mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,727
Nini cha ajabu hapo !!?? Kuna boda boda milioni 1 laki 1 na 20 kila boda boda mmoja akitoa hisa sh 10.000 .x milioni 1 tuu ni bilioni kumi.ni mtaji tosha wa kuanzisha benki 5 mpya kwa kiwango cha sasa hivi cha bilioni 2 .mtaji wa kuanzisha benki. Unashangaa nini huo ndio uongozi unatakiwa wa kuonesha njia.Lowasa raisi wetu. Na pili zingatia elfu kumi nipato la siku moja tuu.kwa boda boda.ataa kama ni dereva tuu atamudu .
Hesabu yako ni sahihi kimtaji. Swali: Je, kuanzisha benki ni kuwa na mtaji tu? Mfano ulio wazi, na unaotolewa sana humu jamvini (CCM na Vyama vya Upinzani, hasa UKAWA wakimpamba mgombea Urais) ni Sekondari za Kata. Matatizo ya Sekondari za Kata si majengo ni pamoja na huduma mhimu ikiwemo uhaba wa raslimaliwatu kuziendesha. Kwa mfano huo, Benki ya Bodaboda ni laghai ya mchana kweupe kupata kura zao. Hata bila kuwa Rais, mjasiriamali anaweza kuanzisha hiyo banki kama inalipa. Rais mtarajiwa atwambie mikakati aliyonayo ya kuweka mazingira mazuri ya kuwekeza au kufanya biashara inayolipa, kwa kila mtu.
TAFAKARI CHUKUA HATUA