Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi

Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi

Mkuu kuona kwangu aibu hakutonisaidia mimi kujifunza lkn kukubali kufahamishwa mambo nisiyoyafahamu hii hunisaidia zaidi kuliko kujifanya mjuzi wa mambo wakati mengine siyajui na huwa daima naamini ktk kujifunza zaidi

Saaafi sana. . . . . Umeonesha ukomavu. . .Hii ndio haswa siri ya wanaojua. . .Kiu ya kujua pasipo kuona aibu
 
Lowassa aliitishaje mkutano bila kuwasiliana na mamlaka anazodai ni za juu? Wanaendeleza uhuni uleule.
 
Lowassa aliitishaje mkutano bila kuwasiliana na mamlaka anazodai ni za juu? Wanaendeleza uhuni uleule.

Mkuu hayo maswali mnajiuliza leo!mlikuwa wapi msmpeleke kwenye vyombo vinavyo husika?
 
Tatzo waTz m2 unapouliz swal unatak uchague jinsi ya kujbiwa. Hii kasumba ya kumchagulia m2 majib haifai,kam hujaelew uliza tena, ukinichagulia jinsi ya kukujib maan yake huna 7bu ya kuniuliza. Keep quite!
 
Ccm mna shida wiki hii unajua alipokuwa ccm alibanwa na kuutetea mfumo yaani alijiuzuru kwa heshima ya mfumo mbovu (serikali ya ccm) sasa yuko nje huru habanwi tena maana ukiwa ccm unakuwa zezeta wa makusudi hata ukiona kweli husemwa sio kweli huku Chadema hakuna hiyo nyekundu nyekundu tisa ni tisa hakuna kugeuza wala kubanwa kama unataka kweli hamia chadema utapata kweli kweli tupu
 
Hivi ni kwa nini kila lowasa akiulizwa kuhusu Richmond anakuwa mkali!!!!??
 
We should learn from the past, but not be stuck in it. Sometimes life circumstances and personal setbacks can haunt and prevent us from seeing our true potential and recognizing new opportunities. What has already happened we cannot change, but what is yet to happen we can shape and influence. At times the first step is simply to break from the past and declare that it is you, not your history, who’s in charge. Goethe reminds us: “Nothing is worth more than this day.” Don’t dwell on the past. Make better choices today and move on.

For all the time I have been here in this forum. This is the best post ever.
 
Nimefuatilia sana comments zenu juu ya mtoa maada hapo juu, ila mie nasema hivi hebu watanzania tujaribu kufanya mabadiliko hata kwa MIAKA 5 TU, ili ccm nao waanze upya kujipanga kuliku kufanya chama cha FAMILIA ZA VIONGOZI, WAKITOKA WANAINGIA WATOTO WAO.PIA MFUMO WA CCM NDO TATIZO KUBWA SANA WALA SI LOWASA, KAMA TATIZO NI LOWASA MBONA BAADA YA KUACHIA NGAZI YA UWAZIRI MKUU AKAINGIA PINDA ALIYEJIITA MTOTO WA MKULIMA BADO YAKAIBUKA DOWNS, ESCROW & GASI,, NNA HATA WATU KUGOJI SAINI YAKE NA KUCHANGISHA FEDHA KUONGA WABUNGE KUPITISHA BAJETI MBOVU YA WAIZARA YA NISHATI NA MADINI..NAMPONGEZA SANA LOWASA
 
Usanii mnafanya nyie msioridhika,badala ya kumwandama aliyesema anahusika na Richmond, akili zenu zimeganda kwa EL! LOWASA has been pushed to the limit,cant you see it with your naked eyes??!!


Mie niko consistent..., napinga ufisadi toka umewekwa wazi na Dr.Slaa.., JF sijaja leo wala Jana.., ninaowashangaa ni wale waliopiga U-TURN za kufa mtu kisa bwana pesa yuko kwenu sasa hivi..,

HUO NI UNAFKI.
 
Wadau Habari; jana ilikuwa siku ya kipekee sana kwa historia ya Tanzania ambayo tuliahidiwa na tuliisikia minong'ono mingi na tetesi za kila leo juu ya kuhama chama kwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiket ya CCM ndugu, EL.

Binafsi nampongeza kwa kuitumia haki yake ya kidemocrasia na kufanya maamuzi magumu; kama mtanzania nisiyefungamana na upande wowote nimestaajabishwa sana na mambo mawili makubwa.

Mosi ni juu ya umiliki wake wa card ya CCM, EL inasemekana ana miliki card namba 15 ya Uwanachama ndani ya CCM, lakini siku ya jana alijivua uwanachama na kupewa rasmi card ya CDM, sasa bado najiuliza imekuaje kamanda huyu amejiondoa CCM na kwenda CDM lkn bado anamiliki card ya chama hicho? Maana jana sikuona akiirudisha card ya CCM ili ichanwe chanwe pale mbele ya macho yetu.

Lakini kama hiyo haitoshi bado najiuliza inawezekanaje Kiongozi mkubwa kama yeye anathubutu kutoa majibu ya hasira mbele ya Taifa hili juu ya swali la msingi ambalo lilimchafua yeye na baadhi ya Viongozi wa wizara husika.

Kwa kusema kwamba NANUKUU; "Nilipoitisha kikao cha "Government negotiation team" nikawauliza mbona nasikia huu mkataba una matatizo?

mimi nina uzoefu wa kuvunja mikataba na huu tuuvunje! wakaomba ruhusa watoke nje kwa saa moja, baada ya hapo waliporudi wakasema wamepigiwa simu toka mamlaka ya juu mkataba usivunjwe "what else could I have done?"

Mwisho wa KUNUKUU, Sasa najiuliza hapa inawezekanaje PM umeitisha kikao cha subordinates wako alafu anatokea wa kukuambia kuwa et nimewasiliana na wakuu wamekataa hilo, nani basi mwenye kupaswa kufanya consultation na Wakuu wenzake kati ya watu hawa wawili EL kama PM au Subordinates?

Lakini pia napata shaka pale namna ambavyo swali la msingi lilivyojibiwa kwa kusema kwamba, NANUKUU; "Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye ushahidi wa mimi kuhusika na Richmond aende mahakamani, kama huna just shut up. Nilichukua uamuzi kwa niaba ya serikali.

Nimeondoka madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka yamepungua, mikono yangu ni misafi na mtu mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele, peleka mahakamani" mwisho wa KUNUKUU; Kwa uelewa wangu wa kawaida kabisa unyeti wa jambo hili haukutaka jibu la namna hii bali watanzania tungeridhishwa zaidi endapo tungepata majibu mazuri kwa kina na yenye kujitosheleza badala ya kuwa mkali kiasi ambacho inatuacha na maswali mengi kwamba ile ni namna ya kututisha na kutuziba midomo kama ambavyo ilitokea pale kwa wana habari wenzangu au ni nini hasa?

Kama hii haitoshi bado najiuliza, Je na ile hoja ya Dr.Slaa kwamba ushahidi wa jambo hili anao na yupo tayari kwenda kuthibitisha mahakamani leo hii sisi watanzania tunaibebaje hii statement kuwa naye alikuwa anabwabwaja tu au namna gani?

Lakini nathubutu kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza Dr.Slaa na wenzake wanasimama vipi Jukwaani kumnadi kwa kumtakasa mtu huyu ambaye wao walikuwa wanachangia kumchafua?

Mambo haya yananipa shida kuyapatia majibu basi nabaki kujiuliza bila mafanikio naombeni wadau mnisaidie kung'amua.
"Majibu ya hasira kwa swali la Msingi"

wewe ni gamba
 
Wewe kwani unataka majibu yapi mengine? kama unayajua majibu si yanakutosha ila Edo ndo kashajibu hapo usitake kulazimisha aseme unachotaka kusikia wewe.
Pili kama simu imepigwa na bos tena kwa surbodinaes wako,huko ni kudhalilishwa sasa wewe ulitaka akaongee nini nae huyo boss wake wakati alishatoa jibu!
Kama hujaridhika msaidie kujibu wewe! kama bado una donge nenda mahakamani
 
Mie niko consistent..., napinga ufisadi toka umewekwa wazi na Dr.Slaa.., JF sijaja leo wala Jana.., ninaowashangaa ni wale waliopiga U-TURN za kufa mtu kisa bwana pesa yuko kwenu sasa hivi..,

HUO NI UNAFKI.

Nenda ACT wanakusubiri kwa hamu
 
Nenda ACT wanakusubiri kwa hamu

Nyie mnaofuata fuata watu nyuma ndio huishia kugeuzwa mapunguani, kama mbowe alivyowafanya jana. Napinga ufisadi kama mtazania. INATOSHA.

sihitaji kumfuata mtu popote au kujilazimisha kufuata tantalila za chama chochote kile. Mimi ni mtu huru.

Nyie mnaosubiri mbowe afikiri na kichwa chake kibovu, halafu ndio muanze na nyie kurudia uporoto alioutoa mmeona yanayowakuta..,

vijeba juzi tu mlikuwa mnakaza mishipa ya shingo kumtukana Lowassa Fisadi, leo hii mnamuita mtakatifu. Njaa shida.

By the way, kuna zawadi natoa kwa yeyote atakayeniletea tweet, text,facebook post or forum post ya Mnyika,Dr slaa na Mdee..,

maana makamanda aibu zimewashika hata simu zimekuwa za moto.

deadline leo saa sita usiku.

kazi kwako
 
Hivi mbona watu mnajidai kujua kitu kabla ya muda wake!!!?? Suala la CHADEMA au UKAWA watamnadi vipi ENL si msubiri kipindi cha kampeni!!! Wewe unachotaka sasa hivi ni nini? Unataka watu wakupe utabiri?

[Hi ni ishara ya kupanic]
 
wa ccm wa ubadhirifu naona mpoo kazini.....ye waziri mkuu ndio maana kaitisha kikao bila mamlaka za juu
 
Ccm mna shida wiki hii unajua alipokuwa ccm alibanwa na kuutetea mfumo yaani alijiuzuru kwa heshima ya mfumo mbovu (serikali ya ccm) sasa yuko nje huru habanwi tena maana ukiwa ccm unakuwa zezeta wa makusudi hata ukiona kweli husemwa sio kweli huku Chadema hakuna hiyo nyekundu nyekundu tisa ni tisa hakuna kugeuza wala kubanwa kama unataka kweli hamia chadema utapata kweli kweli tupu

We kweli bado ujakomaa kisiasa na haufatilii,hebu jiulize huyo lowasa waliempokea leo ilikuwaje kipindi cha nyuma walimwongeaje hao viongozi wa chadema lakn leo n rafk kwao na mtu muhimu.Jenga picha akilin mwako uone kama co unafki na usalit huo wanaowafanyia watanzania
 
Nimefuatilia sana comments zenu juu ya mtoa maada hapo juu, ila mie nasema hivi hebu watanzania tujaribu kufanya mabadiliko hata kwa MIAKA 5 TU, ili ccm nao waanze upya kujipanga kuliku kufanya chama cha FAMILIA ZA VIONGOZI, WAKITOKA WANAINGIA WATOTO WAO.PIA MFUMO WA CCM NDO TATIZO KUBWA SANA WALA SI LOWASA, KAMA TATIZO NI LOWASA MBONA BAADA YA KUACHIA NGAZI YA UWAZIRI MKUU AKAINGIA PINDA ALIYEJIITA MTOTO WA MKULIMA BADO YAKAIBUKA DOWNS, ESCROW & GASI,, NNA HATA WATU KUGOJI SAINI YAKE NA KUCHANGISHA FEDHA KUONGA WABUNGE KUPITISHA BAJETI MBOVU YA WAIZARA YA NISHATI NA MADINI..NAMPONGEZA SANA LOWASA

Tatizo co kubadili vyama hapa kuwatoa ccm wala kumweka nan hapo juu,shida ni kumpata kiongozi bora haijalishi anatokea upande upi ili mradi aweze kusimamia mambo ya watanzania yaende kama yanavyotakiwa.Tuondokane na hii dhana ya kwamba tumpe ukawa mara ccm wote hawa wapo wazur na wabaya nakwambia weng wao wanajal mifuko yao tu hawana maana hata huyo lowasa ambae tunaona n mzur sasa ngojea aingie na kikoc chake utaona moto hao n watoto wa ccm labda kizazi kijacho ambacho hakiijui ccm ndo kitaweza kusimamia mambo vizur lakn co hawa wazee wa sasa,badilika na chukua hatua sasa
 
Back
Top Bottom