Hizi ni mbinu zake tu za kutafuta kujisafisha, atangaze basi na kutowania urais mwaka 2015. Huyu ni mtu mwenye tamaa sana ya madaraka. Angekuwa mtu wa kupima na akiongozwa na busara angeweza sema, mimi uwaziri mkuu ulinishinda je urais itakuwaje? kwani kuna ulazima wowote wa yeye kuwa rais? tujiulize watanzania huyu mtu anapigania kuingia ikulu anataka akafanye nini hasa? Jamani mheshimiwa Lowasa kama unapitiaga JF, tafadhali pumzika ufanye shughuli zako zingine urais uwaachie wengine wanaoweza, sisi kuja kusikia tena mambo ya Richmond hatutaki tena, tumechoka. Watanzania tuliwaamini sana nyie ( wewe, rafiki yako Jk na maswaiba wenu) mlichoifanyia Tanzania mnakijua wenyewe. Sisi leo tunataabika, mambo yako hovyohovyo, hatutaki tena mturudishe huko jamani, kundi lenu haliwezi kuongoza nchi hii. waachie wengine.
Huo ushuhuda anaoenda kutoa ni kukufuru tu kama kweli yeye ni Mkristo anajua, kama atatubu kuwa ni kweli aliingilia mchakato wa Richmond na kuitumbukiza nchi kwenye hasara, mimi nitampongeza na watanzania wanaweza kumsamehe.
Ahsanteni wana sana.