Lowassa: Rushwa ni kansa inayoitafuna nchi

Lowassa: Rushwa ni kansa inayoitafuna nchi

Sijawahi au kumuona Lowasa Bungeni au kwenye mikutano anakemea Rushwa na Ufisadi uliokithiri nchi hii.

Huwa nasikia elimu, vijana nk. Hata sasa imefikia wahisani kukata misaada lakini sijawahi kumsikia Lowasa anakemea ufisadi. Mwenye evidence aweke hapa.

NB: Nahitaji ushahidi wenye mashiko, pia nahitaji angalau matukio matatu kwa kuwa Lowasa amekuwa kiongozi tangu ujana wake
 
Sijawahi au kumuona Lowasa Bungeni au kwenye mikutano anakemea Rushwa na Ufisadi uliokithiri nchi hii. Huwa nasikia elimu, vijana nk. Hata sasa imefikia wahisani kukata misaada lakini sijawahi kumsikia Lowasa anakemea ufisadi. Mwenye evidence aweke hapa

Mkuu umegusa jambo zito sana , ngoja tuone ushaidi utao letwa hapa jukwaani. na TEAM Lowasa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, unawaza kama mimi, leo nilimuuliza rafiki yangu, Mbona LOWASSA haongelei UFISADI ambao ndiyo agenda ya kitaifa?
 
Atazungumziaje masuala a Rushwa na Ufisadi ilhali yeye mwenyewe ni fisadi?
 
Sijaona media za Tanzania kuanza japo kimya kimya kuwabonda maswali mazito hawa wote waliotangaza nia au kusemwasemwa... Tunajua ccm hawataki midahalo ya wagombea wake ndo maana tunapata viongozi bogus. Ni woga wa journalists? au ni Sera za media owners kupaka rangi wagombea hawa?. Kunawandishi wa habari huwanatamani hata kuwapiga kwenzi wanapouliza maswali ya ajabuajabu nakuchekacheka. Mtu km Mamvi ukimpiga swali la rushwa najua anaweza kucollapse kabisaa! Asante mleta hoja yenye mashiko
 
Ndani ya CCM yetu nimewasikia hawa wakipiga kelele kuhusu ufisadi/rushwa:
Warioba
Butiku
Sumaye
 
[h=1]Lowassa akemea rushwa kwenye ardhi[/h]
07/10/2014 | Na Grace Macha | ArushaMikoani | maoni 0 | wasomaji 57
MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, (CCM), amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali na mila wanaochukua rushwa na kuuza ardhi za wananchi wakiwemo wajane kinyume cha utaratibu.
Aidha, ameitaka jamii ya wafugaji kuelewa kuwa ardhi ni utajiri mkubwa, hivyo wailinde kwani wanavyoiuza ndiyo tatizo la ukosefu wa maeneo ya malisho ya mifugo yao linavyozidi kukua.
Lowassa, aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kujadili changamoto za ardhi na mazingira wilayani Monduli uliowashirikisha wajumbe zaidi ya 400 wakiwemo viongozi wa mila (malaigwanani), viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi, (CCM) kuanzia ngazi za Vijiji, Kata na Wilaya.
Alisema kuwa tatizo la ardhi wilayani hapa ni kubwa lakini limekuwa likizidi kuongezeka kutokana na wafugaji kuuza ardhi waliyokuwa wakiitumia kwa ufugaji kwa watu wengine ambao huibadilisha matumizi na kuitumia kwa kilimo na kuendeleza makazi.
Hata hivyo, Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu, alisema kuwa sehemu kubwa ya ardhi ya jimbo hilo imetengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na jeshi, huku eneo dogo likibaki kwa ajili ya matumizi ya wananchi ambao idadi yao imekuwa ikiongezeka, hivyo akawataka washiriki wa
mkutano huo wajadili matumizi bora na endelevu ya ardhi hiyo.
"Tumewaita hapa tujadiliane tuone tatizo liko wapi kisha tushauriane tufanye nini kulimaliza, ndiyo maana tumewaalika wataalam wa ardhi wa halmashauri na Kamaishna msaidizi wa ardhi (Kanda ya Kaskazini),
Doroth Wazala watusaidie," alisema Lowassa.
Kwa upande wake, Mbunge wa viti maalum, Namelok Sokoine (CCM), alisema kuwa wilayani hapa kuna migogoro mingi ya ardhi kuanzia ngazi za familia
na koo, jambo linaloibua uhasama miongoni mwa jamii kutokana na wengine kuamua kupelekana mahakamani.
Chanzo: Tanzania Daima
 
Lowassa akemea rushwa kwenye ardhi

07/10/2014 | Na Grace Macha | ArushaMikoani | maoni 0 | wasomaji 57
MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, (CCM), amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali na mila wanaochukua rushwa na kuuza ardhi za wananchi wakiwemo wajane kinyume cha utaratibu.
Aidha, ameitaka jamii ya wafugaji kuelewa kuwa ardhi ni utajiri mkubwa, hivyo wailinde kwani wanavyoiuza ndiyo tatizo la ukosefu wa maeneo ya malisho ya mifugo yao linavyozidi kukua.
Lowassa, aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kujadili changamoto za ardhi na mazingira wilayani Monduli uliowashirikisha wajumbe zaidi ya 400 wakiwemo viongozi wa mila (malaigwanani), viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi, (CCM) kuanzia ngazi za Vijiji, Kata na Wilaya.
Alisema kuwa tatizo la ardhi wilayani hapa ni kubwa lakini limekuwa likizidi kuongezeka kutokana na wafugaji kuuza ardhi waliyokuwa wakiitumia kwa ufugaji kwa watu wengine ambao huibadilisha matumizi na kuitumia kwa kilimo na kuendeleza makazi.
Hata hivyo, Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu, alisema kuwa sehemu kubwa ya ardhi ya jimbo hilo imetengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na jeshi, huku eneo dogo likibaki kwa ajili ya matumizi ya wananchi ambao idadi yao imekuwa ikiongezeka, hivyo akawataka washiriki wa
mkutano huo wajadili matumizi bora na endelevu ya ardhi hiyo.
“Tumewaita hapa tujadiliane tuone tatizo liko wapi kisha tushauriane tufanye nini kulimaliza, ndiyo maana tumewaalika wataalam wa ardhi wa halmashauri na Kamaishna msaidizi wa ardhi (Kanda ya Kaskazini),
Doroth Wazala watusaidie,” alisema Lowassa.
Kwa upande wake, Mbunge wa viti maalum, Namelok Sokoine (CCM), alisema kuwa wilayani hapa kuna migogoro mingi ya ardhi kuanzia ngazi za familia
na koo, jambo linaloibua uhasama miongoni mwa jamii kutokana na wengine kuamua kupelekana mahakamani.

chanzo: Tanzania Daima
 
Sijawahi au kumuona Lowasa Bungeni au kwenye mikutano anakemea Rushwa na Ufisadi uliokithiri nchi hii.

Huwa nasikia elimu, vijana nk. Hata sasa imefikia wahisani kukata misaada lakini sijawahi kumsikia Lowasa anakemea ufisadi. Mwenye evidence aweke hapa.

Itakuwa ngumu sana. Nimekuwa nikimfuatilia kwa kila tukio na bahati nzuri amekuwa na matumizi mazuri sana ya vyombo vya habari kwa kila tukio la kisiasa au kijamii analolifanya kupata 'coverage' ya 'Media'. Sijawahi kusikia kwa kweli. Na kwa mazingira ya nchi yetu yalivyo kiongozi asiyekemea rushwa anatia shaka kidogo.

Kwa kuongezea katika mada yako pia siridhishwi na ushiriki wake pale bungeni kama Mbunge, sijawahi kumwona au kumsikia akichangia kama ambavyo nilitarajia! Sitaki kuamini kuwa hana cha kuchangia tangu alipoacha cheo cha uWaziri Mkuu!
 
Back
Top Bottom