LOWASA NA KAULI ZA KILAGHAI:
Mgombea wa urais, Lowasa amezidi kuwahadaa Watanzania kwa kauli zake za kilaghai.Hususani anaposema,
Anachukia umasikini na huchukii rushwa sasa ataondoaje umasikini huo?
Anasema anachukia umasikini wala haoneshi kuwa na mipango yoyote ya kiuchumi na kimkakati ya kuiondoa Tanzania kwenye umasikini.
Anachukia umasikini wala haoneshi kama anawachukia marafiki zako wengi wakwepa kodi na wengi wapigaji wanajulikana kwa majina, atauondoaje huo umasikini?
Anachukia umasikini nusu ya Umri wa Maisha yake ameishi Ostabay , juzi tu ndo amepanda daladala kuigiza na ndo ameenda Mbagala ambayo sisi haya ndo maisha yetu,
Na akiwa Ostabay nusu ya marafiki zako ni matajiri tu , Siku zote ndani ya magari ya tinted majirani tajiri , marafiki tajiri anachukia umasikini vipi kama sio ulaghai.
Kama kweli anauchukia umasikini alipo kuwa kiongozi alifanya initiative gani kuiondoa Tanzania kwenye umasikini zaidi ya kushiriki, kuharibu na kuchukua hata vile vidogo ambavyo vingewasaidia watanzania.
Kama anachukia umasikini kule nyumbani Monduli pamoja na utajiri alio nao amewasaidiaje vijana? tuanze kumpima hapo kama kweli kwa sababu sharing is caring and charity begun at home, Maisha ya Monduli ni magumu kupindukia na vijana wanakimbilia Dar es Salaam wakati yeye tajiri!!! Hata kiwanda cha kusindika maziwa ameshindwa kujenga kule Monduli,kama sio ulaghai ndo ataweza kuondoa umasikini!
MTU ambaye ni sehem ya umasikini huu tena kwa kiwango cha juu kabisa anapokuja na nyimbo nzuri kama hizo muda kama huu , atazamwe kwa macho makali usoni , sura na anacho kizungumza mdomoni ni vitu viwili tofauti.
Tafakari kwa Sauti!!!!