Lowassa: Nitamtoa Babu Seya gerezani

Lowassa: Nitamtoa Babu Seya gerezani

Status
Not open for further replies.
mimi nimekuelewa wewe unamaanisha kuna ndugu yako pia yupo SEGEREA sasa ulivyo msikia Mh. Raisi Ndg. ENL kawataja hao baadhi ukachanganyikiwa sio... Hii imekaa hivi hao kawataja kama mfano tu wa kuwakilisha wengi kama hao. Hivyo nakushauri ukae karibu kuorodhesha jina la huyo ndugu yako utasaidiwa tu na atatoka kwa msamaha wa RAISI. Toroka uje M4U.
 
Wananchi watapata FAIDA GANI kutolewa KWA MASHEHE NA babu seya?

LOWASSA alipaswa kuzungumzia matatizo yanayo wakabili wananchi ya kimaendeleo kuliko hayo ya babu seya.Kuna wafungwa wengi waliofungwa kimakosa kwann amewabagua hao? Basi angewazungumzia wafungwa wote kuliko kuleta ubaguzi. KWA hilo alikurupuka.

Wasalaam,

Abel sere from Moshi

Siasa za maji taka haswa ndio hizi. Nchi yenye mahakama wewe na akili zako timamu unatangaza , tena hadharani, kuwa utaiingilia mahakama kesi iliyoko mahakamani utaiondoa na kuifuta. Halafu kesi nyingine ambayo mahakama ilishatoa hukumu na rufaa zote kumalizwa na mtu kupatikana na hatia eti utamwachia huyo mfungwa. Wale wazazi wa watoto walioharibiwa na Babu Seya wanajisikiaje kwa maneno ya Lowasa? Hawa mashehe wa uamsho walipokuwa wakipeta kule Zanzibar waliuawa viongozi wangapi wa kidini yaani mashehe na mapadre? Sisi tunaoona nafuu sasa angalau hali imetulia baada ya wale mashehe wa uamsho kufunguliwa mashtaka tukueleweje wewe Lowasa? Kweli una nia njema na nchi hii????
 
Naona unajitahidi kumback up sana huyo mzee, too late now.
 
kwa hiyo waislamu na wasanii sio wananchi. kweli ccm imechoka kutawala....
 
Wandugu nilimuona mzee lowasa siku ya ufunguzi wa kampeni za ukawa pale jangwani akisema suala la babu seya amelisikia na atalishugulikia ikiwa ataingia ikulu kwa maana atatumia mamlaka kuagiza kesi hiyo kupitiwa upya au hata kuwasamehe watu hao.
Ingawa suala la seya na papii halikuwepo kwenye ilani ya ukawa pengine ni huruma ya kibinadamu imemshika mzee wetu kama inavyoweza kumshika mtu yoyote ikumbukwe hata mawakili waliotetea kesi hiyo akiwemo marandu walilalamika kuwa kesi iliendeshwa bila kufuata kanuni za kisheria.
Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuona tamasha la magereza kumkumbuka mwalimu nyerere likionyeshwa na tbc/tvt wakatumbuiza babu seya na mtoto wake ,kiukweli mwanaume mzima huzuni ilinishika machozi yakanitoka hata wale wahudhuriaji pale ukonga walihuzunika kudhihirisha kesi ya seya imewauzunisha wengi.
hata raisi wetu dr.kikwete huruma ilimshika aliwahi kuwasamehe adhabu ya kifo na kuwaachilia huru askari waliohukumiwa kesi ya mauaji ya imran kombe mwaka 2011 hivyo raisi anayo mamlaka ya kutengua adhabu ya mahakama.
JK AWAACHIA HURU POLISI WALIOMUUA JENERALI KOMBE – Global Publishers
 
Sio babu seya peke yake ni pamoja na mshekhe wetu waliowekwa ndani hadi leo. Kwetu sisi WAISLAMU ni pigo kubwa sana hasa shekhe msellem ambaye ni mfasiri mzuri sana wa kuran kuwekwa ndani kimagumashi. waislamu hatuandamani tena ila yaliyomoyoni mwetu ni OCT 25
 
KINACHOWAPONZA CHADEMA

Nimejaribu kufatilia kwa umakini kampeni za wagombea wa nafasi ya uraisi hasa wa Magufuli na Lowasa,nimebaiini mambo kadhaa yanayompoza Ndugu Lowasa,tatizo kubwa la huyu jamaa ni kutoa ahadi ambazo hazina tija na pia utaekelezaji wake ni mgumu (yeye mwenyewe anashindwa kufafanua utekelezaji wake).

Ahadi kama kumtoa babu seya,kuwatoa magaidi na kumleta balal (hizi hazina tija kwa wananchi),ahadi za kuondoa umasikini,elimu buree,kufufua viwanda n.k amekuwa akizitoa kila anapofanya mkutano bila kueleza mipango au mikakati yake itakavyokuwa!Baadhi ya wananchi wanahisi kama kiongozi huyu amekremua kusema hayo!

Lowasa wananchi wanahitaji mikakati na si ahadi hewa,ahadi unazotoa bado hujaweza tushawishi maana hata mtoto mdogo wa darasa la pili anaweza ongea unayoongea!!
 
Ndo maana anajinye..l.l.l.l! Siasa safi si jadi yake. Yeye anaenda kiujanja ujanja tu
 
Lowasa hajawahi kuwa mwanasiasa mwenye hoja yeye kila kitu anadhani pesa ndiyo inafanya kila kitu lakini pia watanzania walikuwa hawajapata fulsa ya kumsikia kwa kina kwa sasa ndiyo kajipambanua sasa kila mtu kamjua kuwa ni mzugaji tu.
 
Ni kweli elimu bure,kufufua viwanda,kuondoa umasikini.ni mambo yanayohitaji degree kuyatekeleza!!!!!!!!ni ujinga walionao watanzania kama wewe mliopewa na sisiemu kuwa hayo nayo yanahitaji mikakati mikubwa wakati ni swala la kuamua tu lililowashinda mabosi wako.

Hiyo kumleta balali na kumtoa seya ni kutaka kuonyesha ni namna gani hata kuwa tayari kushuhudia upokwaji haki.

Nawewe utwambie mgombea wako kipenzi anapiga push up na kuahidi huduma za afya bure,mahakama ya mafisadi,migambo kukosa kazi,atatekeleza vip?????kwa kupiga push up?au kwa kuimba aliselema???
 
Mbona magufuli hatoi ufafanuzi wa hizo ahadi,tena nyingi sana utadhani ndio tumepata uhuru Leo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom