ambapo mikanda ya picha za vita ya Kimbari nchini Rwanda zilikuwa zinaonyeshwa vijijini kuwatisha wananchi maskini ambao hawana uwezo wa kufuatilia habari kila wakati kutokana na mazingira magumu ya upatikanaji wa mawasiliano wanakoishiambalo si kosa lao bali la mfumo, ambalo limewageuza kichaka cha kujipatia kura kwa kuwatisha kwamba wakichagua mtu mwingine maisha yao yatavurugika, wakati wanojidai wanawajali ndio hao hao wanawageuza ngazi ya wao kuneemeka.
Bado kuna kipindi kigumu kwa sababu wanaoambiwa wasichome visu viongozi(matajiri)wao ndio miili imejaa madonda ya visu vya kunyimwa haki zao.
 
Mbona hakusema kuwa amechomwa kisu wakati akimgombia mkwe wake awembunge.anajipa matumaini yasiyokuwepo na kuwadanganya watu wa makuyuni na umaarufu wake wa kifisadi hana jipya huyo ni wa kumuogopa kama ukoma hata julius alilijuwa hilo na ataendelea kulisimamia hilo.na watannzania tukija kumpa huyu jamaa hii inchi yanayotupata sasa ni cha mtoto.hawa jamaa wana laana ya mwalimu kumbukeni mwalimu aliwakataa hawa leo tunawakumbatia kwakweli hiki tunachokiona leo itakuwa mara mia tutajuta na Tanzania yetu.EDWARD NGOYAYI HAFAI KUWA RAISI WETU WATANZANI TUWE MAKINI JAMANI.
 
Mwizi ni mwizi tuu lowassa mwizi hata fred anajua uploadfromtaptalk1369763280160.jpg uploadfromtaptalk1369763280160.jpg
 
Lowassa: Sina shaka na umaarufu wangu .


Jumanne, Mei 28, 2013 03:41 Na Eliya Mbonea, Monduli
.

MBUNGE wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amesema hana shaka na umaarufu wake Monduli wala Tanzania kwa ujumla. Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana wakati akifungua kampeni za udiwani wa Kata ya Makuyuni huku akikishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kupeleka mgombea wake katika Kata hiyo.
“Eti hawa wanathubutu kujinadi na kujigamba kushinda udiwani Monduli ya Lowassa wakisema watapata kura kwa asilimia 90 jamani haya ni kweli,” alihoji Lowassa na kuongeza:

“Ndugu zangu sina shaka na umaarufu wangu Monduli wala Tanzania.”

Katika mkutano huo, aliwaambia wananchi kwamba anahitaji kuona wakikiadhibu CHADEMA kwa kukipa pigo ambalo hawajawahi kulipata mahali popote nchini.

“Ndugu zangu atakayewapa kura hawa CHADEMA wana wa Makuyuni atakuwa amenichoma kisu mimi, naomba msiwape kura hata moja, naomba muwafundishe adabu,” alisema Lowassa.

Akikishambulia chama hicho kwa kutumia helikopta katika Kata hiyo, alisema siku zote vita vya kiafrika vinapiganwa kwa kutumia askari wa miguu na si helikopita.

Alisema CCM inatumia askari wa miguu kuhakikisha inashinda vita vyake, hivyo haitatishika na helikopita hiyo.

Alikirushia kombora chama hicho kwa kukitaka kisimame hadharani na kujipapanua kama hakihusiki na vurugu

zinazoendelea nchini.

Alisema kama kweli hakihusiki na vurugu zilizopo nchini basi viongozi hao wanapaswa kujihoji ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki.

“Nawaomba hawa CHADEMA wajihoji ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki na vurugu hizi, je wanaifanyia nchi yetu mema au mabaya,” alihoji Lowassa.

hivi alistaafu uwaziri mkuu nchi ipi? hivi kashfa ya richmond imesahaulika? kamwe lowasa hawezi kusafishwa ingawa harambe zake za weekend--weekend zimefanya aanze kuitwa WAZIRI MKUU MSTAAFU. kuhusu umaarufu wake yuko sahihi, maana alipojiuzulu uwaziri mkuu na kurudi monduli wamasai walimshangilia kwa kusema....FISADI...FISADI..FISADI.., wakidhan ni nacho ni cheo zaidi ya hata kile cha uwaziri mkuu hivyo kwa imani yao hiyo ataendelea kuwa maarufu monduli hadi kiyama.
 
MBUNGE wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa,

Hivi haya maneno 'KUJIUZULU' na 'KUSTAAFU' yana maana moja ama yanatumika vyovyote tu.
 
Angekuwa na umaarufu Tanzania kuliko watanzania mbona sasa yule mkwe wake (Sioyi, sijui Sioi) angekuwa mjengoni!! Yaani mara hii ameshasahau Arumeru Mashariki?

Hakuna aliye maarufu kushinda watanzania wenyewe.
 
Bahati mbaya kiswahili hakina neno la kuwa kuwakilisha umaarufu(-ve), km infamous na famous tungemwelewesha umaarufu wake.

Naye ajihoji ndani yake km si fisadi+awaambie CCM nao wajihoji km si magaidi?
 
Kuipa kura Chadema ni sawa na kunipiga kisu cha Moyo- Edward Ngoyai Lowassa ( Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!)
 
Kuipa kura Chadema ni sawa na kunipiga kisu cha Moyo- Edward Ngoyai Lowassa ( Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!)

Tutakupiga vingi sana....wewe ufe tuu na E.L kwani naye kaamua jipa ugonjwa wa moyo.Hapa hana njia nyingine ya kupata heshima zaidi ya kusaidia iangusha CCM km Gorbachev.Akitaka urais atakufa kam Villain....Mark my word.
 
Hizo ndo mbwembwe za manvi; Alisema vivyo hivyo pale Arumeru tukala kichwa asubuhi na mapema pamoja na kumwaga mamilioni yake ya kifisadi , sasa leo hii, ujasili huo sijui anaupata wapi ?
 
Kwa mara nyingine tena polisi wameendelea kutumiwa na ccm wilayani Monduli,kata ya makuyuni kwa kumshikilia Mzee Lasai wa CHADEMA siku ya tatu leo kinyume cha sheria na haki za binadamu,anashikiliwa bila kesi,na kwa maelekezo ya viongozi wa ccm,eti kwa kuwa anaunga mkono CHADEMA
Hakuna jeshi litakaloweza kushindana na nguvu ya umma
 
kumbe monduli ya lowasa
nadhani hii smg ni wapinzan wake ndani ya chama
 
Umaarufu wake umekuja kwa lipi alilolifanya katika kipindi chote alichowahi kushika nafazi za juu Serikalini? Nchi imejaa ufisadi wa kutisha hatijawahi kumsikia akiongelea ufisadi mbali mbali ambao unaingamiza nchi. Nchi imehaa rushwa ya kutisha hatujawahi kumsikia akizungumzia kuhusu rushwa inavyorudisha nyuma maendeleo ya nchi. Mikataba mbali mbali ya rasilimali zetu haina maslahi yoyote kwa Tanzania na Watanzania hatujawahi kusikia akizungumzia lolote kuhusu hili. Hivi huko Serikalini alikuwa akifanya nini miaka yote madudu mbali mbali kama ya EPA, Kagoda, Meremeta, Rada, mikataba ya madini n.k. yakitokea!? Kwanini hakuwahi kuhoji madudu yote haya?

Kama alishindwa kuzuia madudu haya akiwa ndani ya Serikali basi hafai maana hana jipya. Alishapewa nyadhifa mbali mbali Serikalini lakini utendaji wake ulikuwa ni SIFURI hana hata moja ambalo Watanzania tunaweza kusema hili lililofanywa na Lowassa tunaweza kujivunia. Umaarufu wake aendelee kuwa nao lakini tukija kwenye utendaji ni ZERO hafai kabisa.
 
“Nawaomba hawa CHADEMA wajihoji ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki na vurugu hizi, je wanaifanyia nchi yetu mema au mabaya,” alihoji Lowassa.

Hakyanani wanasiasa mna roho ngumu kama shetani. Yaani Lowassa naye anaweza kuhoji wenzie kama wanaifanyia nchi yetu mema? Ama kweli nyani haoni mqundu wake!
 
Back
Top Bottom