Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi

Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi

........Daah, Mkuu mbona unadhalilisha fani ya uandishi wa habari? Huoni hata aibkujitambulish kuwa ni mwandishi wa habari kasha unaandika "ukoko" namna hii?
 
Wewe ulipoacha kazi na kumia kampuni nyingine ulirudisha na tshirt zote za ofisi??
 
Wadau Habari; jana ilikuwa siku ya kipekee sana kwa historia ya Tanzania ambayo tuliahidiwa na tuliisikia minong'ono mingi na tetesi za kila leo juu ya kuhama chama kwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiket ya CCM ndugu, EL.
Binafsi nampongeza kwa kuitumia haki yake ya kidemocrasia na kufanya maamuzi magumu; kama mtanzania nisiyefungamana na upande wowote nimestaajabishwa sana na mambo mawili makubwa.
Mosi ni juu ya umiliki wake wa card ya CCM, EL inasemekana ana miliki card namba 15 ya Uwanachama ndani ya CCM, lakini siku ya jana alijivua uwanachama na kupewa rasmi card ya CDM, sasa bado najiuliza imekuaje kamanda huyu amejiondoa CCM na kwenda CDM lkn bado anamiliki card ya chama hicho? Maana jana sikuona akiirudisha card ya CCM ili ichanwe chanwe pale mbele ya macho yetu.
Lakini kama hiyo haitoshi bado najiuliza inawezekanaje Kiongozi mkubwa kama yeye anathubutu kutoa majibu ya hasira mbele ya Taifa hili juu ya swali la msingi ambalo lilimchafua yeye na baadhi ya Viongozi wa wizara husika.
Kwa kusema kwamba NANUKUU; "Nilipoitisha kikao cha "Government negotiation team" nikawauliza mbona nasikia huu mkataba una matatizo? mimi nina uzoefu wa kuvunja mikataba na huu tuuvunje! wakaomba ruhusa watoke nje kwa saa moja, baada ya hapo waliporudi wakasema wamepigiwa simu toka mamlaka ya juu mkataba usivunjwe "what else could I have done?" Mwisho wa KUNUKUU, Sasa najiuliza hapa inawezekanaje PM umeitisha kikao cha subordinates wako alafu anatokea wa kukuambia kuwa et nimewasiliana na wakuu wamekataa hilo, nani basi mwenye kupaswa kufanya consultation na Wakuu wenzake kati ya watu hawa wawili EL kama PM au Subordinates?
Lakini pia napata shaka pale namna ambavyo swali la msingi lilivyojibiwa kwa kusema kwamba, NANUKUU; "Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye ushahidi wa mimi kuhusika na Richmond aende mahakamani, kama huna just shut up. Nilichukua uamuzi kwa niaba ya serikali.
Nimeondoka madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka yamepungua, mikono yangu ni misafi na mtu mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele, peleka mahakamani" mwisho wa KUNUKUU; Kwa uelewa wangu wa kawaida kabisa unyeti wa jambo hili haukutaka jibu la namna hii bali watanzania tungeridhishwa zaidi endapo tungepata majibu mazuri kwa kina na yenye kujitosheleza badala ya kuwa mkali kiasi ambacho inatuacha na maswali mengi kwamba ile ni namna ya kututisha na kutuziba midomo kama ambavyo ilitokea pale kwa wana habari wenzangu au ni nini hasa?
Kama hii haitoshi bado najiuliza, Je na ile hoja ya Dr.Slaa kwamba ushahidi wa jambo hili anao na yupo tayari kwenda kuthibitisha mahakamani leo hii sisi watanzania tunaibebaje hii statement kuwa naye alikuwa anabwabwaja tu au namna gani?
Lakini nathubutu kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza Dr.Slaa na wenzake wanasimama vipi Jukwaani kumnadi kwa kumtakasa mtu huyu ambaye wao walikuwa wanachangia kumchafua?
Mambo haya yananipa shida kuyapatia majibu basi nabaki kujiuliza bila mafanikio naombeni wadau mnisaidie kung'amua.
"Majibu ya hasira kwa swali la Msingi"

Mkuu sarakasi za siasa ziko nyingi tu, jaribu kumuuliza Mh Salaa kadi yake ya CCM iko wapi, au jaribu kumuuliza Mh Wassira kadi yake ya NCCR iko wapi, au jaribu kuuliza Mrema ameweka wapi kadi zake za CCM na NCCR.

Mkuu unatakiwa kujua kuwa Tanzania ina mfumo wa utawala. U-dogo hautegemei cheo peke yake, pia unategemea aliyekuteua. Mkuu wa mkoa anaweza kuwa juu ya mkuu wa wilaya, lakini anajibu kwa Rais na si kwa mkuu wa mkoa. Ni sawa na mwanasheria mkuu wa serikali, naye pia ni mteuliewa wa rais kwa hiy anajibu kwa rais. ...tatizo ni kuwa Lowassa amejibu swali hilo mara nyingi na watu wanaeldelea kuuliza. Sasa ninachokiona ni kuwa watu wanaouliza hawajui jibu lenyewe na wengine hawajasikia jibu lenyewe.

Sasa tusubiri kama wanaotajwa watakanusha au hawatakanausha. Maana uamuzi kutoka juu maana yake ya moja kwa moja ni kutoka kwa Rais, maana huyo ndiye yuko juu ya AG na juu ya PM, huo ni uelewa wangu mdogo. Kwa tafsiri nyingine Lowassa anatuambia kuwa Rais ndio Richmond, na amesema wazi kuwa mwenye ushahidi kuwa ni yeye autoe au aende mahakamani.

Swali lake lingekuwa la msingi kama lingelenga kwenye issue ya chain of command na centers of decision making
 
Swala la kurudisha kadi ya CCM nalo neno! Swala la RICHMOND bado lina ukakasi,kuna mambo yapo chini ya kapeti, Slaa na atabanwa atoe ushadihi aliosema anao kuhusu ufisadi wa Lowassa
 
kumbe lowasa kweli alikua mkongwe ccm,kadi namba 15 si mchezo asee,huyo ni mwanzilishi
 
Okay, naanza kuelewa sasa sio watanzania wote tunauwezo wa kupambanua kila herufi na hii ipo ndio maana hata darasani mwalimu hutumia namna mbadala ya kumfanya mwanafunzi aelewe kwa wepesi; hii ina maana kwamba tunatofautiana uelewa, Asante kwa kunielewesha.

Sasa imenikumbusha ya ESCROW Ndulu kaandika barua na Mkuu wa kaya kaandika ya kwake kupitia Katibu wake,na Mwanasheria akatoa kadi ya kijani.......................

Na katibu wa Mkullu naye yupo kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge............

Ah!!!!!!!!!!!! Na mie naomba kwenda IKULU kuna biashara huko........................
 
Swala la kurudisha kadi ya CCM nalo neno! Swala la RICHMOND bado lina ukakasi,kuna mambo yapo chini ya kapeti, Slaa na atabanwa atoe ushadihi aliosema anao kuhusu ufisadi wa Lowassa

Wala hana sababu,alikuwa Mpiga Filimbi wa Hameline,akapiga ikasikika..................Matokeo tukayaona na tunaendelea kuyaona hana hatia yakutupigia Filimbi......................
 
Lowassa kapoteza. Chadema hawawana cha kupoteza kwanza Mbowe kashavuta tayari
 
Swala la kurudisha kadi ya CCM nalo neno! Swala la RICHMOND bado lina ukakasi,kuna mambo yapo chini ya kapeti, Slaa na atabanwa atoe ushadihi aliosema anao kuhusu ufisadi wa Lowassa

Hapo nami nasubiri kiongozi wetu mpendwa slaa,mchukia mafisadi jumatatu awasilishe ushahidi mahakamani.
 
Katika hoja yak o ya msingi kuna maswali kadhaa... nanukulu

"Kwa uelewa wangu wa kawaida kabisa unyeti wa jambo hili haukutaka jibu la namna hii bali watanzania tungeridhishwa zaidi endapo tungepata majibu mazuri kwa kina na yenye kujitosheleza badala ya kuwa mkali kiasi ambacho inatuacha na maswali mengi kwamba ile ni namna ya kututisha na kutuziba midomo kama ambavyo ilitokea pale kwa wana habari wenzangu au ni nini hasa?

Kama hii haitoshi bado najiuliza, Je na ile hoja ya Dr.Slaa kwamba ushahidi wa jambo hili anao na yupo tayari kwenda kuthibitisha mahakamani leo hii sisi watanzania tunaibebaje hii statement kuwa naye alikuwa anabwabwaja tu au namna gani?
Lakini nathubutu kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza Dr.Slaa na wenzake wanasimama vipi Jukwaani kumnadi kwa kumtakasa mtu huyu ambaye wao walikuwa wanachangia kumchafua?"
Mwisho wa kunukulu


Sasa hapa ulipata wapi shida ya kuuliza haya maswali kwa Lowasa?? au hata kwa viongozi wengine wa aidha CHADEMA au UKAWA?
Acha uzandiki.. itakuwa vyema utafute nafasi ya kuhojiana nae ili uje na majibu na sio kuona hasira kwa utashi wa macho yako au uoga wa kukosa kujiamaini!

 
Kama atawezesha CDM kuiondoa ccm madarakani potelea mbali yaliyopita tutaona la kufanya huko mbele. Adui wetu sote ni ccm tumpige kwanza
 
Majibu ya hoja zako hizo yako kwenye hotuba ya Mbowe na kama hukumuelewa Mbowe hata akishuka malaika kutoka mbinguni kuja kukuelewesha hautamuelewa.


Mkuu tatizo la hawa CCM wamezoeshwa kukaririshwa ,wanashindwa kujenga picha hata kwa kusikia taarifa..Hotuba za Jana za viongozi wote zilibeba sehemu kubwa ya maswali mengi tuliyokuwa nayo kama wananchi.
 
........Daah, Mkuu mbona unadhalilisha fani ya uandishi wa habari? Huoni hata aibkujitambulish kuwa ni mwandishi wa habari kasha unaandika "ukoko" namna hii?

Mkuu kuona kwangu aibu hakutonisaidia mimi kujifunza lkn kukubali kufahamishwa mambo nisiyoyafahamu hii hunisaidia zaidi kuliko kujifanya mjuzi wa mambo wakati mengine siyajui na huwa daima naamini ktk kujifunza zaidi
 
Duh!!unahis hayo ni majibu.."am sick of tired..." ebu hacheni ushabiki kwa yanayohitaji ufafanuzi ambao hajawahi utoa ata siku moja,anang'ana alishatoa wakati kila siku anasema yale yale

Jibu la maswali yako tumekosa, Tukupe mji utuambie maana ya kitendawili chako?
 
Magamba tukutane october..naomba niwajulishe nimejiandikisha na kadi nnayo
 
Back
Top Bottom