Binafsi nilishtuka sana kumsikia Rais mtarajiwa akiahidi hadharani ku frustrate maamuzi ya Mhimili wa mahakama bila hata kusema atatumia sheria ipi. Tunajua Rais ana mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria nyingine. Lakini msamaha huo hautolewi kihorelahorela na kwa kosa lolote tu bila kufuata guideline zilizopo.
Babu Seya kwa kosa aliloshtakiwa na kufungwa kwalo haliko na muda wa kifungo alichopewa (Maisha) halimo katika orodha ya makosa ya kusamehewa na kutolewa jela. Sijui huyu atakuwa ni Rais wa aina gani.
Nadhani Lowassa amepoteza uwezo wa kutafakari kwa kina na anaoambatana nao pia ni laymen kwa mambo mengi tu achana kuwa laypersons wa kisheria tu.
Huyo mwenyekiti wa CDM ndo layman wa mambo mengi sana na hata anayodhani anajua anayajua kijuujuu tu na nadhani hata washabiki wao wengi ni wa aina hiyohiyo. Wakipewa viroba, wakawekewa mafuta kwenye bodaboda, posho kidogo iso zidi 20000 wako tayari kuandamana na kushangilia lolote litokalo vinywani mwa hao wakubwa zao.
Hivi wewe ambaye una mtoto wako wa kike au kiume mwenye umri wa miaka 10 na kurudi chini hadi 6 anapobakwa tena kwa namna ile ya kuchangiwa na watu zaidi ya mmoja na akaharibiwa sehemu zake za siri mbele na nyuma utakuwa na ushujaa wa kumshangilia rais ajaye anyesema atawaachia huru wabakaji wa aina ya Babu seya?
Mahakama ya Rufaa ndiyo chombo cha juu kabisa cha utoaji haki nchini kwetu na ina majaji weredi sana na kwa hiyo uamuzi wake ni wa mwisho. Leo unawezaje kuwa na rais ambaye anasisitiza kuwa ataingilia uhuru wa Mahakama?
Mleta mada anajielewa?au ---- Fulani maana tunajadili nchi unaleta ya chalinze