Lowassa na siasa za makanisani?

Lowassa na siasa za makanisani?

waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya richmond amecheka tsh.milioni 10 jijini dar kuchangia kituo cha radio upendo fm.

Nini tafsiri yake lowasa kutoa kiwango cha mil.10 kila anapo ombwa kuchangia? Kwa nini hazizidi wala kupungua?

tafsiri yake ni kwamba anazo pesa..
 
IMG_7032.jpg

Waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya Richmond amecheka Tsh.Milioni 10 jijini Dar kuchangia kituo cha Radio Upendo FM.
Nini Tafsiri yake Lowasa kutoa kiwango cha Mil.10 kila anapo ombwa kuchangia? Kwa nini hazizidi wala kupungua?

Hapo kwenye red labda ndiyo masharti aliyopewa na yule mganga wake wa Kinigeria.
 
Kama kawaida yake, mchangishaji wa makanisa EL leo alikuwa Arusha ktk harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Elerai. kaniacha hoi alipoongea km m/kiti wa kamati ya bunge.
 
Anafahamu siri ya utoaji.
Atoaye kwa wingi hupokea kwa wingi.
Atoaye haba naye hupolea haba.
Hilo la kuongea kama m/kiti it just happens kama kila mahali anapewa uenyekiti ubongo nao una adopt hivyo hivyo
 
Safi lowasa mtumikie mungu,wala usichoke
 
Lowasa hasafishiki hata aende mbinguni na kurudi. Ahangaike tu na hayo makanisa. Labda anategemea watasema yeye ni "chaguo la Mungu" 2015.
 
Mi sijaelewa,mantiki ya thread hii ni nini? JESUS-nyumba ya bwana imegeuzwa kuwa pango la walanguzi wa kisiasa.
 
"Nilikuja kutafuta waliopotea, aliye mzima hahitaji daktari ila aliye mgonjwa" Maandiko
 
Jamani, Lowassa si afungue kanisa lake awe anagawa hela kwa waumini kuliko kila siku kwenda kushinda kwenye makanisa ya wenzake?
Kama kawaida yake, mchangishaji wa makanisa EL leo alikuwa Arusha ktk harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Elerai. kaniacha hoi alipoongea km m/kiti wa kamati ya bunge.
 
Siasa zingekuwa zinafikisha mtu mbinguni huyu jamaa nahisi angekuwa wa kwanza kwenda. Lakini sasa siasa ni sawa na upepo tu, hausaidii mtu kufika katika makao ya milele.
.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Sioni tatizo lolote kwa EL kuongoza harambee huko makanisani. Hizi kampeni za kumpinga nadhani zinaongozwa na wanasiasa waoga ambao wanaogopa nguvu na ushawishi wa EL ktk jamii.
 
Lowasa hasafishiki hata aende mbinguni na kurudi. Ahangaike tu na hayo makanisa. Labda anategemea watasema yeye ni "chaguo la Mungu" 2015.

mkuu asafishike kivipi? Kwani ni mchafu? Hebu weka hapa uchafu wake...usifuate mkumbo! God bless u El.
 
mkuu asafishike kivipi? Kwani ni mchafu? Hebu weka hapa uchafu wake...usifuate mkumbo! God bless u El.

Nenda kama muulize Mzee slaa kwanini kamuweka lowasa katika ile list of shame..??
 
Mi kaniacha hoi alipoipongeza serikali kwa kutuliza vurugu zenj kwa niaba ya kamati yake ya bunge, Kanisani?
 
Anafahamu siri ya utoaji.
Atoaye kwa wingi hupokea kwa wingi.
Atoaye haba naye hupolea haba.
Hilo la kuongea kama m/kiti it just happens kama kila mahali anapewa uenyekiti ubongo nao una adopt hivyo hivyo
atoaye kwa wingi pesa za wajenzi huru na ziada au kwa Moyo acha ujinga wewe.Anatoa zake au za watz alizokwisha fyonza sana
 
Back
Top Bottom