Lowassa ni kama Jacob Zuma?

Lowassa ni kama Jacob Zuma?

kingxvi

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Posts
879
Reaction score
152
kwa hali inavyoendelea na jamaa anavyojipanga kuelekea ikulu hana tofauti na jacob zuma jinsi alivyosalitia na bwana thabo mbeki but kutokana na nguvu yake ndani ya ANC akafanya mapinduzi mpaka mwisho huyo ikulu na huyu jamaa ndo anafuata nyayo hizo
 
kwa hali inavyoendelea na jamaa anavyojipanga kuelekea ikuru hana tofauti na jacob zuma jinsi alivyosalitia na bwana thabo mbeki but kutokana na nguvu yake ndani ya ANC akafanya mapinduzi mpaka mwisho huyo ikulu na huyu jamaa ndo anafuata nyayo hizo
 
lowassa hawezi kuwa kama zuma hata kidogo.
huo urais ausahau.
 
usim underestimate lowassa. ana nguvu sana ndani ya ccm na nina hakika atateuliwa na chama. tatizo lake ana maadui wengi ndani ya chama hivyo watahakikisha hashindi. akiwa mjanja asigombee
 
alipoteza urais aliposema "there is a wish I am going to grant". Alikosea kudhani kuwa that wish was uwaziri mkuu. THAT WISH WAS URAIS.

na kwa kauli hiyo tutaraji kususa zaidi akipewa nafasi nyingine.
ningekuwa yeye ningefunga ng'ombe monduli
 
Unajua huyu jamaa sisi tunampa kichwa kuendelea kumjadili maana atadhani kwamba yeye ni mtu ambaye yuko mioyoni mwa watanzania. Ukweli ni kwamba nchi hii hawezi kukabidhiwa msanii wa vitendo na elimu yake!
 
Politics ni uchafu fulani tu,

Katika wanaomwandaa kwenda Ikulu wamo watu usioweza kuwaamini kabisa.
 
Kamwe Lowassa hawezi kuwa kama Zuma kwa sababu nyingi tu na chache kati ya hizo ni hiziz:

1. Hana support yoyote toka kwa wafanyakazi wa nchi hii ambao kwa SA ndiy walikuwa instrumental katika kumnyanyua Zuma;

2. Zuma alikuwa na eloquence ya hali ya juu na alishuka mpaka kwa watu wa kawaida na vijana ambao ndiy walikuwa chachu ya ushindi wake. By the way huyu wa kwetu hapa amewahi hata kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC, Sauti ya Ujerumani au hata VOA? kwa lugha gani?;

3. Mbeki alionekana kama mtu ambaye anajali maslahi ya matajiri na watu weupe na kuwaacha watu weusi na wala wa kima cha chini (kwa hapa kwetu sifa hizi za Mbeki ndizo za Lowassa);

4. Zuma alikuwa na constituency, kwa maana ya kwamba alikuwa ni 'undisputed king' wa wazulu na hao walimpa boost kubwa hasa kwa vile ndilo kabila kubwa kuliko yote. Huyu bwana hapa kwetu hata hao wamasai wenyewe wamem-disown wakidai ni mmeru na hata wangemuunga mkono, hawatoshi kumpa jeuri.

5. Kwa ujumla uungwaji mkono wa huyu bwana umebaki kwa wenye njaa wachache wanaoingia kwenye vikao vya chama na wengine sasa wameanza kumgundua na kuchoshwa na hila zake za hujuma na kiu yake ya kuutaka urais.
 
Acheni hofu watanzania. Huyu bwana ana muda mfupi sana kabla hajaumbuka zaidi na kutamani hata asingeutolea macho huo urais unaomnyima raha na hata kukatiza usingizi kwa ndoto za mara kwa mara.

Hatuwezi kuurejesha ukoloni tena hata kama mkoloni wa sasa ni mweusi mwenzetu.
 
Tutofautishe kasfa binafsi kama za vimada na kashfa za kuliibia taifa. Hawa ni watu tofauti
 
Mkuu nakupa big up! Pamoja na kwamba hata huyu wa kwetu kashfa hiyo haimpiti lakini kweli kashfa ya wizi ni capital offence na haisameheki!
 
lakini mapinduzi anayoyapanga jamaa ndani ya chama ni kama aliyoyafanya jacob zuma cz alianza na ndani ya chama
 
Hata Yesu arudi kesho hili halitawezekana....!
 
Kamwe Lowassa hawezi kuwa kama Zuma kwa sababu nyingi tu na chache kati ya hizo ni hiziz:

1. Hana support yoyote toka kwa wafanyakazi wa nchi hii ambao kwa SA ndiy walikuwa instrumental katika kumnyanyua Zuma;

2. Zuma alikuwa na eloquence ya hali ya juu na alishuka mpaka kwa watu wa kawaida na vijana ambao ndiy walikuwa chachu ya ushindi wake. By the way huyu wa kwetu hapa amewahi hata kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC, Sauti ya Ujerumani au hata VOA? kwa lugha gani?;

3. Mbeki alionekana kama mtu ambaye anajali maslahi ya matajiri na watu weupe na kuwaacha watu weusi na wala wa kima cha chini (kwa hapa kwetu sifa hizi za Mbeki ndizo za Lowassa);

4. Zuma alikuwa na constituency, kwa maana ya kwamba alikuwa ni 'undisputed king' wa wazulu na hao walimpa boost kubwa hasa kwa vile ndilo kabila kubwa kuliko yote. Huyu bwana hapa kwetu hata hao wamasai wenyewe wamem-disown wakidai ni mmeru na hata wangemuunga mkono, hawatoshi kumpa jeuri.

5. Kwa ujumla uungwaji mkono wa huyu bwana umebaki kwa wenye njaa wachache wanaoingia kwenye vikao vya chama na wengine sasa wameanza kumgundua na kuchoshwa na hila zake za hujuma na kiu yake ya kuutaka urais.
Hapo umenena asiyekuelewa ni ni yule asiyetaka kwani ukweli ndio huo.
 
kwa hali inavyoendelea na jamaa anavyojipanga kuelekea ikulu hana tofauti na jacob zuma jinsi alivyosalitia na bwana thabo mbeki but kutokana na nguvu yake ndani ya ANC akafanya mapinduzi mpaka mwisho huyo ikulu na huyu jamaa ndo anafuata nyayo hizo

Huna habari, mwaka 2015 EL atajiunga na CHADEMA na kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia chama hicho. Na mazungumzo kati yao yameisha kamilika inasubiriwa muda tu
 
kwa hali inavyoendelea na jamaa anavyojipanga kuelekea ikulu hana tofauti na jacob zuma jinsi alivyosalitia na bwana thabo mbeki but kutokana na nguvu yake ndani ya ANC akafanya mapinduzi mpaka mwisho huyo ikulu na huyu jamaa ndo anafuata nyayo hizo

attachment.php
 
Attachments

  • Bounce+back+by+Jacob+Zuma.jpg
    Bounce+back+by+Jacob+Zuma.jpg
    21 KB · Views: 154
Jamani mwenzenu ndiyo kwanza uchovu wa kampeni ya urais 2010 bado haujaisha, wakati huo wenzangu mshaanza kampeni za 2015!

Nyie mgekuwa watoto na mimi baba yenu, basi nisingewapa urithi.....!
 
Back
Top Bottom