I say thanks for this useful post, sijui prezidaa alikuwa anafikiri nini hapo, hii ni kuwafanya watanzania wajinga wasio na uwezo wa kifikiri, ni bora hata jk angeacha wakajipigia kampeni wenyewe, sidhani kama wangeshindwa bila kikwete, pili kwani jk aliwapigia kampeni wagombea wote wa ccm, sasa kwa nini hawa. This was a big mis-calculation.
Na asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga jiwe, Yesu akatazama chini na kuandika ardhini alipoinua macho wakawa wameondoka wote, nasema, JK umejipalia makaa, ndugu yangu, unawatosa watatu, wakati kunawengi, umeshau aliyekuwa MP wwa Rombo? hukumtosa, unajua ufisadi unaofanywa Maliasili umeamua vp?
Unajua nini kunaendelea TRA, bandarini, viwanja vya ndege, mipakani umechukua juhudi gani? hawa ni wa bunge watatu, je unadhani ndiyo mianya pekee inayosababisha ufisadi kukua? Unakumbuka Azimio la Arusha sababu yake kuu nini? Siyo ufisadi? japo wengine tulikuwa bado au wadogo sn, lkn hatua ya Moringe sokoine kukomaa na mafisadi kuanzia wahindi mpaka wafanya kazi wa serikali ndiyo ulikuwa msingi pekee wakuiponya nchi, lkn hii hatua ni kuosha kikombe nje ndani kuna mende japo niwadogo lkn maji hayanyweki.
Hakika nasema akina kabwela walala hoi tunakuambia kuwa ukitaka kuiponya nchi jukumu kubwa nikuwafilisi watendaji wakuu waserikali ambao unadhani au unauhakika na uporaji wamaliasili za nchi, nadhani siku hizi usalama wa taifa wamekuwa si watunza siri, hata ukiwatuma kwenye viwanja vya ndege kuwa wafanya kazi badala yake wataanza kufanya ufisadi.
Mawaziri husika hawafanyi kushtukiza kukagua utendaji wa mipaka yetu, nakumbuka kufanyiwa rusha hapo nyerere airport, lkn leo ukisema unageukiwa wewe, ndug, dhambi hii japo umesema kwa kuponya kidonda cha kujikwaa kisiasa km ulipomwambia EL, unasababisha jipu ambalo kweli kupona kwake ni kulitumbua kwa kisu na usaha ukitoka watu wote watasema haaa! kumbe ccm wako hivi!
Laiti ungesema yaliyopita si ndwele wa TZ kwaniaba ya wote tunaomba msamaha, halafu huko chinichini uchukuwe hatua ya kumwaga mboga, wao wangekula ugali bila kujua mboga inakuja hau imemwagwa, lkn unasema namwaga, wao wanasema cc ugali hatuli tunamwaga, wote mnalala njaa, ccm siyo mama, siyo baba, wakijitoa nakusema wakotayari kuwaomba msamaha wa TZ na wakakubaliwa wakirudi ulingoni kivinge, ww utakuwa unajipumnzisha ndipo watakuambia ukakalale lupango kwani hukusema ukweli kuhusu mali zako, nasema ukimaliza muhula wako ck zinaendelea, nakusikitikia hukuona mbali, utajiamaliza mwenyewe, hawa watuwakitubu nakurudisha mali walizochukua nakuomba msamaha kwa wanachi je utasmeaje?
Amani ya kweli huja kwa kusameheana nakuomba yalopita yasirudiwe, na utendaji wa serikali uboreshwe.