VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Usomi si tu wingi wa shahada,stashahada au astashahada. Usomi hasa ni uwezo wa kutumia elimu,hasa fani yako,katika maisha halisi. Ndivyo alivyo Lowassa. Lowassa ni msomi wa shahada ya sanaa toka UDSM. Amejifunza na kufuzu maigizo,ngoma,utunzi wa mashairi na mazingaombwe.
Sasa Lowassa anatumia usomi wake. Fani yake. Alipotamka tu Rais Kikwete kuwa wanachama wawashawishi wagombea wazuri,Lowassa akapata pa kutokea. Kwakuwa msomi wa usanii hupaswa kuwa sharp,mbunifu na muangalifu,Lowassa akatumia haraka fursa.
Kinachoonekana na kusikika sasa,ni zao la usomi wa Lowassa. Hakuna mwanasiasa mkongwe chamani mwenye usomi wa usanii kama Lowassa. Wengine hutumia usanii wa kuzaliwa tu. Usomi una raha yake!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam