Lowassa na kauli za kilaghai

Lowassa na kauli za kilaghai

nimeelewa sana uzi wako na hakika hii ni tafukuru chokonozi imara ambayo tunapaswa kujihoji ni kwa namna gani sanaa kama taaluma ya awali inavyoendelezwa mpaka kwenye maisha halisi ya watu
 
Ndo maana hawezi kukaa mikoani, kila akienda anakumbuka maisha ya hanasa mjini anaamu kurudi dar, hawezi kutusaidia sisi wa chini hata kwa miaka 20, hawezi. Amezidiwa na akina Mkono,Dewji na Abood, wamesaidia sana kwao tena kwa kutoa pesa zao mifukoni wakati mwingine na wote wakiwa CCM, huyu Lowassa ni mpigaji, yeye anajua kupiga tu.

Kwanza,KWANINI UMFANANISHE MO.DEWJI(Tajiri no.1 TZ kwa sasa,no.27 in top50 richest men in africa/akiwa ni mtazania pekee kushika nafasi hiyo ya juu kwenye chart hiyo...source:FORBES-2015) Na LOWASSA???
 
Nani kakuambia matatizo huwa yanaisha hapa duniani? Matatizo yataendelea kuwepo tu siku zote ndio maana hata katika nchi zilizoendelea kuna sera na chaguzi. Sera na ahadi zitakuwepo sikuzote za maisha yetu hapa duniani. Mpaka leo ulaya na marekani bado kuna matatizo na yataendelea kuwepo sembuse hapa kwetu Tanzania?? Mfano mzuri angalia jirani zako hapo Kenya, walisema wanataka mabadiliko, wakayapata, matokeo yake matatizo yao yamezidi tena zaidi, sasa hivi tunavyoongea waalimu wamegoma na serikali imetangaza kuwafukuza kazi wote watakaoshindwa kurudi makazini. Wakati huo huo Uhuru Kenyatta amesema serikali yake haina pesa za kuwalipa, wakati yeye mwenyewe ni tajiri wa kutupa tena hana tofauti na huyo lowassa wenu anayewadanganya.

Jambo la msingi bhana ni kuangalia ukweli tu. Ukiujua ukweli utakuweka huru. CCM sio chama kibaya, lakini kilikuwa kinamalizwa na watu kama akina lowassa ambao ni mafisadi. Magufuli ni mtu safi na tuna uhakika ataibadilisha CCM na kuanzia November mwaka huu utajiaonea wewe mwenyewe uchapakazi wa Dr. Magufuli. Magufuli atashinda urais na sio kama atamaliza matatizo yote lakini nafuu itaonekana. #HapaKaziTu chagua MAGUFULI.
Mkuu kwa taarifa yako tu ni kwamba Magufuli kashaanza kumpongeza Lowassa. Na hilo nampongeza Magufuli kwani ni kuonyesha kuanza kukomaa kisiasa tofauti na alipo anza kampeni. Lifanyie kazi utaupata ukweli.
 
lazima tuwe namaswali ya kujiuliza kama haya ingekuwa ni vyema sana
tusiwe kama nyumbu tuu tunashangilia tuu bila kujijua,lowassa tunae mwongelea ni nani?fisadi hatuna haja na mtu aliye tufilisi taifa hili
 
anauchukia umaskini ndo maana alikaa
osyerbay na sio manzese,hivi magufuli anavyo sema serikali ya magufuli itakuwa ya viwanda wakati umeme hata wakuwasha mafriji ya soda ni shida hivyo viwanda vitaendeshwa kwa mishumaaa?

Mkuu hawa MAFISIEMU WAONGO SANA...ETI HUYO MAGUFULI WAO ANASEMA TANZANIA YANGU ITAKUWA "TANZANIA YA VIWANDA"...SASA SIJUI HIVYO VIWANDA VINAENDESHWA NA KOKOTO AU...MAANA KWA SASA TUNAONA ATA HUO UMEME WA KUWESHA TV TUANGALIE TAARIFA YA HABARI HAUPO,SASA SIJUI HUYO MAGUFULI WAO ANAPOTOA AHADI ANAMAANISHA AU ANAFIKIRI ANAWAAMBIA WATOTO???,MARA ASEME ATAJENGA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA...MBONA ALIVYOKUWA WAZIRI WA UVUVI HATUKUONA HICHO KIWANDA CHA SAMAKI HATA KIMOJA???...,MARA MIL.50 KILA KIJIJI UTADHANI KAAMBIWA WANANCHI WANASHIDA NA PESA...BADALA YA KUSHUSHA BEI BIDHAA ILI WANANCHI WATUMIE KIDOGO WANACHOKIPATA KWENYE MIHANGAIKO YAO YA KILA SIKU KUMUDU GARAMA ZA MAISHA,YANI WOTE WAONGO HADI YULE MGOMBEA MWENZA WA CCM NDO BALAAA...WEWE ONA HAPO⬇
IMG-20150913-WA0002.jpg
 
Kati ya kauli inayonikera ni ati ataanzisha benki ya wenye bodaboda na mama lishe, je wakulima sio marafiki zake ambao ni 80% ya wa Tanzania?

Labda kama wewe ni gamba,maana unavyosema "je wakulima"...unafikiri ataanzisha benki ngapi???,KUMBUKA WAKULIMA AMESHAWAJALI KWA UPANDE WAO NA ALISEMA "ATA WAFUTIA KODI NA USHURU KWENYE MAZAO YAO,ATAWAONDOLEA MFUMO WA STAKABADHI GHALANA,MAZAO YATAKUWA NA RIBA"...SIKUELEWI UJUE ULITAKA AWAGUSIE VIPI WAKULIMA???
 
LOWASA NA KAULI ZA KILAGHAI:

Mgombea wa urais, Lowasa amezidi kuwahadaa Watanzania kwa kauli zake za kilaghai.Hususani anaposema,

Anachukia umasikini na huchukii rushwa sasa ataondoaje umasikini huo?

Anasema anachukia umasikini wala haoneshi kuwa na mipango yoyote ya kiuchumi na kimkakati ya kuiondoa Tanzania kwenye umasikini.

Anachukia umasikini wala haoneshi kama anawachukia marafiki zako wengi wakwepa kodi na wengi wapigaji wanajulikana kwa majina, atauondoaje huo umasikini?

Anachukia umasikini nusu ya Umri wa Maisha yake ameishi Ostabay , juzi tu ndo amepanda daladala kuigiza na ndo ameenda Mbagala ambayo sisi haya ndo maisha yetu,

Na akiwa Ostabay nusu ya marafiki zako ni matajiri tu , Siku zote ndani ya magari ya tinted majirani tajiri , marafiki tajiri anachukia umasikini vipi kama sio ulaghai.

Kama kweli anauchukia umasikini alipo kuwa kiongozi alifanya initiative gani kuiondoa Tanzania kwenye umasikini zaidi ya kushiriki, kuharibu na kuchukua hata vile vidogo ambavyo vingewasaidia watanzania.

Kama anachukia umasikini kule nyumbani Monduli pamoja na utajiri alio nao amewasaidiaje vijana? tuanze kumpima hapo kama kweli kwa sababu sharing is caring and charity begun at home, Maisha ya Monduli ni magumu kupindukia na vijana wanakimbilia Dar es Salaam wakati yeye tajiri!!! Hata kiwanda cha kusindika maziwa ameshindwa kujenga kule Monduli,kama sio ulaghai ndo ataweza kuondoa umasikini!

MTU ambaye ni sehem ya umasikini huu tena kwa kiwango cha juu kabisa anapokuja na nyimbo nzuri kama hizo muda kama huu , atazamwe kwa macho makali usoni , sura na anacho kizungumza mdomoni ni vitu viwili tofauti.

Tafakari kwa Sauti!!!!

kwa hizo ahad za ccm kwenye kampen huwa zinatekelezka wakipata madaraka?
acha ushabiki mandazi cc tunaimani nae hata akikaa kimya asiongee lolote ni tutampigia kura tyu maana hamna namna tumechoshwa na kitu kinaitwa ccm kifie mbali yan tulivyo choshwana hiko chama hata ukawa wangeeka jiwe tungelipigia tyu na kwan huyo magufuli ana sera gan ambayo ina mashiko zaid ya kushangaa na kupiga push up kwenye majukwaa!pili yy mbona alikuw wazir tena ndio mshaur wa raisi alishindwaje kuuondoa umaskin kipind yupo wazir wa miundo mbinu na akiwa kama mshaur wa rais sasa hv anajifanya anaweza.ccm ife tyu imetutesa vya kutosha sasa baaaaaaaasi.kura ya kwa rowasa na za marafik zangu zaid ya 200 wana iman na lowasa co maccm.
 
Labda kama wewe ni gamba,maana unavyosema "je wakulima"...unafikiri ataanzisha benki ngapi???,KUMBUKA WAKULIMA AMESHAWAJALI KWA UPANDE WAO NA ALISEMA "ATA WAFUTIA KODI NA USHURU KWENYE MAZAO YAO,ATAWAONDOLEA MFUMO WA STAKABADHI GHALANA,MAZAO YATAKUWA NA RIBA"...SIKUELEWI UJUE ULITAKA AWAGUSIE VIPI WAKULIMA???

achana nae huyo gamba usikute ana maslah na ccm yake atuache cc malofa twende na mabadiliko
 
Mbona wamasai wanalia kwao mondulo lowassa ni mlaghai sana
 
achana nae huyo gamba usikute ana maslah na ccm yake atuache cc malofa twende na mabadiliko

Mnanichekesha kabisa
Eti mwataka mabadiliko

Anzen na katiba ya chadema isiyokuwa hata na tone la demokrasia

Fanyen uchaguz wa mwenyekiti wa chadema
Na sio kuchaguliwa na mtei
mkishayafanya hayo njoon sasa tujadiliane kama kweli tunahitaji mabadiliko ndani ya ccm au nje ya ccm

Cc.
nyumbu wote
 
Ili nchi yoyote iendelee inahitaji viwanda kwaajili ya kupunguza kuagiza vitu kutoka nje
Na pia duala la ajira

Ili ujenge uchumi wa viwanda huna budi kuwa na soko la ndani na nje
Pia uwe na malighafi pamoja na wataalam wake
Bila kusahau umeme wa kuaminika

Yote tunayo ila Umeme ndo tulikuwa hatujakamilisha
Lakin sasa umeme umeanza kuwa stable
Kukatika katika kwa umeme saiv n sabsb ya uwashwaji wa mitambo ya gesu ya mtwara na majaribio mbalimbali yanayofanywa
Bt baada ya hapo
Tanzania nzoma tutakuwa tunatumia umeme wa gesi
Na
Mgao w Umeme utakuwa n historia tena Tanzania
Huu ndio tunauita ulaghai
 
Back
Top Bottom