Lowassa: Nimeshawishika, Nitagombea urais...!

Lowassa: Nimeshawishika, Nitagombea urais...!

tusipokuwa makini huyu masai ataingia ikulu huku tunaona.
 
Sara yangu ya Leo. E Mungu tuondolee kikombe hiki sisi Waja wako Watanzania. Hii timu itatuacha watupu.
 
jamani hebu tuweni wakweli,hivi katika CCM ya sasa kuna mtu anaweza kugombea ubunge ua urais bila kumwaga pesa?? sema wanatofautiana mbinu za kuhonga/kutoa rushwa ila wote ndani ya CCM wanatumia hela nyingi sana kusaka vyeo,iwe ubunge au urais na hata udiwani
 
Mzee mamvi na Profesa tezi tunajua hamkukutana vichororoni, Mungu sikia kilio chetu tumesulubika kwa miaka 10, pls God tuokoe na hili jinamizi lilojaa mamvi uso mzima ili hiyo miaka mingne 10 tupumue baada ya kusota kwa muongo mzma.
 
Baba wa taifa hayati Nyerere alishasema Lowasa hafai kuwa raisi huu wosia wa umuhimu sana kwa vijana wote.
 
tusipokuwa makini huyu masai ataingia ikulu huku tunaona.

Hata mie nimeanza kuogopa mkuu kuna watz wengi wanaoendekeza shibe ya siku 1 inavoonekana watatuangusha hili jitu na mamvi yake hela lilizonazo zinalibeba aiseee!
 
Baba wa taifa hayati Nyerere alishasema Lowasa hafai kuwa raisi huu wosia wa umuhimu sana kwa vijana wote.

KATIBU MYEKA WA NYERERE: JINA LA MWALIMU LINATUMIWA VIBAYA NA KAMBI YA LOWASSA

Katibu Myeka wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mzee SAMWEL KASORI ameibuka na kufukua ukweli uliojificha, baada ya baadhi ya wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kulihusisha jina la Mwalimu na mbio za urais. Itakumbukwa kuwa Feb. 10 mwaka huu, Mbunge wa mbinga Magharibi, John Komba alidai kabla Mwalimu Nyerere hajaaga dunia alimkubali (aliridhika na) LOWASSA.

KATIBU Myeka wa Nyerere, Mzee Samweli Kasori amesema, Mwalimu alitilia shaka uadilifu wa LOWASSA na hakuwahi kuridhika na utendaji wake hata kidogo. Mzee Kasori anaendelea kusema Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa LOWASSA alikuwa ni mmoja wa wagombea nafasi ya urais mwaka 1995 na alienfukiwa kwa hoja nzito ya kutokuwa Mwadilifu na Babab wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere.

Mzee Kasori anasema baada ya kuenguliwa, Lowassa alimpigia simu kumuomba amuombee kwa baba Taifa aende Monduli amsafishe ili asikose Ubunge kutokana na maneno aliyoyasema Dodoma ya kumuengua kwenye kugombea Urais, jambo ambalo lilikuwa vigumu kwake(yeye mzse Kasori). Baada ya Lowassa kuona Mzee Kasori amekataa akamtumia mzee Rashid Mfaume Kawawa ndipo mzee Kawawa akampigia Simu Mzee Kasori kutekeleza maombi ya Lowassa kwa Mwalimu.

Baada ya purukushani zote za Mzee Kasori kuhakikisha ujumbe unamfikia Mwalimu bila kuzikwza pande zote yaani Lowassa, Mzee Kawawa na Mwalimu, Nyerere alikuja alihitimisha hoja hiyo huku akionekana kukasirishwa sana kitendo hicho kwa maneno yafuatayo:
1. Nyerere alimwambia Mzee Kasori, nenda umwambie Kawawa asiwe mjinga kama LOWASSA.

2. Nyerere alipokutana na Kawawa akamuuliza, Rashidi, nilimtuma Mzee Kasori akwambie usiwe mjinga kama LOWASSA, amekwambia?

3. Baada ya swali hilo Nyerere akamwambia, Kawawa, Lowassa ni mtoto mdogo sana kwa Mzee Kasori na kwa maana hiyo ni jasiri sana mpaka amtume mzee anayemzidi. Nyerere akaenda mbali akamwambia Kawawa, kwa vile umeniambia wewe maneno haya naamini angeniambia Mzee Samwel Kasori nisingeamini. NYERERE akasema ujasiri huu wa Lowassa kwa nini hakuutumia kutuambia ukweli kuhusu mali alizonazo nyingi kuzidi mimi(yeye Nyerere) ambaye nimekuwa rais wenu kwa kipindi kirefu?

4. Mwalimu alihitimisha mjadala wa LOWASSA kumuomba amsafishe Monduli ili asikose urais kwa kumwambia Kawawa, "Bwana Rashidi, nakuomba hivi, Kamwambie Mwenyekiti wa CCM, Mh. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowassa na nitagharamia mkutano huu kwa pesa zangu mwenyewe, kamwe msitumie pesa za Chama wala serikali, Monduli sitokwenda, kwa umri wangu, LOWASSA ni mtoto wangu tena mdogo sana na kwa heshima niliyonayo kwangu na kwa Chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina la bwana Lowassa asikose ubunge

Mzee, Samwel Kasori anamalizia kwa kusema " MKUTANO ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowassa.

Hadi Baba wa Taifa anafariki, sikuwahi na sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowassa anakanusha alivyolimbikiza mali akiwa tumishi wa CCM na Serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza"

Hila anazotumia Lowassa kuingia Ikulu ni za kutilia mashaka na wote wanaoitakia mema nchi yetu wanatakiwa kuwa makini na mbinu hizo
 
CCM imeingia mtegoni. Bila EL naiona kama vipande vipande. Wachague kusuka au kunyoa. Hapa panahitajika POTELEA MBALI LIWALO NA LIWE kumuacha huyu ndugu.
 
Huyu bwana anatupa mashaka maana anatumia nguvi nyingi sana kutaka kuingia Ikulu.

Ninawashangaa sana wanaomuunga mkono huyu bwana bila kujiuliza ana nia gani hasa na hii nchi.

Ukitaka kitu inabid utumie uwezo na assets zako kukipata.
Asingetumia hiyo nguvu, watu wangesema aah huyu hana nguvu hafiki popote.
Tunamsapoti coz there is no other better choice.
 
CCM imeingia mtegoni. Bila EL naiona kama vipande vipande. Wachague kusuka au kunyoa. Hapa panahitajika POTELEA MBALI LIWALO NA LIWE kumuacha huyu ndugu.

Muda wa kumuacha alikuwa zamani, too late now.
 
Baba wa taifa?Kwa yeye ndio nani?
Aende zake huko.

Mtu anayesaka madaraka kwa kutumia pesa hafai kupewa uongozi anatakiwa kuogopwa kama Ebola.Baba wa taifa wewe na upeo wako mdogo huwezi kumjua .
 
WanaJF,

Ni vizuri kuwa OBJECTIVE kama unataka kutoa hukumu kwa mtu. Kila mwanadamu ana mapungufu yake lakini kwenye suala la uongozi lazima tuangalie uwezo wa mtu hasa katika kusimamia TARATIBU, SHERIA na KANUNI. Lakini lililo kuu kabisa ni kuwa na mtu mwenye MAAMUZI au anayeweza kufanya MAAMUZI lakini siyo maamuzi magumu. Maamuzi magumu ni kushindwa kufikiri na kuwa na strategic thinking. Maamuzi magumu ni pale ambapo hakuna mbadala wa jambo fulani. Kwa mfano, hakukuwa na jinsi yoyote ambayo Mwl Nyerere angeacha kuamuru Jeshi la Tz kumpiga Idd Amini Dada.

Tutafakari kwa kina ila kama kuna watu ambao wanafikiri Lowassa hatakuwa Rais basi ni vizuri wakamrudia Mungu awaongoze sawa sawa maana mzee huyu kuliko aache kugombea na possibly kuwa Rais maisha yake yatakuwa mafupi sana kwa sababu amedhamiri. Binafsi naona ana sifa za kuwa Rais haya mengine ni vionjo tu vya kibinadamu ambavyo wewe na mimi pia tunavyo.
 
Sara yangu ya Leo. E Mungu tuondolee kikombe hiki sisi Waja wako Watanzania. Hii timu itatuacha watupu.

Umenena vyema mkuu watanzania siyo wajinga wa kusahau kama Lowasa anavyotegemea raisi ajaye atatoka nje ya ccm.
 
Back
Top Bottom