Lowassa ndiyo kimbilio letu Watanzania kuelekea kwenye mafanikio

Wana JF.
Historia inajibainisha yenyewe kwamba watu makini wa sampuli kama ya Lowassa hawachelei kurejea nafasi za hapo awali.

Na ujio wao huwa ni wa kishindo kikubwa na hicho kishindo ndicho haswa kinawatia viwewe wale mahasimu wake wa kisiasa kutokana na kuona wazi wazi kushindwa kuhimili historia ya utendaji kazi wa Lowassa unaotambulika na kukubalika ndani ya jamaii.

Sote tumeshudia utendaji wa Lowassa kwa nyakati zote tangu mwaka 1975, Mbunge wa Monduli kwa kipindi chote hicho kaweza kufanya mambo yanayoonekana kwa macho ambapo kwa namna mojo ama nyingine yataendelea kuwanafaisha waliopo na vizazi vijavyo.

Lowassa, alipigana vilivyo ongezeko la shule, hakuwapa nafasi ya kupumua wakuu wa mikoa wa wilaya katika ujenzi wa shule hizo.

Hali hiyo ilisababisha ongezeko kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 15,816 mwaka 2010 ambalo ni sawa na ongezeko la wastani wa shule 1559 hali iliyowezesha wanafunzi kuongezeka kutoka 7,541,208 hadi 8,419,305. Haya yote ni matunda ya kazi ya Edward Lowassa.

Tunakumbuka ya kwamba huyu huyu Lowassa aliweza kuvunja mkataba mbovu wa City Water kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Lowassa alipokuwa Waziri wa Ardhi alisimama kidete pale alipogundua Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamempa mfanyabiashara eneo la Mnazi Mmoja.

Lowassa hakubaliana na uamuzi huo na kuamuru wananchi wauvunje uzio wake na mabati aliyoweka na hivyo eneo la uwanja kurudi kwa Serikali na Wananchi

inawezekana akawa kiongozi mzuri, lakini kwakuwa anatoka katika chama kibovu ccm hafai kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi kumi
 
Lowasa nakumbuka alikuja tanga akamshusha kiongozi mbovu bila ya kumuangalia usoni tena ilisemekana el. ndio alimuweka pale Tanga ambapo mtu mwingine hawezi fanya hivyo.
 
Ha! Ha! Ha! Ha! Unanikumbusha mbali sana...Nungu FC juzi wamefiwa na mtu wao muhimu Mwenyekiti Babu Chela.

Mkuu kumbe na wewe wa maeneo yale nini? Nilikuwa sijajua huo msiba shukurani kwa taarifa. Tumefukuzwa maeneo hayo bwana na watu wa Mrima!
 
Kipindi cha Lowassa, kumekuwepo na ongezeko la wanafunzi wanaosoma sekondari kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1.638,669.

Kazi hii nzuri ilifanyika ndani ya kipindi kifupi tu.
 
Mkuu mie mitaa yangu Aggrey kule Congo kwa jamaa si hunajua tena zamani Kariakoo wote tunajuana..pole sana mkuu...unamjua Picadili?
 
Watanzania haswa wale wa kanda ya Ziwa hawatamsahau Lowassa katika maisha yao. Hali hii ilitokana na uthubutu wa kuhoji uhalali wa maji ya ziwa Victoria kwenda Misri kupitia Suez Canal wakati wa kanda ya ziwa hawana maji.

Lowassa alivunja mkataba huo wa kikoloni na sasa wananchi wa Mwanza, Shinyanga na Kahama wananufaika na maji ya Ziwa Victoria kwa matumizi mbalimbali mradi uliogharimu zaidi ya Bilioni 200 lakini una manufaa kwa vizazi na vizazi

Kweli EL ni mwanaume kama kweli aliweza kuvunja mkataba (wa Misri na Uingereza) ambao yeye hakushiriki kuusaini. Napata taabu kidogo hapo pamoja na sifa zake nyingi unazotangaza.
 
Kipindi cha Lowassa, kumekuwepo na ongezeko la wanafunzi wanaosoma sekondari kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1.638,669.

Kazi hii nzuri ilifanyika ndani ya kipindi kifupi tu.

Hili halina ubishi. Japo asilimia kubwa ya shule hizi zina mwalimu mmoja, hazina madawati, hazina maabala wala nyumba za walimu. Walimu wakipangwa huripoti na kuondoka. Nadhani angelenga ubora wa elimu kuliko wingi wa wanafunzi na madarasa wanaovuka madarasa pasipo kupata fursa ya kufundishwa. Nasikitika kusema kwa hili kulikuwa na kukurupuka.
 
Mhhh let's wait .. but sintopenda kuona chadema wanaingia ikulu ..
 
Kweli EL ni mwanaume kama kweli aliweza kuvunja mkataba (wa Misri na Uingereza) ambao yeye hakushiriki kuusaini. Napata taabu kidogo hapo pamoja na sifa zake nyingi unazotangaza.

Msome vizuri Mchuzi wa Bata, kataja kazi alizofanya Lowassa, sio sifa.
 
Jana nilikuwa kwenye vijiwe vya vijana fulani hivi wa maeneo ya hapa dar. Kulikuwa na vijana kama kumi hivi nikajichanganya nao wakaninunulia tangawizi nikawa nakunywa. Gumzo likawa kuhusu uongozi wa nchi hii: vijana wakawa wanabadilishana mawazo kuhusu rais ajaye. Nilishangaa sana kwani vijana saba kati ya wale kumi walisema kwamba nchi hii anatakiwa Lowassa kwa kuwa anaweza kusimamia mambo. Wakasema Lowassa aliwaletea maji watu wa shinyanga. Nikawaambia mbona Lowassa ana kashfa basi mmoja wao akaniuliza hivi nchi hii nani si mwizi? Nikanyamaza kimya nikanywa tangawizi yangu nikaondoka kwenda kunywa Jack Daniels zangu. Sikuwa na jibu nikawaahidi nitarudi leo!
Hivi ninyi watu mnalipwa shillingi ngapi? Mbona hata watoto wadogo vijijini wanajua kuwa maadui wa jamii sasa hivi ni wanne: Ujinga, maradhi umaskini na Lowasa!
 
Wana JF.
Historia inajibainisha yenyewe kwamba watu makini wa sampuli kama ya Lowassa hawachelei kurejea nafasi za hapo awali.

Na ujio wao huwa ni wa kishindo kikubwa na hicho kishindo ndicho haswa kinawatia viwewe wale mahasimu wake wa kisiasa kutokana na kuona wazi wazi kushindwa kuhimili historia ya utendaji kazi wa Lowassa unaotambulika na kukubalika ndani ya jamaii.

Sote tumeshudia utendaji wa Lowassa kwa nyakati zote tangu mwaka 1975, Mbunge wa Monduli kwa kipindi chote hicho kaweza kufanya mambo yanayoonekana kwa macho ambapo kwa namna mojo ama nyingine yataendelea kuwanafaisha waliopo na vizazi vijavyo.

Lowassa, alipigana vilivyo ongezeko la shule, hakuwapa nafasi ya kupumua wakuu wa mikoa wa wilaya katika ujenzi wa shule hizo.

Hali hiyo ilisababisha ongezeko kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 15,816 mwaka 2010 ambalo ni sawa na ongezeko la wastani wa shule 1559 hali iliyowezesha wanafunzi kuongezeka kutoka 7,541,208 hadi 8,419,305. Haya yote ni matunda ya kazi ya Edward Lowassa.

Tunakumbuka ya kwamba huyu huyu Lowassa aliweza kuvunja mkataba mbovu wa City Water kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Lowassa alipokuwa Waziri wa Ardhi alisimama kidete pale alipogundua Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamempa mfanyabiashara eneo la Mnazi Mmoja.

Lowassa hakubaliana na uamuzi huo na kuamuru wananchi wauvunje uzio wake na mabati aliyoweka na hivyo eneo la uwanja kurudi kwa Serikali na Wananchi

Na katika mchakato huo, akafanikiwa kuwa milionea wa kupitia siasa, na tajiri kuliko mwanasiana mwingine yoyote aliyepata kutokea katika jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Wana JF.
Historia inajibainisha yenyewe kwamba watu makini wa sampuli kama ya Lowassa hawachelei kurejea nafasi za hapo awali.

Na ujio wao huwa ni wa kishindo kikubwa na hicho kishindo ndicho haswa kinawatia viwewe wale mahasimu wake wa kisiasa kutokana na kuona wazi wazi kushindwa kuhimili historia ya utendaji kazi wa Lowassa unaotambulika na kukubalika ndani ya jamaii.

Sote tumeshudia utendaji wa Lowassa kwa nyakati zote tangu mwaka 1975, Mbunge wa Monduli kwa kipindi chote hicho kaweza kufanya mambo yanayoonekana kwa macho ambapo kwa namna mojo ama nyingine yataendelea kuwanafaisha waliopo na vizazi vijavyo.

Lowassa, alipigana vilivyo ongezeko la shule, hakuwapa nafasi ya kupumua wakuu wa mikoa wa wilaya katika ujenzi wa shule hizo.

Hali hiyo ilisababisha ongezeko kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 15,816 mwaka 2010 ambalo ni sawa na ongezeko la wastani wa shule 1559 hali iliyowezesha wanafunzi kuongezeka kutoka 7,541,208 hadi 8,419,305. Haya yote ni matunda ya kazi ya Edward Lowassa.

Tunakumbuka ya kwamba huyu huyu Lowassa aliweza kuvunja mkataba mbovu wa City Water kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Lowassa alipokuwa Waziri wa Ardhi alisimama kidete pale alipogundua Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamempa mfanyabiashara eneo la Mnazi Mmoja.

Lowassa hakubaliana na uamuzi huo na kuamuru wananchi wauvunje uzio wake na mabati aliyoweka na hivyo eneo la uwanja kurudi kwa Serikali na Wananchi

You are entitled to your opinion. Lakini ngoja tukuambie. Poverty cycle katika nchi hii itavunjwa kwa kufanya massive investments kwenye nishati na hasa umeme. Wewe unafahamu kwamba ukiwa na umeme wa uhakika na wenye bei nafuu, gharama za uzalishaji katika nyingi ya consumables hushuka na hivyo kupunguza mfumuko wa bei. Umeme wa uhakika na wa bei nafuu unachochea uwekezaji wa hali juu utakaotoa ajira za uhakika na hivyo kupunguza jeshi la wasio na ajira ambalo yeye ameliita ni bomu linalotaka kupasuka.

Tunapozungumzia nishati, na hasa umeme, inanikumbusha TANESCO na mchakato wa Richmond ambao yeye aliungilia kwa maslahi yake na kuufanyia ufisadi unaoigharimu TANESCO na nchi hii mabilioni ya shilingi kila mwezi. TANESCO iko ICU na moja ya sababu ni mikataba tata na ya kinyonyaji, ukiwemo ule wa Richmond. Lowassa ananufaika na malipo ya Dowans na inasemekana yeye na mshirika wake wamchota zaidi ya dola milioni 80 kwa mikataba ya kifisadi na bado yeye ni mnufaika wa malipo ya bilioni 90 ya Dowans. Haishangazi kuona kwamba ana fedha nyingi na ananunua ufuasi mkubwa wa kumpigia debe humu jamvini na nyingine kuwanunua viongozi wa nyumba zetu za ibada.

Ni kweli Lowassa alishawishi serikali kuvunja mkataba wa Bi-Water na Dawasco. Hata kama alidai amefanya hivyo kwa maslahi ya nchi na kwa nia njema, hatua hii iliigharimu serikali zaidi ya dola milioni 11 za gharama za uendeshaji wa kesi. Kiasi hiki ni kikubwa kuliko kile ambacho kingelipwa kwa kampuni hii, kama wangeenedelea na mkataba wao mpaka pale ambapo ungekuwa umeishia. Alifanya hivyo akijua kwamba miwsho wa yote yeye atanufaika kwa kupata sehemu ya mgao wa legal fees.

Na hiki kichekesho cha mradi wa maji wa ziwa Victoria. mradi huu uliasisiwa na serikali ya awamu ya tau kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kuridhiwa utekelezaji wake na baraza la mawaziri. Uliasisiwa toka enzi za mzee Mwinyi na upembuzi yakinifu ulifanyika miaka ya mwanzoni mwa tisini. Yeye kama kiongozi mwingine yeyote wa wizara husika alikuwa na jukumu la kuutekeleza. Na hili la kutetea matumizi ya bonde la mto Nile, ni suala ambalo lilikuwa na msimamo thabiti wa baraza la mawaziri na serikali ilimtuma yeye kama msemaji wa wizara kwenda kuwasilisha msimamo wa nchi.

Unazungumzia suala la yeye Lowassa kweza kuondoa njaa. Hiki ni kichekesho kwa sababu angetakiwa kuanza kufanya hivyo Monduli, kabla hajafikiria watu wa makete na Nanyumbu au Misenyi. Monduli imekuwa ikiishi kwa chakula cha msaada kila mwaka, leo huyu aliyeshindwa kuwasaidia watu wake wasiozidi laki 4 ndo ataweza kuokoa mamilioni ya watanzania?

Kwa ujumla, kama nchi hii inataka suluhisho la matatizo yetu basi hatua inayopasa kuchukuliwa ni kumfikisha mahakamani Lowassa na washirika wake na kuwafilisi na kuwaamuru kurejesha matrilioni yote waliyowaibia wananchi. Kamwe hatuwezi kukubali usemi wa mchawi mpe mwana akulelee kama msingi wa kutauta matatizo yetu.
 
Safi sana, hayo uliyosema hayafiki hata 1/8 ya aliyofanya mteule huyu. Yapo mengi, mengi makubwa. Anapigwa vita ambavyo maadui sasa wanaelemewa na kubaki wakitoa visingizi visivyo na msingi..

smart people talk and justfy by evidence
and aurgu strongly!unaposema kafanya mengi yapi hayo make amekuwa kwenye system toka miaka ya sabini hadi anateuliwa kuwa mkurungenzi wa aicc it was 1989, now tell us kafanya nini, shule kajenga sawa then kinachoendela ni nini? it is a failed plan!tusishadadie vitu vya kijinga na kutukuza ujambazi badala yake tuwe na mwamko wa kifikra na kutafuta utatuzi wa matatizo ya nchi kwa kutumia watu wenye intergrity isiyo na mashaka!
 
Hili halina ubishi. Japo asilimia kubwa ya shule hizi zina mwalimu mmoja, hazina madawati, hazina maabala wala nyumba za walimu. Walimu wakipangwa huripoti na kuondoka. Nadhani angelenga ubora wa elimu kuliko wingi wa wanafunzi na madarasa wanaovuka madarasa pasipo kupata fursa ya kufundishwa. Nasikitika kusema kwa hili kulikuwa na kukurupuka.

watanzania wanalenga zaidi zaidi kwenye wingi na sio ubora, huu ni ufinyu wa fikra!
 
Wana JF.
Historia inajibainisha yenyewe kwamba watu makini wa sampuli kama ya Lowassa hawachelei kurejea nafasi za hapo awali.

Na ujio wao huwa ni wa kishindo kikubwa na hicho kishindo ndicho haswa kinawatia viwewe wale mahasimu wake wa kisiasa kutokana na kuona wazi wazi kushindwa kuhimili historia ya utendaji kazi wa Lowassa unaotambulika na kukubalika ndani ya jamaii.

Sote tumeshudia utendaji wa Lowassa kwa nyakati zote tangu mwaka 1975, Mbunge wa Monduli kwa kipindi chote hicho kaweza kufanya mambo yanayoonekana kwa macho ambapo kwa namna mojo ama nyingine yataendelea kuwanafaisha waliopo na vizazi vijavyo.

Lowassa, alipigana vilivyo ongezeko la shule, hakuwapa nafasi ya kupumua wakuu wa mikoa wa wilaya katika ujenzi wa shule hizo.

Hali hiyo ilisababisha ongezeko kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 15,816 mwaka 2010 ambalo ni sawa na ongezeko la wastani wa shule 1559 hali iliyowezesha wanafunzi kuongezeka kutoka 7,541,208 hadi 8,419,305. Haya yote ni matunda ya kazi ya Edward Lowassa.

Tunakumbuka ya kwamba huyu huyu Lowassa aliweza kuvunja mkataba mbovu wa City Water kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Lowassa alipokuwa Waziri wa Ardhi alisimama kidete pale alipogundua Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamempa mfanyabiashara eneo la Mnazi Mmoja.

Lowassa hakubaliana na uamuzi huo na kuamuru wananchi wauvunje uzio wake na mabati aliyoweka na hivyo eneo la uwanja kurudi kwa Serikali na Wananchi

mbona umesahau alivyojimilikisha lunch za taifa????
 
Hivi ninyi watu mnalipwa shillingi ngapi? Mbona hata watoto wadogo vijijini wanajua kuwa maadui wa jamii sasa hivi ni wanne: Ujinga, maradhi umaskini na Lowasa!

Na wewe umelipwa shilingi ngapi? Watoto wadogo wa kijijini kwenu hao! Mtu ukitoa mawazo yako unakuwa umelipwa? Basi kila nayeandika humu amelipwa ukiwemo wewe ambaye umelipwa sijui na nani ili uje kuyasema hayo uliyoyasema.
 
Watanzania haswa wale wa kanda ya Ziwa hawatamsahau Lowassa katika maisha yao. Hali hii ilitokana na uthubutu wa kuhoji uhalali wa maji ya ziwa Victoria kwenda Misri kupitia Suez Canal wakati wa kanda ya ziwa hawana maji.

Lowassa alivunja mkataba huo wa kikoloni na sasa wananchi wa Mwanza, Shinyanga na Kahama wananufaika na maji ya Ziwa Victoria kwa matumizi mbalimbali mradi uliogharimu zaidi ya Bilioni 200 lakini una manufaa kwa vizazi na vizazi

Watu wengine bwana sijui mnatolewa wapi??
  1. huo mradi wa waji toka ziwa victoria aliinitiate Mkapa na ndio maana hata wakati wa ufunguzi credit zilienda kwa Mkapa na wala sio Lowassa
  2. hao wanaowapa hela kuwa kampenia humu muwe mnawaambia kwanza wawapeleke shule eeeeh! et maji kutoka lake victoria yanapitia suez canal kwenda Egypt (Misri).......... inaelekea huna uelewa wowote wewe ila unatumika tu. toka lini mto nile umekuwa canal tena ya suez. nakushauri rudi kwenye makabrasha library unaweza pata hata elimu kidogo ya haya mambo kwa ujumla.
  3. wewe .......................................
 
watu wengine bwana sijui mnatolewa wapi??
  1. huo mradi wa waji toka ziwa victoria aliinitiate mkapa na ndio maana hata wakati wa ufunguzi credit zilienda kwa mkapa na wala sio lowassa
  2. hao wanaowapa hela kuwa kampenia humu muwe mnawaambia kwanza wawapeleke shule eeeeh! Et maji kutoka lake victoria yanapitia suez canal kwenda egypt (misri).......... Inaelekea huna uelewa wowote wewe ila unatumika tu. Toka lini mto nile umekuwa canal tena ya suez. Nakushauri rudi kwenye makabrasha library unaweza pata hata elimu kidogo ya haya mambo kwa ujumla.
  3. wewe .......................................

nakuwa na wasiwasi na wasomi wa tanzania, kama wako hivi basi ukombozi wa taifa letu una kazi kubwa sana, unawaza kumsimika rais ambaye kimsingi intergrity yake ni questionable na sio kuwa anasingiziwa???tutamature lini sisi, wasomi mchango wenu ni upi ktk taifa hili?nani asiyejua mtu huyu, nadhani kuna watu wamekula pesa za kumkampenia na sio kwamba hawajui ukweli lakini watambue kwa namna moja au nyingine watakuwa washukiwa wakuu wanaotumika kuangamiza nchi kwa mara ya tatu mfululizo yani kuazia mkapa kikwete na sasa huyu huyu anayeona ikula na kuililia sijui anatafuta nini!
 
Wakubali wakatae El for 2015.Wakigoma kama kawaida wapige mbizi tu
 
Back
Top Bottom