Lowassa na siasa za makanisani?

Lowassa na siasa za makanisani?

Yuko mtu hapa anayeweza kusema mbele ya macho ya Mungu yeye ni bora kuliko Lowasa? Hakuna! Kidini msimamo ni huu: usihukumu ili usije kuhukumiwa!

Kuna anayetaka kusema hapa Lowasa anyimwe kushiriki katika shughuli za kiroho kama kuchangia ujenzi wa kanisa? Kama anaruhusiwa kushiriki na kama Parokia imeona ana uwezo mkubwa wa kuwasaidia, kwanini wasimwalike?

Ukitaka unaweza kumtenga Lowasa kisiasa, ila ukitaka kumtenga kiroho unafanya kosa kubwa. Unakiuka amri ya Mungu inayosema usihukumu (kiroho).
 
Harambee si sehemu ya misingi ya imani ya kikatoliki, kwa hiyo kilichofanywa huko mwanza ni njaa za watu wachache wanaotumia kanisa kujifaidisha.

Kukariri ni kubaya,acheni kuchanganya dini na siasa!tena ni vyema ukaifuta kauli yako kwani Roma haija anza harambee jana wala juzi,halafu ni vyema 2kawa wawazi kwamba Roma haina njaa,Roma ni moja kati ya makanisa yanayongozwa na wasomi wenye uelewa mkubwa,pia usishangae licha ya wewe kujitakasa kwamba ni msafi mbele za mungu kuliko lowasa kumbe ukawa mwenye dhambi tena inayonuka kuliko lowasa,tafakari juu ya wizi,masengenyo,unafiki,uzandiki,uzinzi kwako.acha kuzungumza upupu!
 
huyu masota si ndio aligombea ubunge ilemela akabwagwa kura za maoni na dialo?nadhan atakuwa kundi la lowasa na ni mpango wa urais huo.
 
Kieleweke;2802782]"Mimi ni mkatoliki na ninajua kuwa Lowasa hajawahi kualikwa kwenye dhifa za namna hii kwenye majimbo mengi. Niambieni ni lini mliwahi kusikia kuwa Lowasa amealikwa kwenye kuongoza dhifa ya Kanisa Katoliki kama ambavyo ameitwa huko Mwanza. D'Salaam ndiyo makazi ya Lowasa. Mke wake Regina si tu ni mkatoliki mwenzetu bali ni mshiriki mkuu wa mambo ya Kanisa na hadi ametunga kitabu kuhusu ziara yao kule Israel. Lakini jiulizeni kwamba ni lini Edward Lowasa binafsi alipewa nafasi jimboni D'Salaam kama anayopewa huko Mwanza?
Kanisa Katoliki limekuwa ni linaongozakatika kuupinga ufisadi. Askofu wa Jude Thaddaeus wa Dodoma alitoa pongezi kwa wanasiasa walioufichua ufisadi. Askofu huyo alitoa pongezi hizo siku ya kumsimika Askofu Msonganzila kama askofu mpya wa Musoma. Kumbuka ilikuwa ni miezi mitatu baada ya Dr. Slaa kutamka list ya mafisadi na vilevile mwezi mmoja kabla Lowasa hajajiuzulu mwenyewe kwa kushindwa kujitete bungeni kwa tuhuma za ufisadi wa RICHMOND zilizotafitiwa na timu ya Dr. Mwakyembe.
Wakati askofu Jude Thadaesu anatoa pongezi kwa kina Slaa alikuwa askofu wa Dodoma lakini alisoma pongezi zile kama rais wa Baraza la Maaskofu wa Tanzania. Leo, askofu Jude Thaddeus hayuko Dodoma bali sasa yuko Mwanza! Bado ni rasi wa Baraza la Maaskofu!
Halafu hukohuko Mwanza ndiko Lowasa ameanza kuonyesha anakubalika ndani ya Kanisa Katoliki!
Hapa tunahitaji umakini wa hali ya juu. Kwanza nina wasiwasi kama askofu amejulishwa mapema kuhusu uchangiaji huo. Wenye kujua namba za Jimbo Kuu la Mwanza bado siku ya kesho inaweza kutumika kuulizia ofisini kwake kama kweli anajua.
Lowasa hajathibitika kuwa ni fisadi. Lakini hajawahi kukanusha kutohusika na RICHMOND inayotutesa hadi kesho. Kwa nini aliitupilia mbali nafasi ya kujitetea bungeni ambapo ilikuwa ni nafasi ya nzuri ya kujisafisha mbele ya umma kuliko kutumia njia zingine.
Kanisa Katoliki limepinga sana ufisadi. Kama mafisadi hawajaakmatwa na bado kuna wale wanatuhumiwa kwa ukaribu, leo Kanisa linaenda kujiweka karibu nao. Ukweli ni kwamba Kanisa Katoliki linajiweka katika mahala pagumu kwenye vita hii y ufisadi. Lisijilaumu pale litakapoanza kuulizwa "mbona watuhumiwa mnawaalika wanapowachangia hizo pesa zao".
Ninalifahamu hili kanisa langu kuhusu mambo ya ushoga (homosexuality). Ni moja ya maknisa machache kama si pekee ambalo linapinga kwa ukali suala la ushoga. Ninalipongeza liendelee hivyo. Lakini kama linapinga ushoga na hajakamatwa mtuhumiwa wa ushoga basi ina maana kuwa kuwa mtuhumiwa wa ushoga hakumfany mtuhumiwa asikubaliwa na kanisa kuongoza harambee.
Hivyo, Tanzania kuna watuhumiwa wengi tu wa ushoga. Baadhi yao ni matajiri. Maadam hawajatiwa hatiani basi tutarajie nao siku moja tusikie wakiitwa kwenye Parokia mojawapo ili kuongoza harambee! Tusilalamike ikifika huko.
Haijapita miaka miwili wenzetu nadhani walutheri walikataa hela ya Rostam Azizi. Naikumbuka issue ile ambapo ilibidi viongozi wa Kanisa waingilie kati na kusema Rostam alialikwa na kikundi cha kwaya na si viongozi wa Kanisa. Kama sikosei ilibidi kile kikundi kirudishe hela zile kwa Rostam na kuomba samahanani.
Je, haya si mazingira yaleyale kama ya case ya Rostam na walutheri wale. Nimelisoma gazeti na mleta mada hajakosea hata nukta. Lakini kama mmesoma vizuri hakuna palipoandikwa kwamba Paroko amemualika Lowasa. Kwa mazingira yaleyale yaaliyopita kwa Rostam, basi inawezekana huyu mwenyekiti wa Parokia ambaye ni mlei ameandaa jambo zima na labda Paroko au padri wa pale ameshirikishwa mwishoni sana.
Kama Paroko hana taarfia basi hata askofu Jude Thadeus wa jimbo hilo inawezekana habari hii ndiyo inamtaarifu.
Habari inaeleza kuwa Lowasa anaushawishi ndicho kigezo cha kumualika hapo parokiani. Hivi lina ukweli hili? Kama ni hivyo mbona hamjasikia Kanisa Katoliki likimualika Reginald Mengi. Ukweli nikwamba kama ninavyoshangaa Lowasa kualikwa nitashangaa kusikia Kanisa Katoliki kumualika Mengi tangu siku Mengi alipotamka kwamba viongozi wa dini wahimize uvaaji wa Condom".

Umeeleza mambo mengi ambapo mengi ya hayo unaonekana haujafanya analysis bali umeungaunga habari mbalimbali za magazetini. Kikubwa,usichanganye misimamo na imani za kidini na siasa/sheria. Jambazi anaweza kutubu kwa dhati kwa Mungu na akasamehewa dhambi zake bila masharti yeyote,na Mungu huwa anamwambia tu enenda zako,wala usitende dhambi tena. Lakini jambazi huyohuyo akikubali dhambi zake in court of law huwa haachwi. Atafungwa. Hiyo ni moja ya tofauti kati ya mambo ya imani na mambo ya siasa/sheria.Elewa mpaka sasa hakuna shtaka lelote aliloshtakiwa Lowasa. Ni tuhuma tu za magazeti na vyombo vingine vya habari. Ukichunguza wanaomtuhumu,wamesimamia kwenye jambo moja tu! Richmond!. Nalo halim link direct. Yesu alisema"Asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga mawe mtu huyu". Kisha akamwambia,"enenda zako, imani yako imekuponya".Hata wewe mtoa mada una madhambi yako mengi tu. Je wakutenge hapo kanisani kwako?!. Mambo ya ki sheria yafanywe kisheria na mambo ya ki imani yaende ki imani.
 
Sidhani kama kuna ukweli ktk hili. na kama likitokea kuwa kweli nadhani kanisa litakuwa limekwisha kabisa. Yaani sipati picha na sina uhakika kama hizi taarifa zimemfikia Pengo na maaskofu wengine wa kanisa langu hili zuri, mweeeeeee! Lowassa kuchangia kanisa katoliki,oooopssssssss! an abomination of the century, pheeeeeeeeeeeeeeeew! Tusubiri tuone kama ni kweli!

Mimi ni Mkatoliki wa kawaida na si msemaji wa Kanisa lakini ninavyofahamu ujenzi wa kanisa lolote uko chini ya Parokia mahalia na Kamati za Ujenzi zinazoundwa na Baraza la Walei ndizo hupendekeza mbinu mbalimbali za kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi ikiwa ni pamoja na harambee kama hiyo.
Maaskofu wala Baraza la Maaskofu (Kwa maana TEC) hawahusiki moja kwa moja na ujenzi wa kanisa kwa zaidi ya kutoa sera na maelekezo inapobidi na nina uhakika hata Askofu wa Jimbo hajafahamu juu ya mwaliko wa Lowassa ingawa siwezi kumsemea kama ataafiki au la.
Kulilaumu Kanisa zima ni kutolitendea haki. Ninachoelewa Kanisa Katoliki kama moja ya asasi makini sana kwa kutafakari na kuchukua hatua si rahisi kuingizwa kwenye mtego wa wazi kama huu. Ni vigumu kutoa maoni zaidi maana hata hiyo habari yenyewe tunaambiwa ni ya magazeti kwa maana kwamba si habari rasmi.
Mimi naamini msimamo wa kanisa juu ya kupinga ufisadi, ugandamizaji wa haki za wanyonge, ushoga ikiwa na utoaji mimba hauyumbi wala hautikisiki.
Tofauti kabisa na madhehebu karibu yote misimamo na sera za Kanisa Katoliki huanzia na kuratibiwa na chanzo kimoja, ndicho kiti cha Mtakatifu Petro yaani Baba Mtakatifu na si rahisi kwa kikundi au hata Askofu kufanya kinyume cha maelekezo ya Uongozi mkuu na kuachwa hivihivi. Maaskofu wanalielewa hilo vema zaidi na msimamo wao ni wazi. Narudia tena kusema kamwe, popote duniani kanisa haliwezi kushirikiana na wezi, vibaka, mashoga, watoaji mimba na wahalifu wengine isipokuwa pale wanapotafuta toba na kumrudia Mungu.
Kristu -Tumaini letu.
 
mimi ni mkristo nakubaliana na mkakati wa kupambana na ushenzi wa udini wa kuwapendelea waislamu hata pale wasipoweza kitu, sijali tunatumia mbinu gani kupambana na ushenzi wa JK na Ramadhani Dau. Je mnafahamu kwamba pale NHC baada ya mchakato wa kumpata mwanasheria kufika mwisho na mtu kuajiriwa order ikatoka ikulu kazi hiyo apewe mke wa Ridhwani na amepewa.Pamoja na kujikomba kwake mchechu amelalamika huku akijua kwamba yeye mwenyewe kaingia kwa style hiyo, eti Shirika la Umma lenye kutumia V8VX za mamilioni bila kuzalisha senti tano kwa kukusanya madeni yaliyopita hii ni epa nyingine ni vile tu watanzania wapumbavu tunatabia ya kushabikia vitu na kama ananilea nkya alivyosema, kuishia na postmortem
 
Yuko mtu hapa anayeweza kusema mbele ya macho ya Mungu yeye ni bora kuliko Lowasa? Hakuna! Kidini msimamo ni huu: usihukumu ili usije kuhukumiwa!

Kuna anayetaka kusema hapa Lowasa anyimwe kushiriki katika shughuli za kiroho kama kuchangia ujenzi wa kanisa? Kama anaruhusiwa kushiriki na kama Parokia imeona ana uwezo mkubwa wa kuwasaidia, kwanini wasimwalike?

Ukitaka unaweza kumtenga Lowasa kisiasa, ila ukitaka kumtenga kiroho unafanya kosa kubwa. Unakiuka amri ya Mungu inayosema usihukumu (kiroho).
Mkuu,
Lowasa amekuwa anaalikwa kwenye harambee hizi kwa kuwa yeye mwenyewe amekuwa akichangia kiasi kikubwa kwenye harambee hizi achilia mbali michango ya rafiki zake. Kinachowauma wengi ni ukweli kuwa huyu bwana anachanga fedha ambazo amewaibia waTz, labda kama unataka tuamini kuwa Lowasa si mwizi.
 
Wandugu, haya mambo yana hekima zake. Hivi jamani ni kweli hatusali na majambazi, wauaji, wazinzi, wachawi na wengineo wenye matendo machafu pengine kuliko lowasa ambae dhambi yake ya nje tunaijua..? Je huwa tunawafukuza au huwa tunazikataa sadaka zao..? By the way mnataka hzo pesa zikamnufaishe nani.., shetani? Hata hivo inategemea unalichukuliaje hili suala, kama mrengo wako ni wa kisiasa hasa siasa zile zilizomshinda RA obvious hutakua na mtazamo chanus juu ya mh lowaasa, kama unalitazama hili kwa mrengo wa dini then thts good and here we go, lowasa ni mwenye dhambi sawa kana kwamba ss hatuna.., mnataka akaungame wapi hzo dhambi wandugu? Kwamba kwa vle tayari ana dhambi kwa hio atengwe afe na dhambi zake wakati " hakuja kwa ajili ya wasafi bali kwa wenye dhambi" ni hayo tu na mtazamo wangu. You can argue in otherway also.
 
Acheni roho mbaya.mnataka kumtenga el na siasa hata na imani?washenzi nyie.nani kawaambia kuwa hakutubu dhambi zake.!kama alitubu mbele ya mungu mnataka awajuze?el songa mbele achana na maneno uchwara ya wacheza bao.
 
Mimi ni mkatoliki na ninajua kuwa Lowasa hajawahi kualikwa kwenye dhifa za namna hii kwenye majimbo mengi. Niambieni ni lini mliwahi kusikia kuwa Lowasa amealikwa kwenye kuongoza dhifa ya Kanisa Katoliki kama ambavyo ameitwa huko Mwanza. D'Salaam ndiyo makazi ya Lowasa. Mke wake Regina si tu ni mkatoliki mwenzetu bali ni mshiriki mkuu wa mambo ya Kanisa na hadi ametunga kitabu kuhusu ziara yao kule Israel. Lakini jiulizeni kwamba ni lini Edward Lowasa binafsi alipewa nafasi jimboni D'Salaam kama anayopewa huko Mwanza?
Mkuu,
Alikuwa parokia ya Rwamlimi jimbo la Musoma jumapili iliyopita kuongoza harambee kama hii. Nashindwa kujua kama mialiko hii ina baraka za maaskofu wa majimbo husika.
 
Unaweza ukaliona katika mtazamo huo, ila mimi nadhani kwa jinsi huyu Bw. Lowassa alivyotokatoka ktk utumishi wa Umma, Mwenyekiti wa Parokia hawezi kusema huyu Bw. Lowassa ana mahusiano mazuri na jamii au jamii inamkubali, jamii gani anayoizungumzia huyu Mwenyekiti???Jamii hii ni ya sisi Watanzania tulioingizwa mjini na Lowassa na Kundi lake la Wahuni?? Mi nadhani aseme yeye kwa ajili ya tamaa zake za hela ameamua kumualika huyo bwana kwakuwa anafahamiana kwa ukaribu na mafisadi hivyo mafisadi wengi watakuja kutoa fedha haramu hapo kanisani. Under normal circumstance Padri anadhani wachangiaji watatoka wapi kama wana nyakato wameshindwa???Mwenyekiti kapima kaona wananyakato hawana hela hivyo kaamua kusaka hata Fedha haramu ili mradi kanisa lijengwe.

Kanisa litakufa kwa sababu ya tamaa zake za pesa. sasa hivi kama huna pesa huwezi kuwa kiongozi wa kanisa na wala hutothaminiwa. Wenzetu ulaya kanisani hawaendi kwa wingi kama Africa, nadhan walishaona jinsi kanisa linavyopotoka. Kanisa endeleeni kutamani fedha haramu halafu muone mtapoishia. Mungu pia alikataa Sadaka ya Cain kwani alikuwa mchakachuaji. Au katika hili mlilolifanya, Biblia zenu hazina huo mstari wa Cain na Abel???? Kama kanisa mnatamaa hivi, mtashindwa kukemea wafanya maovu.Na ndivyo hali ilivyo hivi sasa. Au mwenyekiti na wewe na Fisadi??

Yupo wapi Mtikila. alikuwa anabweka sana na ufisadi, Rostam akatoa ushahid kuwa Mtikila alimfwata akamkopa hela. Hadi leo Mtikila analiapproach suala la ufisadi kwa aibu sana. Kanisa acheni njaa na tamaa za kipumbavu.

mtoto akikunyea mkono utaukata?na kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi.bravo lowasa endelea na juhidi zako. pale magogoni lazima ukae
 
Mimi ni mkatoliki na ninajua kuwa Lowasa hajawahi kualikwa kwenye dhifa za namna hii kwenye majimbo mengi. Niambieni ni lini mliwahi kusikia kuwa Lowasa amealikwa kwenye kuongoza dhifa ya Kanisa Katoliki kama ambavyo ameitwa huko Mwanza. D'Salaam ndiyo makazi ya Lowasa. Mke wake Regina si tu ni mkatoliki mwenzetu bali ni mshiriki mkuu wa mambo ya Kanisa na hadi ametunga kitabu kuhusu ziara yao kule Israel. Lakini jiulizeni kwamba ni lini Edward Lowasa binafsi alipewa nafasi jimboni D'Salaam kama anayopewa huko Mwanza?

Kanisa Katoliki limekuwa ni linaongozakatika kuupinga ufisadi. Askofu wa Jude Thaddaeus wa Dodoma alitoa pongezi kwa wanasiasa walioufichua ufisadi. Askofu huyo alitoa pongezi hizo siku ya kumsimika Askofu Msonganzila kama askofu mpya wa Musoma. Kumbuka ilikuwa ni miezi mitatu baada ya Dr. Slaa kutamka list ya mafisadi na vilevile mwezi mmoja kabla Lowasa hajajiuzulu mwenyewe kwa kushindwa kujitete bungeni kwa tuhuma za ufisadi wa RICHMOND zilizotafitiwa na timu ya Dr. Mwakyembe.

Wakati askofu Jude Thadaesu anatoa pongezi kwa kina Slaa alikuwa askofu wa Dodoma lakini alisoma pongezi zile kama rais wa Baraza la Maaskofu wa Tanzania. Leo, askofu Jude Thaddeus hayuko Dodoma bali sasa yuko Mwanza! Bado ni rasi wa Baraza la Maaskofu!
Halafu hukohuko Mwanza ndiko Lowasa ameanza kuonyesha anakubalika ndani ya Kanisa Katoliki!

Hapa tunahitaji umakini wa hali ya juu. Kwanza nina wasiwasi kama askofu amejulishwa mapema kuhusu uchangiaji huo. Wenye kujua namba za Jimbo Kuu la Mwanza bado siku ya kesho inaweza kutumika kuulizia ofisini kwake kama kweli anajua.

Lowasa hajathibitika kuwa ni fisadi. Lakini hajawahi kukanusha kutohusika na RICHMOND inayotutesa hadi kesho. Kwa nini aliitupilia mbali nafasi ya kujitetea bungeni ambapo ilikuwa ni nafasi ya nzuri ya kujisafisha mbele ya umma kuliko kutumia njia zingine.

Kanisa Katoliki limepinga sana ufisadi. Kama mafisadi hawajaakmatwa na bado kuna wale wanatuhumiwa kwa ukaribu, leo Kanisa linaenda kujiweka karibu nao. Ukweli ni kwamba Kanisa Katoliki linajiweka katika mahala pagumu kwenye vita hii y ufisadi. Lisijilaumu pale litakapoanza kuulizwa "mbona watuhumiwa mnawaalika wanapowachangia hizo pesa zao".

Ninalifahamu hili kanisa langu kuhusu mambo ya ushoga (homosexuality). Ni moja ya maknisa machache kama si pekee ambalo linapinga kwa ukali suala la ushoga. Ninalipongeza liendelee hivyo. Lakini kama linapinga ushoga na hajakamatwa mtuhumiwa wa ushoga basi ina maana kuwa kuwa mtuhumiwa wa ushoga hakumfany mtuhumiwa asikubaliwa na kanisa kuongoza harambee.

Hivyo, Tanzania kuna watuhumiwa wengi tu wa ushoga. Baadhi yao ni matajiri. Maadam hawajatiwa hatiani basi tutarajie nao siku moja tusikie wakiitwa kwenye Parokia mojawapo ili kuongoza harambee! Tusilalamike ikifika huko.

Kanisa lingejifunza kupitia kwenye scandal ya Freemasons. Kitendo cha jamaa wa freemasons kuwa karibu na viongozi wa kanisa katoliki kunalitesa na hadi kuna watu wengi tu wtanaamini kuna uhusiano mkubwa wa Freemasons na Ukatoliki.

Haijapita miaka miwili wenzetu nadhani walutheri walikataa hela ya Rostam Azizi. Naikumbuka issue ile ambapo ilibidi viongozi wa Kanisa waingilie kati na kusema Rostam alialikwa na kikundi cha kwaya na si viongozi wa Kanisa. Kama sikosei ilibidi kile kikundi kirudishe hela zile kwa Rostam na kuomba samahanani.

Je, haya si mazingira yaleyale kama ya case ya Rostam na walutheri wale. Nimelisoma gazeti na mleta mada hajakosea hata nukta. Lakini kama mmesoma vizuri hakuna palipoandikwa kwamba Paroko amemualika Lowasa. Kwa mazingira yaleyale yaaliyopita kwa Rostam, basi inawezekana huyu mwenyekiti wa Parokia ambaye ni mlei ameandaa jambo zima na labda Paroko au padri wa pale ameshirikishwa mwishoni sana.

Kama Paroko hana taarfia basi hata askofu Jude Thadeus wa jimbo hilo inawezekana habari hii ndiyo inamtaarifu.

Habari inaeleza kuwa Lowasa anaushawishi ndicho kigezo cha kumualika hapo parokiani. Hivi lina ukweli hili? Kama ni hivyo mbona hamjasikia Kanisa Katoliki likimualika Reginald Mengi. Ukweli nikwamba kama ninavyoshangaa Lowasa kualikwa nitashangaa kusikia Kanisa Katoliki kumualika Mengi tangu siku Mengi alipotamka kwamba viongozi wa dini wahimize uvaaji wa Condom.

Hayo ndiyo yangu.

wel said mkuu, na hi ndo shida ya kanisa kuangalia zaid material things badala ya spiritual na moral, mwenyekiti wa parokia au kamati za ujenzi anachaguliwa kwa hela yake na sio upendo na imani aliyonayo kwa Mwokozi. Hapa linapendwa pochi! Na hili pia ni gamba. Unaweza kuta paroko anashanga unaposema Yesu anaponya, eti na yeye haamini kwa sabab kuvuta muujiza kunategemea na imani uliyo nayo na si uprofesa wako wa elimu ya dini. Sishangai mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kanisa akijisogeza kwa ELo, wanataka kuvuta hela yake. Na hi haikubaliki. Hata kama watu wanacema ELo ametubu wakati hajawahi kutamka maneno either kutoa ufafanuzi wa tuhuma dhidi yake, au kuwaomba msamaha waTZ. Na hi toba n ya Kichina.
 
mtoto akikunyea mkono utaukata?na kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi.bravo lowasa endelea na juhidi zako. pale magogoni lazima ukae

Lowassa akiwa Rais wa TZ nita-slimu na kwenda Somalia kuungana na masela wa al-Shabaab.
 
Hekalu langu limekuwa pango la wanyang'anyi...mie ni muumini wa katoliki ila kwa hili mauti yataliandama kanisa hili,tunajenga ama tunabomoa?
ROMAN CATHOLIC is that beast revealed in Revelation. Fuatilieni mjue ukweli ili uwaweke huru.
Hakuna cha ajabu wao kumpigia magoti huyu Ngoyai
 
Hii habari ya Lowassa na ufisadi wa RICHMOND mie siwezi kumtuhumu Lowassa moja kwa moja,manake Makyembe alitoa ripoti yake ndefu tu bungeni tukaisikia na kuielewa vizuri lakini hapo ili haki na demokrasia ipatikane alitakiwa na Lowassa apewe nafasi ya kujitetea na yeye alete ripoti yake ndefu tuu hapo ndio tupime tuweze kumhukumu kama fisadi au laa lakini haya mambo ya kisiasa wanasema ni fisadi halafu anasikilizwa mtu wa upande mmoja tu,hapo hamna kitu.
Halafu kuhusu swala la kanisa la katoliki kumwalika lowassa mbona sio issue ya ajabu mbona kuna watu walikuaga majambazi,wezi na matapeli sasa hivi wametubu na niviongozi wa kanisa,kanisa ni kimbilio la wenye zambi ili wasafishwe kwa damu ya yesu aliyewambwa pale msalabani.
 
MINI naona kama kigezo cha kutohudhuria lowassa kanisa katoliki ni RICHMOND BASI hata Kikwete alipaswa kuto alikwa katika harambe na Shughuli zote na KATOLIKI.

HATA PINDA AMBAYE NI MSEMAJI WA KIKWETE NAYE ANGEPINGWA!!!
SIJUI KAMA KASHISHA YA DAWA ZA KULEVYA INGEELEKEZWA KWA KATOLIKI???
 
Mimi ni mkatoliki
Kanisa lingejifunza kupitia kwenye scandal ya Freemasons. Kitendo cha jamaa wa freemasons kuwa karibu na viongozi wa kanisa katoliki kunalitesa na hadi kuna watu wengi tu wanaamini kuna uhusiano mkubwa wa Freemasons na Ukatoliki.
Hayo ndiyo yangu.
Ndugu yangu Kieleweke, nami pia ni Mkatoliki tena niliyebahatika kufika mpaka St. Peters, Basilica pale Rome. Pia nimevisoma vitabu vya mwandishi Malachi Martin kuhusu Ukatoliki, lakini kama Mkatoliki mwaminifu, hupaswi kuuzungumzia in public uhusiano huo wa Ukatoliki na Freemasons, na kudai wengi wanaamini!.. Weingi hao ni wewe na hao wengine lakini Wakatoliki wenyewe tunamuamini Mungu Mmoja katika Holly Trinity, na Kanisa ni Moja Tuu!, Takatifu Katoliki la Mitume!.

Tukirudi kwenye mwaliko wa Mhe. Edward Lowassa, nawaombeni sana, mnyonge, mnyongeni, haki yake mpeni!. Lowassa ana kosa gani?!.

Hata kama ni kweli ni mdhambi kihivyo, kwani Yesu alikuja kwa ajili ya nani?. Hakusema " Wote wenye mizigo, waje kwangu, nami nitawapumzisha?". Lowassa ameshaipeleka mizigo yake kunako husika, sasa anasubiri 2015 kuwatubia Watanzania katika ujumla wetu, na November, 2015, uwepo wa Mungu wa kweli, utajidhihirisha wazi na kuthibitisha kuwa "Mwacheni Mungu, Aitwe Mungu".
 
Hata kama watu wanacema ELo ametubu wakati hajawahi kutamka maneno either kutoa ufafanuzi wa tuhuma dhidi yake, au kuwaomba msamaha waTZ. Na hi toba n ya Kichina.
Kiresua, sisi Wakatoliki, kwanza, tunajutia dhambi zetu, na kujuta huko, tunajutia moyoni, pili tunatubu kwa Mungu na sii kwa mwanadamu, na mwisho tunafanya malipizi kwa kutenda yaliyo mema.

As far as EL is concerned, ana dhambi gani ya kutubia wananchi?.. Kwa vile yeye sii malaika, atakuwa alishajuta, ameshatubu, hiki mnachokiona na kukisikia sasa kuhusu EL ni kufanya tuu malipizi. 2015 rais atatoka Kaskazini.
 
naomba mwenye namba ya simu ya QS. pastory Masota anipe nimpe tahadhari kuu. jambo ninalojua mwenyekiti wa hii parokia pastory masota aligombea ubunge kwa tiketi ya ccm akaangushwa na dialo. huenda sasa anatumika bila kujua na asije akaliweka kanisa matatani. naomba mwenye simu yake anipe. nitampigia alikuwa mate wangu pale ARDHi insitute na ni mmiliki wa kampuni ya ujenzi ya ARMSTRONG INTERNATIONAL
 
Back
Top Bottom