Lowassa ni msomi, anapata nyomi

Lowassa ni msomi, anapata nyomi

Ni ule utakao wekwa na chama.
Hapo ndiyo penye tatizo, utawekwa lini? Chama kinatakiwa kiwe na utaratibu unaofuatwa na wote na siyo selective. Hili si jambo la dhatura au kusitukiza, linaeleweka wakati wote. Unakumbuka waziri mkuu aliye madarakani ametangaza nia (tena baada ya wengine kufungiwa) na hajafungiwa!
 
shida ni kwamba, kila mnapomponda huyo Lowasa, ndio mnavuta attention ya kila mtu kumfuatilia
 
hakuna mjeshi msomi, vyeti vyao vinaonesha kabisaaaaaa, hata kama watu wataogopa kusema
 
Usomi si tu wingi wa shahada,stashahada au astashahada. Usomi hasa ni uwezo wa kutumia elimu,hasa fani yako,katika maisha halisi. Ndivyo alivyo Lowassa. Lowassa ni msomi wa shahada ya sanaa toka UDSM. Amejifunza na kufuzu maigizo,ngoma,utunzi wa mashairi na mazingaombwe.

Sasa Lowassa anatumia usomi wake. Fani yake. Alipotamka tu Rais Kikwete kuwa wanachama wawashawishi wagombea wazuri,Lowassa akapata pa kutokea. Kwakuwa msomi wa usanii hupaswa kuwa sharp,mbunifu na muangalifu,Lowassa akatumia haraka fursa.

Kinachoonekana na kusikika sasa,ni zao la usomi wa Lowassa. Hakuna mwanasiasa mkongwe chamani mwenye usomi wa usanii kama Lowassa. Wengine hutumia usanii wa kuzaliwa tu. Usomi una raha yake!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
wachomeee
 
VUTA-NKUVUTE nimekusoma vizuri sana,ni kweli mheshimiwa kule songea alitangaza kuwa wenye hadhi ya kugombea inabidi washawishiwe na ndio kinachotokea .........ila wasiwasi wangu ni huyo anayeshawishiwa, ni kweli alikuwa hana nia mpaka masheikh, wachungaji na wanavyuo wamfuate ndio akubali? Kweli jamaa ametumia vizuri elimu yake ya sanaa..........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom