Lowassa ni mwepesi mno: Amezoea kushindwa

Lowassa ni mwepesi mno: Amezoea kushindwa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Ukimtazama na kumsikiliza Edward Ngoyai Lowassa unaweza kunibishia. Ukimtazama na kumsikiliza tena Lowassa utaniamini. Ukimtazama na kumsikiliza Lowassa kwa mara ya tatu, hutatamani kumtazama na hata kumsikiliza mara nyingine. Ni msanii kwelikweli. Lowassa anajipambanua kama dawa ya umaskini wa Tanzania. Ameshindwa vibaya kuuondoa umaskini wa Monduli tu aliyoiongoza kwa miaka 25 kama Mbunge.

Lowassa anapokaririwa akisema kuwa ndani ya CC na NEC hakuna wa kukata jina lake unaweza kumuamini. Anajichora kama mpambanaji na shujaa hasa. Anajichora kama mwenye misuli imara chamani na asiyezuilika. Mtazame tena Lowassa na utabadili mtazamo wako. Lowassa amejaa woga na kutojiamini. Ndiyo maana anashtukiashtukia. Anacheza filamu ya takwimu wakati wenzake wamesharejesha fomu na fomu zimeanza kuchambuliwa! Ameshindwa mapema.

Kulipokuwa na fukuto la ufisadi katika Jengo jipya la UVCCM, Lowassa aliingia kwenye mpambano na Nape Nnauye. Lowassa akiwa Waziri Mwandamizi Serikalini na mmoja wa wanabodi ya Udhamini ya UVCCM,Nape alikuwa kijana mdogo na mchanga ndani ya UVCCM. Nape alimpeleka puta Lowassa na kumlaza macho. Lowassa, kwa sisi wachambuzi,alishindwa na Nape.

Mwaka 2008, Lowassa aliingia tena ulingoni kupambana na Dr.Harrison Mwakyembe akiwa na Kamati yake teule ya Richmond. Hapa Lowassa alipigwa KO na kuishia kulalama na kulialia kutafuta huruma. Akasingizia kuwa Uwaziri Mkuu ndiyo uliolengwa. Angekuwa mpambanaji angepambana. Hata PM Pinda anamzidi. Pinda amebaki imara pamoja na Operesheni Tokomeza, Operesheni Kimbunga na Escrow.

Kwenye uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki (baada ya kifo cha Hayati Jeremiah Sumari), Lowassa alipanda tena ulingoni. Safari hii alikuwa kichama zaidi. Aliongoza kampeni za mgombea wa CCM na pia ni mkwewe, Sioyi Sumari. Akiwa katika uwanja wa nyumbani-karibu kabisa na Monduli, Lowassa aligaragazwa na kijana wa miaka 25 toka CHADEMA,Joshua Nassari aka Dogo Janja.

Sitaki kutaja kushindwa kwake kununua mvua za kutengeneza Thailand na hata Shule za Kata. Nataka mumtazame na kumsikiliza tena Lowassa halafu mshuhudie usanii wa mtangaza nia huyu. Chamani, Lowassa ni mwepesi na ameshazoea kushindwa. Hana upekee wowote na atayapokea matokeo yoyote Julai 12.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.
 
Kila nikiwaambia watu kwamba Lowassa si chochote na hata akikatwa hana madhara kwa CCM, watu hawaelewi. Lowasa anatishia nyau, lakini hakinka ATAKATWA. Aliondolewa Malechela kwenye kinyang'anyiro cha uraisi na likuwa tishio kweli enzi za Mkapa na chama hakikuyumba , sembuse huyu mnunuzi wa utu wa Mtanzania na kibaraka wa matajiri?
 
Kuna wakati Mungu akipanga mambo yake, huwafanya watu mioyo yao iwe migumu, ili kujidhihirisha utukufu wake kwao!. Mimi sizungumzii Julai 12, bali nazungumzia October 25!, hata Musa alipoanza harakati za kuwakomboa wana wa Israel, alikutana na vikwazo vingi ikiwemo Mungu kuifanya mioyo yao iwe migumu lakini mwisho wa siku, utukufu wake ulijidhihirisha wazi!.

Kwa Tanzania, huu ni mwaka wa lile "Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!"

"Wewe ni mwamba, na juu ya mwamba huu, nitalijenga taifa langu!" aliambiwa!.

Pasco
 
ikifika hiyo julai 12 ndio mtaamini kwamba lowasa ni rais ajaye wa taifa hili so hamna haja ya kuanza kubwabwaja bwabwaja tusubiri muda utasema tu just few days left
 
Hivi kama lowassa hafai mbona watu kila siku mnahangaika kumuongelea,tena maneno mengi yamekaa kishoga shoga,lowassa ni mwamba ambao hautikisiki kwa maneno ya kishoga shoga,let the Tanzanian decide what they want.
 
Umeyajuaje kama nawe si shoga? Kijana unapotea

Mzee Tupatupa

Kuwa mwanaume wa kweli,kama kuna mgombea wako kakutuma umchafue mtu sababu ya njaa zako na wewe ukakubari unaonyesha ni jinsi gani ure not strait,pambana kwa hoja ila sio kumchafua mtu bila sababu za msingi,na pili i am not ignorant like you.
 
Twende taratibu kijana. Hapo kwenye bandiko langu, uchafu ni upi? Bainisha hata neno moja la uongo hapo

Mzee Tupatupa
 
Kuwa mwanaume wa kweli,kama kuna mgombea wako kakutuma umchafue mtu sababu ya njaa zako na wewe ukakubari unaonyesha ni jinsi gani ure not strait,pambana kwa hoja ila sio kumchafua mtu bila sababu za msingi,na pili i am not ignorant like you.

anamchafuaje aliyekwishachafuka?....kama hajachafuka sema hizo milions anazogawa anazitoa wapi na kila mara anadai kusema ukweli kuhusu richmond mbona hasemi?
 
anamchafuaje aliyekwishachafuka?....kama hajachafuka sema hizo milions anazogawa anazitoa wapi na kila mara anadai kusema ukweli kuhusu richmond mbona hasemi?

Waamuzi wa mwisho ni watanzania.
 
Hivi kama lowassa hafai mbona watu kila siku mnahangaika kumuongelea,tena maneno mengi yamekaa kishoga shoga,lowassa ni mwamba ambao hautikisiki kwa maneno ya kishoga shoga,let the Tanzanian decide what they want.
Aache usanii, kwanza,anaoufanya ndio watu wataacha kumuongelea, kwani kila kukicha anakuja na usanii mpya watu watakaa kimya???! !!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom