Lowassa na siasa za makanisani?

Lowassa na siasa za makanisani?

Mkuu,
Alikuwa parokia ya Rwamlimi jimbo la Musoma jumapili iliyopita kuongoza harambee kama hii. Nashindwa kujua kama mialiko hii ina baraka za maaskofu wa majimbo husika.

Haiahitaji baraka za askofu kumualika mtu kuchangia ujenzi! Acheni unafiki, pengo alishasema kanisa halitawatenga watuhumiwa wa ufisadi! Hata Yesu alikula kwa Zakayo!
 
kikwete bilionea,ridhiwan bilionea,.hakuna ufisadi zaidi ya huu..richmond ilikuwa deal ya jk na rostam ndio maana lowasa anaamini he is clean enough to be president na ccm hawawezi kumfukuza for they know who is behind richmond scam.
 
Du hii nayo imetulia,Roman Catholic kwa umakini walio nao, hili la huyu jamaa du LITALETA UTATA KWENYE JAMII.Japo Edward yaweza kuwa katubu lakini kwa hali ya tafsiri ya UMMA [WATANZANIA] kwa yale waliyoyasikia kuhusu Edward kupitia vyombo halali vya habari vya Umma na binafsi na walio wengi hasa kwenye miji yetu mikuu na wilayani kutoa tafsiri ya hukumu dhidi yake basi,ni vigumu kwa mtu huyu kupata tiketi ya UMMA huo huo uliolishwa taarifa ama ya UKWELI ama YA UONGO dhidi ya Mtuhumiwa kumpa nafasi ya KUJITANABAISHA NA KUNDI AMBALO AMECHAFULIWA KWAO HIVYO KUMPA SIFA ZA KUTOSHA KUMTOA KWENYE KADA YA KUWA KIONGOZI WA SHUGHULI ZA UMMA ZIWE NI ZA KIROHO AU KIJAMII.

Manake hii ni sawa na tafsiri ya Mwalimu Nyerere na liwaya za Mtukufu Cizar na Mkewe,Kwani kitendo cha Mke wa Mtukufu huyu kutuhumiwa kwa jambo ovu basi kinatoa dhamana ya kuto aminika kwa Mke wa Cizar kwa jamii ambayo mumewe Cizar anaitawala au anaihudumia.Pata Picha hiyo kuwa tuhuma kwa mke wa Cizar ni dhamana tosha ya kumuhukumu.Kwa tafsiri hiyo basi ni hakika Cizar mwenye hata fikra tu za kusikika dhidi ya uovu au matendo mabaya ya jamii yake inapaswa isiwepo.Japo kibinadamu wa leo jambo hili ni kama Picha ya kuigiza lakini kwa watu makini na wanaomjua MUNGU basi ili jambo linamaana kubwa sana.

Ndio Wanadamu tuliowengi nikiwemo mimi mwenyewe tunamapungufu yetu.Lakini nina hakika mapungufu haya ni vigezo vya wanadamu vile vile kujifunza kupitia mapungufu hayo kumludia MUUMBA na kujua mapungufu hayo yana madhara gani kwa jamii ya mtuhumiwa.Ndani ya jamii pamoja na kuwa kila mtu anamakosa yake lakini kuna makosa yanayomghalimu Mwanajamii kwa kiwango kikubwa sana kuliko makosa mengine.Mfano makosa ya uzinifu,wizi,uongo,kuua na mengineyo kama ushirikina nk.Makosa kama hayo yana kishindo [impact] kubwa kwa umma popote pale duniani.Leo hii mgombe Urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican kwenye uchaguzi unaokuja anapata matatizo sana kwa tuhuma za udhalilishaji wa wanawake kwenye miaka ya tisini [1990s].Yani matendo yake binafsi ya miaka ya hiyo leo hii yanamnyima dhamana ya kuwatumikia raia wenzie wa Taifa hilo kubwa duniani.

Tufike sehemu wale wanaoamini wanauwezo mkubwa wa kuchezesha turufu juu zaidi kuliko wenzao MUNGIU nae siku hizi anafungua MAONO na ufahamu kwa WANANCHI walio wengi huko mitaani.Hivyo kitendo cha kuwafanya HAWAJUI LOLOTE ni KUDHALAU UWEZO WA MUNGU.Na wakati mwigine MUNGU upenda kuleta AIBU KUBWA kwenye taasisi kubwa na nyeti za kiimani ili kufungua ukurasa mpya wa taasisi hizo kujiangalia na kuludi kwenye msingi wa heshima yake na kuendelea kumtumikia MUNGU na si watu.

Kwa walio bahatika kuangalia kipindi cha ITV cha MOVIE YA KINAIJERIA JUMAPILI ZILIYOPITA ZA TAREHE [ 30 Sep -6 Nov ] kulikua na movie kuhusu Mwanaume alieangaikia penzi la binti toka akiwa anasoma shule ya msingi.Mwanume huyu alighalimika kwa binti huyu na wazazi wake wakijua dhahili mchango wa Mwanaume huyu.Ikatokea kutafuta maisha Mwanaume huyu akapotea kijijini.alipoludi kuja kuchukua Mke yani binti aliyekuwa anamhudumia alistahajabu kukuta binti tayari ni mtawa [sister] kwenye dhehebu la Roman Catholic.Mwanaume huyu alipigania kumpata binti huyo toka katika nyumba ya Watawa [Convent].Hakika wa busara ya Kanisa Binti yule aliachishwa UTAWA japo si kwa mapenzi ya binti na familia yake,lakini kwa faida ya kanisa ilibidi kumsukuma nje [Kumtoa Pasipo hiari yake kwa kuwa binti hakutaka kwahisia zake za ndani kuacha utawa [usister] yeye na nyumayake familia yake].

Kanisa lilifanya hayo ili kuweka sawa kanuni na misingi na nidhamu ya dhamira ya WITO kuwa wito uwa HAUNA MBADALA.Daima mwenye wito anavutwa na hisia za ndani pasipo na shaka.Kuna wakati ASKOFU WAKEA NA MAMA MKUU [Kiongozi wa Watawa ndani ya Nyumba ya Watawa[Convent] ] waliomba idhini ya binti kuwa waite polisi waje kumchukua Mwanume yule alipokuja wakati fulani kwenye Nyumba ya Watawa kudai Mke wake.Binti yule alikataa kwa msingi kuwa atashughulikia swala la Mumewe huyo asie lasmi.Picha hiyo ya kukataa ndiyo iliondoa tafsiri ya wito wa binti kwa kuwa kwa usumbufu wa raia yule.Na hivyo kufikwa rasmi na uamuzi wa kanisa kumuondoa kwenye utumishi wa kanisa kwa dhamana ya UTAWA na hivyo kumpa uhuru rasmi wa yeye kuamua rasmi atumikie WITO wa KUOLEWA.Na kweli hatimae aliolewa na mumuwe huyo wa utotoni.

Hivyo ifike wakati kanisa lijue kuwa japo Lowasa anaweza kuwa binafsi ndani yake kuwa na ANAACHANA NA dhamila isiyo lasmi ya KUACHANA NA MATENDO YANAYOTAJWA KUMHUSISHA NA UFISADI NA MATENDO MENGINE MACHAFU KWENYE JAMII.KANISA KWA KUMKUMBATIA LOWASA BASI NI KUWATAWANYA MAELFU YA WAUMINI WAKE,BASI NI VEMA WAKALIJUA HILO KABLA YA AIBU HIYO KUWAFIKA JAPO DHAMILA YA LOWASA INAWEZA KUWA NUSU NI KAMA YA BINTI MTAJWA JUU KUOLEWA AU NUSU KUMTUMIKIWA MUNGU.

Kuna mengi uenda yatafumuka,ambayo kanisa wakingangania uenda yakaweka picha ya kanisa pabaya sana japo ni kwa dhamila njema ya Mwanampotevu lakini ambae hawana uhakika wa kumchunga kwa kuwa hayuko ndani ya imani ya mrengo wao.
 
Kiresua, sisi Wakatoliki, kwanza, tunajutia dhambi zetu, na kujuta huko, tunajutia moyoni, pili tunatubu kwa Mungu na sii kwa mwanadamu, na mwisho tunafanya malipizi kwa kutenda yaliyo mema.

As far as EL is concerned, ana dhambi gani ya kutubia wananchi?.. Kwa vile yeye sii malaika, atakuwa alishajuta, ameshatubu, hiki mnachokiona na kukisikia sasa kuhusu EL ni kufanya tuu malipizi. 2015 rais atatoka Kaskazini.

Pasco, asante kwa ufafanuzi, najizuiya kuingia kwenye mjadala huu lakini nashindwa, Pasco, ni kweli toba ni ya moyoni kana imani ilivyo ya moyoni! ila huwezi ukaniibia gari leo halafu ukajifanya husikii nikilalamika nimeibiwa gari, halafu ukaenda Kanisani kutubu... na baada ya kutubu siku inayofuata ukaanza kulitumia gari ulilyoniibia, je hiyo toba ni sawa???? eti Pasco ..... heee, si unaona eee!!

Au labda kwa makosa nimehisi kama jirani yangu umeniibia gari, kumbuka tulikuwa marafiki sana, nikakutuhumu umeniibia halafu ukaaa kimya na uhusiano wangu na wewe haujarudi kwa sababu nimehisi umeniibia..... jee, hutakuwa na hatia kwangu kwa kukaa kimya na mimi kuendelea kukutuhumu? huoni kwamba unasababisha nenendelee kuwa na hisia mbaya juu yako nikamkosea Mwokozi Yesu kwa ajili yako? huoni pia kuwa kwa kutotaka suluhu, kwa wewe tu kufungua kinywa chako na kusema nami tukarudia urafuki wetu, as far hakuna aliye mkamilifu chini ya mbingu tukaendea na urafiki na kuwa wamoja kama Mwokozi alivyo tuombea!!?

Pasco, be frank, alipaswa kutolea ufafanuzi siku nyingi eti atasema sikupewa nafasi ya kujitetea, wakati tangu ajiuzulu ni Miaka 4 sasa, au alitaka tumpe nafasi gani? na alisha sema atalitolea ufafanuzi muda muafaka.... mpaka atakapo tolea ufafanuzi na wanachi wakaridhika WaTZ bado hawana amani na mtu huyu!!!! na mm sina Amani naye hata kidogo.

Pasco hata mini ni wa Kaskazini na ni Mkatoliki pia, lakini kwa staili hii ni bora kutopata Raisi wa namna hii millele kutoka kaskazini! ( na huu Pasco ni ubaguzi kusema hivi) kwani kascazini kuna nini, kwani wengine sio waTZ? acha hizo mkuu!!!
 
kuanzia leo mimi namkubali lowasa mia kwa mia. hata urais na apewe.
 
Tusihukumu jamani, hukumu yetu haihesabiwi na wanadamu maana hawajui makosa yetu, yeye ametenda na tumeyasikia ila hatujui Mungu atamhukumuje. Tumwombee Mungu atubu dhambi zake kwani Mungu ni mwingi wa fadhila na rehema.
 
Hilo kanisa wanajua back ground ya EL au wanatumia mtu ni mtu alimladi wamechangisha sio
 
Lowassa ni Jambazi na Fisadi Papa si sawa kabisa kualikwa Kanisani kwenye shughuli muhimu kama hiyo. Huyu Fisadi alitakiwa awe jela saa hizi lakini bado yuko mtaani anakula kuku kwa mrija. Nyinyi wapambe wa Lowassa msitake kumtetea hapa, Viongozi wa hiyo dayosisi pia wamechemsha kumualika Fisadi na Jambazi aliekubuhu kwenye hiyo harambee.
 
Jamani kanisa limeingizwa kwenye siasa. nadhani ni weakness ya viongozi wachache wa jimbo la Mwanza ambao wamelainishwa na fedha.....ambazo Mheshimiwa anazo nyingi na bado anasubiri cut yake itakapolipwa Dowans
 
Maneno matupu tupu, so far Lowassa is doing great!
 
Mim ni mkatoriki lakin siungi mkono Lowasa kualikwa kwenye hiyo harambee! Hovyo kabisa hizi dini za siku hizi hakuna kitu,wanawaza hela tu!

Mkuu, umenishangaza sana. Unazungumzia dini, dhehebu au kanisa kama jengo? Kama ni jengo ulitegemea lingejengwaje kama si kwa michango ya watu, hususan waumini? Au unafikiri bado wapo wajomba kutoka Ulaya wa kuwaletea pesa za kujengea nyumba za ibada kama awali? Kuhusu Mhe. EL, mimi nami sioni tatizo, si swala letu kuhukumu utakaso wa mtu, hata Bw. Yesu alikula na wadhambi, japo simaanishi kwamba Mhe. ni mmojawapo.
 
..........tutabaki kumnyoshea kidole Lowassa (kumbuka ni kimoja vinne vinatuelekea wenyewe), kwamba ni fisadi , naam, ametubu/atatubu, atasamehewa, sisi tutabaki na uzinzi wetu, unafiki wetu, uzandiki wetu, upashikuna wetu, kutamani kwetu (hasa nyumba za majirani/kila anayepita mbele yetu), na yote yanayofananana na haya;tutaishia na kufa na dhambi zetu.
 
...........mwuulize Mwandosya yaliyomkuta kwa JK, alisema kama wewe, kwamba jamaa akipata urais atahama nchi mpaka amalize muda wake, mwuulize alihamia wapi? acheni kutung'ong'a
Lowassa akiwa Rais wa TZ nita-slimu na kwenda Somalia kuungana na masela wa al-Shabaab.
 
..........tutabaki kumnyoshea kidole Lowassa (kumbuka ni kimoja vinne vinatuelekea wenyewe), kwamba ni fisadi , naam, ametubu/atatubu, atasamehewa, sisi tutabaki na uzinzi wetu, unafiki wetu, uzandiki wetu, upashikuna wetu, kutamani kwetu (hasa nyumba za majirani/kila anayepita mbele yetu), na yote yanayofananana na haya;tutaishia na kufa na dhambi zetu.
Katubu? Amerudisha hela alizoiba kwa ufisadi wake? Toba katika imani ya kikristo kwa mtu aliyeiba lazima iendane na kurudisha mali ya wizi kwa mwenye mali. Bila hilo hakuna cha toba hapo. Je, karudisha mabilioni yetu watz?
 
Du hii nayo imetulia,Roman Catholic kwa umakini walio nao, hili la huyu jamaa du LITALETA UTATA KWENYE JAMII.Japo Edward yaweza kuwa katubu lakini kwa hali ya tafsiri ya UMMA [WATANZANIA] kwa yale waliyoyasikia kuhusu Edward kupitia vyombo halali vya habari vya Umma na binafsi na walio wengi hasa kwenye miji yetu mikuu na wilayani kutoa tafsiri ya hukumu dhidi yake basi,ni vigumu kwa mtu huyu kupata tiketi ya UMMA huo huo uliolishwa taarifa ama ya UKWELI ama YA UONGO dhidi ya Mtuhumiwa kumpa nafasi ya KUJITANABAISHA NA KUNDI AMBALO AMECHAFULIWA KWAO HIVYO KUMPA SIFA ZA KUTOSHA KUMTOA KWENYE KADA YA KUWA KIONGOZI WA SHUGHULI ZA UMMA ZIWE NI ZA KIROHO AU KIJAMII

Manake hii ni sawa na tafsiri ya Mwalimu Nyerere na liwaya za Mtukufu Cizar na Mkewe,Kwani kitendo cha Mke wa Mtukufu huyu kutuhumiwa kwa jambo ovu basi kinatoa dhamana ya kuto aminika kwa Mke wa Cizar kwa jamii ambayo mumewe Cizar anaitawala au anaihudumia.Pata Picha hiyo kuwa tuhuma kwa mke wa Cizar ni dhamana tosha ya kumuhukumu.Kwa tafsiri hiyo basi ni hakika Cizar mwenye hata fikra tu za kusikika dhidi ya uovu au matendo mabaya ya jamii yake inapaswa isiwepo.Japo kibinadamu wa leo jambo hili ni kama Picha ya kuigiza lakini kwa watu makini na wanaomjua MUNGU basi ili jambo linamaana kubwa sana.

Ndio Wanadamu tuliowengi nikiwemo mimi mwenyewe tunamapungufu yetu.Lakini nina hakika mapungufu haya ni vigezo vya wanadamu vile vile kujifunza kupitia mapungufu hayo kumludia MUUMBA na kujua mapungufu hayo yana madhara gani kwa jamii ya mtuhumiwa.Ndani ya jamii pamoja na kuwa kila mtu anamakosa yake lakini kuna makosa yanayomghalimu Mwanajamii kwa kiwango kikubwa sana kuliko makosa mengine.Mfano makosa ya uzinifu,wizi,uongo,kuua na mengineyo kama ushirikina nk.Makosa kama hayo yana kishindo [impact] kubwa kwa umma popote pale duniani.Leo hii mgombe Urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican kwenye uchaguzi unaokuja anapata matatizo sana kwa tuhuma za udhalilishaji wa wanawake kwenye miaka ya tisini [1990s].Yani matendo yake binafsi ya miaka ya hiyo leo hii yanamnyima dhamana ya kuwatumikia raia wenzie wa Taifa hilo kubwa duniani.

Tufike sehemu wale wanaoamini wanauwezo mkubwa wa kuchezesha turufu juu zaidi kuliko wenzao MUNGIU nae siku hizi anafungua MAONO na ufahamu kwa WANANCHI walio wengi huko mitaani.Hivyo kitendo cha kuwafanya HAWAJUI LOLOTE ni KUDHALAU UWEZO WA MUNGU.Na wakati mwigine MUNGU upenda kuleta AIBU KUBWA kwenye taasisi kubwa na nyeti za kiimani ili kufungua ukurasa mpya wa taasisi hizo kujiangalia na kuludi kwenye msingi wa heshima yake na kuendelea kumtumikia MUNGU na si watu.

Kwa walio bahatika kuangalia kipindi cha ITV cha MOVIE YA KINAIJERIA JUMAPILI ZILIYOPITA ZA TAREHE [ 30 Sep -6 Nov ] kulikua na movie kuhusu Mwanaume alieangaikia penzi la binti toka akiwa anasoma shule ya msingi.Mwanume huyu alighalimika kwa binti huyu na wazazi wake wakijua dhahili mchango wa Mwanaume huyu.Ikatokea kutafuta maisha Mwanaume huyu akapotea kijijini.alipoludi kuja kuchukua Mke yani binti aliyekuwa anamhudumia alistahajabu kukuta binti tayari ni mtawa [sister] kwenye dhehebu la Roman Catholic.Mwanaume huyu alipigania kumpata binti huyo toka katika nyumba ya Watawa [Convent].Hakika wa busara ya Kanisa Binti yule aliachishwa UTAWA japo si kwa mapenzi ya binti na familia yake,lakini kwa faida ya kanisa ilibidi kumsukuma nje [Kumtoa Pasipo hiari yake kwa kuwa binti hakutaka kwahisia zake za ndani kuacha utawa [usister] yeye na nyumayake familia yake].

Kanisa lilifanya hayo ili kuweka sawa kanuni na misingi na nidhamu ya dhamira ya WITO kuwa wito uwa HAUNA MBADALA.Daima mwenye wito anavutwa na hisia za ndani pasipo na shaka.Kuna wakati ASKOFU WAKEA NA MAMA MKUU [Kiongozi wa Watawa ndani ya Nyumba ya Watawa[Convent] ] waliomba idhini ya binti kuwa waite polisi waje kumchukua Mwanume yule alipokuja wakati fulani kwenye Nyumba ya Watawa kudai Mke wake.Binti yule alikataa kwa msingi kuwa atashughulikia swala la Mumewe huyo asie lasmi.Picha hiyo ya kukataa ndiyo iliondoa tafsiri ya wito wa binti kwa kuwa kwa usumbufu wa raia yule.Na hivyo kufikwa rasmi na uamuzi wa kanisa kumuondoa kwenye utumishi wa kanisa kwa dhamana ya UTAWA na hivyo kumpa uhuru rasmi wa yeye kuamua rasmi atumikie WITO wa KUOLEWA.Na kweli hatimae aliolewa na mumuwe huyo wa utotoni.

Hivyo ifike wakati kanisa lijue kuwa japo Lowasa anaweza kuwa binafsi ndani yake kuwa na ANAACHANA NA dhamila isiyo lasmi ya KUACHANA NA MATENDO YANAYOTAJWA KUMHUSISHA NA UFISADI NA MATENDO MENGINE MACHAFU KWENYE JAMII.KANISA KWA KUMKUMBATIA LOWASA BASI NI KUWATAWANYA MAELFU YA WAUMINI WAKE,BASI NI VEMA WAKALIJUA HILO KABLA YA AIBU HIYO KUWAFIKA JAPO DHAMILA YA LOWASA INAWEZA KUWA NUSU NI KAMA YA BINTI MTAJWA JUU KUOLEWA AU NUSU KUMTUMIKIWA MUNGU.

Kuna mengi uenda yatafumuka,ambayo kanisa wakingangania uenda yakaweka picha ya kanisa pabaya sana japo ni kwa dhamila njema ya Mwanampotevu lakini ambae hawana uhakika wa kumchunga kwa kuwa hayuko ndani ya imani ya mrengo wao.

Badala kujenga hoja kwa maandiko unajenga kwa movie za kinaijeria!!!
 
Jitahidini kuwaelewa wakatoliki na falsafa za dini hasa wakristo juu ya wadhambi,hata yesu aliwahi kusema ya kwamba hakuja kwa watu wema bali wadhambi,kumbukeni falsafa ya dini na ya siasa zina tofauti kubwa.dini inawataka wadhambi ili iwatoe huko kwenye dhambi lakini ukweli wa siasa ni kuwakana wadhambi japo mambo ni tofauti kidogo kwa chama cha magamba CCM.Japo sina hakika na lengo hasa la kuitwa kwa Lowasa huko MWZ tukiachilia mbali kumchuna fedha ambazo zimetokana na kuwaibia wananchi wa TZ, sijapata picha halisi na wala mantiki ya kumwalika Lowasa,binafi sina haja hat ya shilingi kumi yake kutokana na yale aliyoyafanya ndani ya TZ

Unatakiwa kuielewa vizuri hiyo falsafa. Lengo ni kuwafanya wadhambi watubu na kuacha dhambi zao kabisa na siyo kuungana nao ili kutumia walivyochuma kwa dhambi. Hiyo ni kuendeleza na kuikuza dhambi mkuu.
 
Tanzania tuna tatizo kubwa kuliko mnavyodhani. Je leo Lowasa akitubu hana msamaha? Mbona Mkapa ambaye ni Mkatoliki kabisa akialikwa mahali hamsemi, hivi hapa tulipo sasa hivi kati ya Mkapa na Lowasa nani katufikisha hapa tulipo? kama ni hivyo basi ni vema kila kiongozi wa CCM alaaniwe mahali popote alipo kwani ndiyo wametufikisha hapa. Ni vema dhambi za Lowasa tunazifahamu, je Pinda, hivi huko anakotupeleka kwenda kuuza nchi kwa kisingizio cha kilimo kwanza, ardhi anayosimamia wauziwe wamarekani tutapona? Huko mbele ya safari tutakuja gundua kuwa Pinda atakuwa ni mbaya zaidi kuliko Lowasa.
Mmesahau Kilaini enzi hizo alivyosema Kikwete ni chagua la Mungu? si alikuwa jirani na Pengo, mi sishangai Lowasa kualikwa huko kwani mlitaka wamualike nani? Ni heri aalikwe Lowasa toka CCM, ndiyo mjue CCM inavyotumia makanisa na misikiti ni suala kuchanga kete vizuri
 
Katubu? Amerudisha hela alizoiba kwa ufisadi wake? Toba katika imani ya kikristo kwa mtu aliyeiba lazima iendane na kurudisha mali ya wizi kwa mwenye mali. Bila hilo hakuna cha toba hapo. Je, karudisha mabilioni yetu watz?

Nisaidie ndugu yangu! Ni shilingi ngapi Lowasa katuibia?
 
Pasco, asante kwa ufafanuzi, najizuiya kuingia kwenye mjadala huu lakini nashindwa, Pasco, ni kweli toba ni ya moyoni kana imani ilivyo ya moyoni! ila huwezi ukaniibia gari leo halafu ukajifanya husikii nikilalamika nimeibiwa gari, halafu ukaenda Kanisani kutubu... na baada ya kutubu siku inayofuata ukaanza kulitumia gari ulilyoniibia, je hiyo toba ni sawa???? eti Pasco ..... heee, si unaona eee!!

Au labda kwa makosa nimehisi kama jirani yangu umeniibia gari, kumbuka tulikuwa marafiki sana, nikakutuhumu umeniibia halafu ukaaa kimya na uhusiano wangu na wewe haujarudi kwa sababu nimehisi umeniibia..... jee, hutakuwa na hatia kwangu kwa kukaa kimya na mimi kuendelea kukutuhumu? huoni kwamba unasababisha nenendelee kuwa na hisia mbaya juu yako nikamkosea Mwokozi Yesu kwa ajili yako? huoni pia kuwa kwa kutotaka suluhu, kwa wewe tu kufungua kinywa chako na kusema nami tukarudia urafuki wetu, as far hakuna aliye mkamilifu chini ya mbingu tukaendea na urafiki na kuwa wamoja kama Mwokozi alivyo tuombea!!?

Pasco, be frank, alipaswa kutolea ufafanuzi siku nyingi eti atasema sikupewa nafasi ya kujitetea, wakati tangu ajiuzulu ni Miaka 4 sasa, au alitaka tumpe nafasi gani? na alisha sema atalitolea ufafanuzi muda muafaka.... mpaka atakapo tolea ufafanuzi na wanachi wakaridhika WaTZ bado hawana amani na mtu huyu!!!! na mm sina Amani naye hata kidogo.

Pasco hata mini ni wa Kaskazini na ni Mkatoliki pia, lakini kwa staili hii ni bora kutopata Raisi wa namna hii millele kutoka kaskazini! ( na huu Pasco ni ubaguzi kusema hivi) kwani kascazini kuna nini, kwani wengine sio waTZ? acha hizo mkuu!!!
Hivi Lowasa kaiba nn jamani?
 
Back
Top Bottom