Lowassa "nitaanzisha benki ya bodaboda"

Lowassa "nitaanzisha benki ya bodaboda"

Ni bora wangekuwa wanamuandikia cha kuongea huyu jamaa, jamaa kichwani hakuna kabisa anaropoka yanayokuja kichwani tu,Bank ya bodaboda ya nini hizi bank tulizonazo za kazi gani?
yaani yeye hii kazi ya bodaboda imemvutia sana mpaka awafungulie na bank?
Lowasa hatoi taswira ya rais ambaye anaweza kutoa kauli ya kuinspire inayoweza kuwa quoted vizazi kwa vizazi
 
Akihutubia wananchi wa mjini Kiomboi katika Jimbo la Iramba Magharibi, Lowassa aliahidi kuwa akichaguliwa ataanzisha benki ya boda boda. Wakati ukiyasikiliza haya na wewe tumia akili zako.

Za kuambiwa changanya na zako.

Huyu jamaa akili kweli zimo?

benki ya bodaboda???????.

asee lowasa ni mwisho asee....ha ha ha ha

Yesuuuuuu komnyo ya kwanswa Lowassa ngikiyo? Banki ya bodaboda? Halafulee? Ngienda wapi kudanganya mbatu? Yesuuuuuu ngikiyo mabesa? Acha ujingaaaa Lowassa njoo huku moshi unjwe kitochi cha mbege, siasa ni za magufuli!! Mburaaa, huku huku migombani ukiongelea ukawa Yesuuuuuu unamwagiwa mbege usoni..... #hapakazitu babangu
#mabadiliko peleka mamlaka husika ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Njoo unywe kitochi wewe achana na siasa za nyani!!
#hapakazitu

Asisahau naya mama ntilie pamoja na wamachinga.

Kumbe bora azungumze dakika mbili tu
akizungumza mda mrefu ndo kama haya sasa
what next?benki ya mama lishe?

Hivi bodaboda ni ajira?au ni tatizo la miundo mbinu mibovu?

Kila nchi hasa zilizoendelea zina bodaboda?

yeye akienda Ujerumani kutibiwa huwa anakuta bodaboda huko?

Hivi lowasa anadhani watu wanaakili nyepesi kama zake?

Lowasa janga sugu la wazawa?

Oneni na huyo mnayemuabudu alichokizungumza.

https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-kushusha-neema-kwa-bodaboda-na-machinga.html
 
Mliisha wahi kujiuliza juu ya tamko la CCM kuwa itatoa Million 50 kila kijiji je kuna impact yeyote kwa maendeleo ya Mtanzania kwa kutoa hizo fedha kwenye kijiji? CCM iliweza kutamka kuwa itaanzisha Bank ya Wakulima, Bank ya wanawake kuna tofauti gani na kuanzisha Bank ya Boda boda? kama Mkapa na Mke wake wameweza kuanzisha Bank je kwa vijana wengi ambao ni boda boda hawawezi kukusanywa kwa pamoja na kuongozwa chini ya usimamizi wa serikali na wao kuweza kuanzisha Bank yao?

Mnapo pinga kitu ni vema kabla mkatafakari kwa kina pia kupitia matamko ya nyuma yaliyowahi kutamkwa na hao viongozi wenu mnaowaabudu kuliko hiki mnachokifanya mnajishushia heshima.
Hii inathibitisha tu kuwa mgombea wa UKAWA kichwani kutupu.
Kwanza anamuachia Babu Seya, halafu haoengi chochote juu ya mafisadi.

Bado namuuliza anaenda Ikulu kufanya nini?
 
пьжсосвд хд типфи яьхьл гьнсхь пщс ьщьнькиеиюь нсягдхаьхь хь пьососвд

гьз еихжхи хд остз щс двь снеивд гьщь еьз еьхтсь гьеьеиюд нсягдхаьхь хь пьжсосвдл

Come on nigga!! Mbona hunijibu? Umechokoza Sasa umenasa!!
 
Ni bora wangekuwa wanamuandikia cha kuongea huyu jamaa, jamaa kichwani hakuna kabisa anaropoka yanayokuja kichwani tu,Bank ya bodaboda ya nini hizi bank tulizonazo za kazi gani?
yaani yeye hii kazi ya bodaboda imemvutia sana mpaka awafungulie na bank?

Tatizo watu wengine mnafikiri kwa Masab......ri. Eleweni kuwa unaweza kutumia watu wenye matatizo katika umoja wao kuwaendeleza, bodaboda ni tatizo ila imewaunganisha vijana wakaacha uhalifu na wakafanya kazi ya halali, ili kuwatoa stage moja kwenda nyingine kwa kutumia umoja wao unaweza waanzishia bank yao hiyo itawafanya wapate mtaji wa kuanzisha miradi mingine yenye tija na faida zaidi kwa kuwatumia wenyewe ku-raise mtaji na kuwaongezea kidogo. Hivi huoni tatizo la Magamba kwenye kudharau maoni ya waTZ kwenye katiba mpya limezaa UKAWA ambayo imekwenda beyond katiba mpya iliyokuwa source ya kuundwa kwake na sasa inalikomboa taifa kutoka kwenye makucha ya mkoloni mweusi!Acheni masabur..... yafanye kazi yake tumieni akili kufikiri
 
Nini cha ajabu hapo !!?? Kuna boda boda milioni 1 laki 1 na 20 kila boda boda mmoja akitoa hisa sh 10.000 .x milioni 1 tuu ni bilioni kumi.ni mtaji tosha wa kuanzisha benki 5 mpya kwa kiwango cha sasa hivi cha bilioni 2 .mtaji wa kuanzisha benki. Unashangaa nini huo ndio uongozi unatakiwa wa kuonesha njia.Lowasa raisi wetu. Na pili zingatia elfu kumi nipato la siku moja tuu.kwa boda boda.ataa kama ni dereva tuu atamudu .

Kwa hiyo shida ya bodaboda ni benki?
 
Japo hili wazo linaweza kubezwa na wengi hasa wapinzani wake. Ila ukiliangalia kwa jicho pana, linawezekana na linaweza kuleta tija kubwa tu kuliko inavyodhaniwa. Kwani kumbuka watakaojiunga si Boda boda tu, humo pia wanaweza ingia madereva wa Bajaji na hata wenye vipato vya chini. Tena itarahisisha sana hata kuwapatia mikopo hao madereva wa Bodaboda. Kumbukeni Bodaboda zina kazi zaidi ya kubeba abiria. Kuna maeneo watu ndio zinatumika kufanyia shopping za maduka hasa vijijini. Hata matajiri ni rahisi kumkopesha dereva wa Bodaboda kupitia Benki inayoeleweka kuliko mikataba ya mali kauli ambayo unaweza kulizwa hivihivi. Na wengi madereva wamelizwa kwa style hii.

Hebu tujiulize ile Benki ya wanawake au Mkombozi mtaji ni nini hasa mpaka Rugemalira akaamua kupitishia yale mabilioni kule? Kama Efatha kaanzisha, Mkono kaanzisha sembuse Bodaboda ambao wana uhakika na kipato kwa siku hakipungui 10,000.00Tshs. Ulishajiuliza CRDB ile ya mkulima ilianzishwa kwa malengo na mtaji toka wapi? Nasisitiza Sio CRDB Bank Plc hii ya sasa ya makaburu.
 
Cha ajabu kipi hapo...hebu tafiti ni vijana wangapi leo wangegeuka mateja na vibaka lakini wamejiajiri kupitia bodaboda...viva Lowassa
 
Hili si kwa chadema/ukawa tu bali hata ccm kweli tumefika mahali wanasiasa wametuziba macho kwa kutudanganya suluhu ya ajira ni kuwapa vijana bodaboda wakati watoto waviongozi wanajazana BOT?? Tusikubali hadaa hii kubwa watu wanahitaji elimu japo sio hata ya vyuo vikuu lakini vyuo vya ufundi ni kitu muhimu sana kama tunataka kutatua swala la ajira.

Nikisoma watu ambao akili zao ziko timamu huwa nafarijika sana LACHERO keep good mkuu
 
Last edited by a moderator:
Japo hili wazo linaweza kubezwa na wengi hasa wapinzani wake. Ila ukiliangalia kwa jicho pana, linawezekana na linaweza kuleta tija kubwa tu kuliko inavyodhaniwa. Kwani kumbuka watakaojiunga si Boda boda tu, humo pia wanaweza ingia madereva wa Bajaji na hata wenye vipato vya chini. Tena itarahisisha sana hata kuwapatia mikopo hao madereva wa Bodaboda. Kumbukeni Bodaboda zina kazi zaidi ya kubeba abiria. Kuna maeneo watu ndio zinatumika kufanyia shopping za maduka hasa vijijini. Hata matajiri ni rahisi kumkopesha dereva wa Bodaboda kupitia Benki inayoeleweka kuliko mikataba ya mali kauli ambayo unaweza kulizwa hivihivi. Na wengi madereva wamelizwa kwa style hii.

Hebu tujiulize ile Benki ya wanawake au Mkombozi mtaji ni nini hasa mpaka Rugemalira akaamua kupitishia yale mabilioni kule? Kama Efatha kaanzisha, Mkono kaanzisha sembuse Bodaboda ambao wana uhakika na kipato kwa siku hakipungui 10,000.00Tshs. Ulishajiuliza CRDB ile ya mkulima ilianzishwa kwa malengo na mtaji toka wapi? Nasisitiza Sio CRDB Bank Plc hii ya sasa ya makaburu.[/
FONT]

Ndio maana unaambiwa tatizo sio bank ya boda boda ila inatakiwa ku accommodate hao wa vipato vya chini kwa taasisi zilizopo kwa masharti nafuu na riba ndogo ili hii shida ife kabisa sio kujaza benki kila mtaa. . .Mara boda boda hapa ya wauza mboga huku mama lishe. . .Mtaa wa pili. . . Mafundi ujenzi, next house ya waziba pancha, mtaa wa tatu. . . Makonda na madereva. . .Next turn washona siti za magari. . . .benki mji mzima za nini!!!!

Patchy work. . . ., .!!!
 
Mbona kuna benki ya kina mama?

Kama CRDB, NBC, NMB zingekuwa na mazingira mazuri hiyo ya wanawake ingekuwa ya nini haswa. . . . . . .Unavunja daraja unanunua kivuko kwa michango ya wananchi halafu unawaambia wamejiwezesha. . . . .
 
Nini cha ajabu hapo !!?? Kuna boda boda milioni 1 laki 1 na 20 kila boda boda mmoja akitoa hisa sh 10.000 .x milioni 1 tuu ni bilioni kumi.ni mtaji tosha wa kuanzisha benki 5 mpya kwa kiwango cha sasa hivi cha bilioni 2 .mtaji wa kuanzisha benki. Unashangaa nini huo ndio uongozi unatakiwa wa kuonesha njia.Lowasa raisi wetu. Na pili zingatia elfu kumi nipato la siku moja tuu.kwa boda boda.ataa kama ni dereva tuu atamudu .

Mkuu hao jamaa hawafikirii nje ya box wao siku zoote ni ndani ya box tu. Na ndio maana kila kitu cha kimaendeleo kwao ni ajabu. Hawana tofauti na binaadamu wa zama za ujima.
 
Nini cha ajabu hapo !!?? Kuna boda boda milioni 1 laki 1 na 20 kila boda boda mmoja akitoa hisa sh 10.000 .x milioni 1 tuu ni bilioni kumi.ni mtaji tosha wa kuanzisha benki 5 mpya kwa kiwango cha sasa hivi cha bilioni 2 .mtaji wa kuanzisha benki. Unashangaa nini huo ndio uongozi unatakiwa wa kuonesha njia.Lowasa raisi wetu. Na pili zingatia elfu kumi nipato la siku moja tuu.kwa boda boda.ataa kama ni dereva tuu atamudu .
Mawazo ya umachinga mentality.
Nchi itaende,ea saa ngapi?
 
Ndugu tambua kuwa kwenye mgawanyo wa majukumu na kazi za ajira zipo za aina nyingi Boda boda ni sehemu ya ajira kwa vijana kwani wanatoa huduma kwa jamii, unapozungumzia juu ya ajali wanazopata na kupoteza maisha hilo ni tatizo ambalo linasababishwa na wahusika wa kusimamia usalama barabarani kwani hawatoi miongozo ya kutosha kwa hawa vijana na pia miundombinu ya barabara zetu ni duni kwani barabara nyingi anazojisifia magufuli ni nyembamba na zingine zina makorongo makubwa na madogo kuhusu suala la Viwanda na Kilimo ni sawa vijana kujikita huko lakini kwa wingi wa vijana waliopo sasa hawawezi wote kujikita huko pia ikumbukwe elimu wanayopata hawa vijana wengi wao utakuta wanaishia kidato cha nne sekondari za Kata.

Japan ina eneo dogo kuliko Tanzania, tena wakazi wake ni zaidi ya mil 150. Ulisha sikia wameopt bodaboda kama ajira kwa vijana wao. Usimtetee Lowasa, hizo fikra za kizamani ndo zimetufikisha hapa. Tunataka fikra mpya. Lowasa anafanya repackaging fikra zilizofeli na kiziita mabadiliko. Tuache kuwatetea wagombea maana mwisho wa Siku sisi ndo tunaumia.
 
Back
Top Bottom