Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na video "zilizovuja" katika mitandao zikimuonesha Mgombea wa UKAWA ndugu Edward Ngoyai Lowassa akiwa anasogezwa na kuandaliwa wakati wa kufanyiwa mahojiano yanayorushwa kwenye kituo cha TV cha ITV. Aliyezivujisha alikuwa na mpango wa kumdhalilisha kama inavyoonekana kwenye video hizo.
Lakini hizo sio video za Kwanza ama picha za kwanza, kumekuwepo na mfululizo wa video na picha mbalimbali zinazoonyesha Mzee akishindwa kuongea, ama akielekea msalani na nyinginezo za kumdhalilisha.
Leo, mchana huu akiwa kwenye ndege na Mheshimiwa Mbowe, imetumwa picha hii na kusambazwa kwenye mitandao ya Kijamii.
Simple analysis ya hii picha, inaonyesha mpiga picha amekusudia Ubaya, tena Ubaya dhahiri.
Mpiga picha alishindwaje kutafuta angle nzuri akapiga picha yenye kiwango hata atuletee picha haina quality, inamuonesha Mzee hajakaa stable, amepinda kama gari iliyokatika centrebolt. Lakini pia inamuonesha amefungwa fungwa mikanda kama vile hawezi kukaa bila mhimili wa mikanda hiyo..
Peni ya Mzee iko upside down, sasa hii maana yake nini..? Ukiiangalia kwa makini ni kama vile Mzee anasinzia, kwa ufupi ni picha mbovu inayodhalilisha.
Kama alikuwa anataka kumpiga picha kwa ajili ya Public kwanini asimuandae..?