Lowassa ndiyo kimbilio letu Watanzania kuelekea kwenye mafanikio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa ndiyo kimbilio letu Watanzania kuelekea kwenye mafanikio

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mshume Kiyate, Jan 21, 2012.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana JF.
  Historia inajibainisha yenyewe kwamba watu makini wa sampuli kama ya Lowassa hawachelei kurejea nafasi za hapo awali.

  Na ujio wao huwa ni wa kishindo kikubwa na hicho kishindo ndicho haswa kinawatia viwewe wale mahasimu wake wa kisiasa kutokana na kuona wazi wazi kushindwa kuhimili historia ya utendaji kazi wa Lowassa unaotambulika na kukubalika ndani ya jamaii.

  Sote tumeshudia utendaji wa Lowassa kwa nyakati zote tangu mwaka 1975, Mbunge wa Monduli kwa kipindi chote hicho kaweza kufanya mambo yanayoonekana kwa macho ambapo kwa namna mojo ama nyingine yataendelea kuwanafaisha waliopo na vizazi vijavyo.

  Lowassa, alipigana vilivyo ongezeko la shule, hakuwapa nafasi ya kupumua wakuu wa mikoa wa wilaya katika ujenzi wa shule hizo.

  Hali hiyo ilisababisha ongezeko kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 15,816 mwaka 2010 ambalo ni sawa na ongezeko la wastani wa shule 1559 hali iliyowezesha wanafunzi kuongezeka kutoka 7,541,208 hadi 8,419,305. Haya yote ni matunda ya kazi ya Edward Lowassa.

  Tunakumbuka ya kwamba huyu huyu Lowassa aliweza kuvunja mkataba mbovu wa City Water kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

  Lowassa alipokuwa Waziri wa Ardhi alisimama kidete pale alipogundua Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamempa mfanyabiashara eneo la Mnazi Mmoja.

  Lowassa hakubaliana na uamuzi huo na kuamuru wananchi wauvunje uzio wake na mabati aliyoweka na hivyo eneo la uwanja kurudi kwa Serikali na Wananchi
   
 2. magistergtz

  magistergtz JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kweli kabisa. Lowassa anafaa na ndo mtu pekee ( labda na Maghufuli) ambae ataifanya ccm ishinde 2015
   
 3. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Safi sana, hayo uliyosema hayafiki hata 1/8 ya aliyofanya mteule huyu. Yapo mengi, mengi makubwa. Anapigwa vita ambavyo maadui sasa wanaelemewa na kubaki wakitoa visingizi visivyo na msingi..
   
 4. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hizo kampeni zenu chafu za kuosha kaniki haziwafikishi popote. Huyo mnayemtetea hauziki hata kwenye gulio. Ni mwizi, mjivuni, na mwenye tamaa ya madaraka
   
 5. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Lowassa ni muhujumi uchumi hatufi na wala hafai kuongoza Tanganyika yetu, labda akaongoze familia yenu,. Kama unampenda nenda kamuombe awe mkuu wa familia yenu, hawezi kuwakiongozi wa Tanganyika yangu
   
 6. B

  BigMan JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mbona umesahau na mengine ikiwa ni pamoja na kuuza nyumba za nhc kama zake kwa madai ya kwamba zinarejeshwa kwa wamiliki wake wa awali, alitafuna fedha za mafuriko ya korogwe, alipiga teni parcent ya magari ya awali ya wabunge, alitafuna mamilioni ya fedha akiwa aicc na la hivi karibuni kawadhulumu vijana wa kimasai fedha walizochangisha katika marathoni iliyofanyika london kiasi cha dola 100,000
   
 7. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu hivi hunaweza kuyatolea ushahidi wa hayo maneno yako?

  Tunapaswa kufahamu kuwa hakuna binadamu aliyemkamilifu kwa asilimia zote isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee.

  Hivyo kwa Lowassa kama binadamu, pamoja na wewe kila mmoja na ana mapungufu yake!
   
 8. a

  adobe JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  lowasa na jk nani mwizi zaidi?mbona hata EPA kinara ni jk hadi kutaka kum mwakyeke gavana.
   
 9. a

  adobe JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  kijeba cha roho.tz inatakiwa mpiga kazi ka el ili muache kucheza bao.anaehujumu uchumi ni jk badala ya kufanyakazi anatumia rasilimali zetu kujenga mahoteli na kumnunulia riz magari
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ingekuwa vizuri kama ungekuja na facts na data za kutosha ili kuthibitisha maneno yako, ulichofanya wewe umekuja na maneno matupu kwenye uwanja wa Graat Thinkers!!
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Jamani ujasiriamali wowote ambao unaingiza pesa unakubalika, naomba mnPM na mimi ili nijiunge kwenye hilo kundi la kumsafisha Lowasa maana inaonekana limetengewa bajeti nzuri.
  Msiwe na mashaka na mimi nitabadili ID na nitampigia kampeni kwa nguvu zangu zote maana hii njaa sasa imetamalaki.
   
 12. l

  lilove Member

  #12
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hilo ni kimbilio lako si la watanzania
   
 13. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tupende tusipende, nchi yetu yapasa kuongozwa na mtu asiyeona haya, mithili ya kuvaa ngozi ya kondoo usoni. Nchi haiwezi kupiga hatua kwa kucheka, kutabasamu, kutotoa maamuzi, kutegemea misaada, kutokuwa na misingi ya kujitegemea kiuchumi. kutotolea ufafanuzi wa kina wa mambo mazito ya nchi hususan-UCHUMI.
  Lowassa angeendelea kuwepo madarakani baa la njaa lingepungua kama si kuisha, alishaweka mikakati na premier wa Thailand juu ya kilimo cha mvua za kutengeneza...na alishazuru nchi hiyo kwa minajili ya kukuza kilimo na si KILIMO KWANZA.
  Ukitazama kwa mapana:-
  • Alianza kwa suala la kujenga shule za chini na azma kuziboresha.
  • akaelekeza akisi kwenye kilimo na alishatembelea Thailand.
  • Ambacho angefatia nacho ilikuwa ni jinsi ya kutengeneza ajira mpya hususan kwa rika la vijana.
  Japo anazo scandals pesa zikimkalia mbele...waila ni mtendaji zaidi na zaidi. Namwamini kiutendaji na ufuatiliaji wake.
   
 14. l

  lilove Member

  #14
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tena ni jambawazi huyo
  nani kakwambia jambazi anawema akitaka lake hata kama kukuua atakuua
   
 15. l

  lilove Member

  #15
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna upungufu na uchafu visifananishwe
   
 16. l

  lilove Member

  #16
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe njaa nmdo inawasumbua hao wapiga debe, kweli njaa mbaya
   
 17. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kizuri chajiuza wakulu....
  Naona mnakaribia kupasuka misuli ya makolomelo kwa kupaza sauti za sifa na utukufu wa huyo bwana!
  Ahsante tumewasikia, nadhani kuna mda na mahali sahihi mtayaeleza hayo na labda mambo yatakuwa kama mnavyotaka..... Yaani Rais wa JMT..... Lol
   
 18. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania haswa wale wa kanda ya Ziwa hawatamsahau Lowassa katika maisha yao. Hali hii ilitokana na uthubutu wa kuhoji uhalali wa maji ya ziwa Victoria kwenda Misri kupitia Suez Canal wakati wa kanda ya ziwa hawana maji.

  Lowassa alivunja mkataba huo wa kikoloni na sasa wananchi wa Mwanza, Shinyanga na Kahama wananufaika na maji ya Ziwa Victoria kwa matumizi mbalimbali mradi uliogharimu zaidi ya Bilioni 200 lakini una manufaa kwa vizazi na vizazi
   
 19. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kama hauko kwenye pay roll yake basi utakuwa umetoroka hospitali ya Milembe!!!
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Jana nilikuwa kwenye vijiwe vya vijana fulani hivi wa maeneo ya hapa dar. Kulikuwa na vijana kama kumi hivi nikajichanganya nao wakaninunulia tangawizi nikawa nakunywa. Gumzo likawa kuhusu uongozi wa nchi hii: vijana wakawa wanabadilishana mawazo kuhusu rais ajaye. Nilishangaa sana kwani vijana saba kati ya wale kumi walisema kwamba nchi hii anatakiwa Lowassa kwa kuwa anaweza kusimamia mambo. Wakasema Lowassa aliwaletea maji watu wa shinyanga. Nikawaambia mbona Lowassa ana kashfa basi mmoja wao akaniuliza hivi nchi hii nani si mwizi? Nikanyamaza kimya nikanywa tangawizi yangu nikaondoka kwenda kunywa Jack Daniels zangu. Sikuwa na jibu nikawaahidi nitarudi leo!
   
Loading...