Lowassa na Jakaya Kikwete ndio Maadui wakuu wa ushindi wa CCM 2015 sio CHADEMA

Niseme nini? Mimi naona hatua ya kwanza tuiondoe CCM madarakani. Nikisema sasa hivi watani-Kolimba

Nani akukoombe mkuu? Lete tu hapa ndiomaana yakuweka ID fake hakuna wakukukolimba, labda mimi ndio niogope!
 
hivi ushindi wao unatokana nanini hasa maana mwawakataa mno yakheeeeeee

Ushindi gani mkuu?

Tanzania ina idani ya watu 45milioni kwa sensa 2000 kati yao wapiga kura ni 26 milioni

Sasa nikuulize Kikwete alichaguliwa na wapiga kura wangapi mwaka 2010?

Watz waliopiga kura ni 5+ milioni, jiulize kwanini ni hao tu?

Kikwete alishinda kwa kura 3+ milioni, jiulize kwa nini?

Je rais wa watu wanaokadiriwa 50milioni anaweza kuchaguliwa na watu 3+ milioni??

Haiingii akilini mtu kusifu ushindi wa aina hiyo, bali kulaani
 
Huyu Yericko Nyerere ni ccm, wanachadema hawawezi kutoa ushauri mzuri hivi

Umeona eeh. Yericko Nyerere ni CCM damu. Ana uchungu kabisa na chama chake ndo maana ametoa ushauri mzuri sana ili chama kiendelee kutawala. Hakuna mtu yeyote aliyewahi kumpa adui yake ushauri mzuri ili eti aendelee kudumu. Kawaida humwombea maisha mabaya na kifo juu! Yericko ni rafiki wa CCM, ndo maana hapendi kuona kinatoswa 2015. Asante mkuu Yericko. Ushauri wako utazingatiwa na amini usiamini mwaka 2015 CCM kitaendelea kuwa chama tawala, CHAMA KUBWA.
 
Swali lako halina mlingano wa ccm na chadema!

Labda ungesema ipi tofauti kati ya mgomba na mpapai?

Ipi kubwa kati ya 35 na 20,tofauti ya namba hizo jumlisha 2000 ndizo zinatusumbua kila siku hapa jf.Kiukweli ni chama kizuri but hakina mizizi mirefu kama iulivyo mbuyu (CCM),chenyewe kimejiimalisha kwenye matunda yaliyo juu tu (mgomba) ambapo yeyote apitae hutamani matunda yake na pindi wakitokea watu zaidi ya wawili walio na nguvu sawa kuyagombania matunda yake na mmojawapo akawa na panga kali (pesa/nafasi) kuliko mwenzake basi mgomba huu utakatwa mara moja ama kwa hasira au wivu wa ndizi zinazokaribia kuiva.Kwani mmojawapo anaweza sema ni bora tugawane tu ili wakuvundika na akavundike.Kuhusu mbuyu (CCM) sifa yake kuu ni kuwa na mizizi mirefu,minene na matunda yake hukomaa kwa tabu sana na matunda yake kuanzia gamba lake la juu na mbegu zake ni ngumu na hata ukizisugua mbegu zake sakafuni tayari moto utapata.
 
Umeona eeh. Yericko Nyerere ni CCM damu. Ana uchungu kabisa na chama chake ndo maana ametoa ushauri mzuri sana ili chama kiendelee kutawala. Hakuna mtu yeyote aliyewahi kumpa adui yake ushauri mzuri ili eti aendelee kudumu. Kawaida humwombea maisha mabaya na kifo juu! Yericko ni rafiki wa CCM, ndo maana hapendi kuona kinatoswa 2015. Asante mkuu Yericko. Ushauri wako utazingatiwa na amini usiamini mwaka 2015 CCM kitaendelea kuwa chama tawala, CHAMA KUBWA.

Asante sana kwa kuupokea ushauri wangu,

Kama kweli unaamini chama cha ccm kitaupokea itakuwa heri, japo ni 0.09% ya kuupokea!
 
Ipi kubwa kati ya 35 na 20,tofauti ya namba hizo jumlisha 2000 ndizo zinatusumbua kila siku hapa jf.Kiukweli ni chama kizuri but hakina mizizi mirefu kama iulivyo mbuyu (CCM),chenyewe kimejiimalisha kwenye matunda yaliyo juu tu (mgomba) ambapo yeyote apitae hutamani matunda yake na pindi wakitokea watu zaidi ya wawili walio na nguvu sawa kuyagombania matunda yake na mmojawapo akawa na panga kali (pesa/nafasi) kuliko mwenzake basi mgomba huu utakatwa mara moja ama kwa hasira au wivu wa ndizi zinazokaribia kuiva.Kwani mmojawapo anaweza sema ni bora tugawane tu ili wakuvundika na akavundike.Kuhusu mbuyu (CCM) sifa yake kuu ni kuwa na mizizi mirefu,minene na matunda yake hukomaa kwa tabu sana na matunda yake kuanzia gamba lake la juu na mbegu zake ni ngumu na hata ukizisugua mbegu zake sakafuni tayari moto utapata.

Kuwa na chama kikongwe sio tiketi ya kushinda uchaguzi,

PNU cha Emilio Mwai Kibaki kiliundwa wiki moja kabla ya uchaguzi Nchini Kenya na kilishinda,

Didir Rastiracar wa Madagasca alishinda uchaguzii kwa chama alichokiunda ndani ya mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani kwa mapinduzi ya kiraia, tena alikuwa DJ mtaani tu ndani ya jiji la Antananarivo!

Sasa miaka ishirini ya Chadema ni mingi sana, tayari kimeshapita mapito magumu na mazuri!
 
Pengine wana ccm wanajua ama hawajui adui yao mkuu katika kilele cha kushika dola ya nchi hii tajiri huku wakaazi wake ni MAFUKARA totoro.

Tangu rais wangu kipenzi Jakaya wa Musoga ashike hatamu za uongozi mwaka mwaka 2005, chama kilianza kupoteza umaarufu ndani na nje ya nchi, niukweli uaiopingika kuwa JK alikikuta chama kikiwa katika mwangaza mkuu wa kisiasa, chama kikijinadi chenyewe, chama kikisikika hata kwa walioenda vidatu, chama kikisikika hata kwa walio peponi.

Fikiria sana mwanaccm, nini sababu za ccm kutoweka moyoni mwa Watanzania? Jiulize sana, je Jakaya ni sababu? Tafakari zaidi mwana ccm, harakati za raisi JK za kuelekea magogoni na kampeni za urais wake wa mwaka 2005 ziliratibiwa na kufanikishwa kwa fedha kharamu, nasema kharamu kwa ukweli ulio wazi,

Labda nirejea kidogo mapito ya KAGODA=CCM, MEREMETA=CCM, DEEP GREEN=CCM nk. Hayo yote makampuni yalizaliwa kwa lengo la kufanikisha ushindi wa ccm,

Hivyo rais wa Tanzania ni moja ya maadui wa ccm kushinda 2015 kwakuwa ametokana na zao la ufisadi, kamwe hawezi kunyoshea kidole mafisadi waliomuweka madarakani, zaidi atawasamehe na kuwaambia warudishe pesa hizo huku wananchi wakishindwa kuthibitisha kama kweli zimerudi au laa, Watanzania sio wajinga, wanaelewa na wataijibu ccm 2015, na jibu litakuwa na kishindo kikuu.

Baada ya kuingia madarakani Jk alimteua SWAHIBA wake Edward Lowassa kuwa Waziri Mkuu wa Nchi, Malengo ya wawili hawa na mazingira yao ilikuwa waje wapokezane kijiti, na walikula nadhiri kabisa hata kujipambanua mbele za umma kuwa urafiki wao HAWAKUKUTANA barabarani ni (urafikimaalumu)

Mwaka 2007 tofauti za wawili waliokula nadhiri maalumu ilianza kuonekana hasa baada ya kuanza kuingizana mjini, wanaiba wote mwisho wasiku mmoja anajifanya hahusiki, Lowasa alichukia sana akawa mweusi tiiiiii, yaani kwa tuliobahatika kumtizama kupitia runinga ya TBCccm pale Dodoma siku ile nae anaamua kumwaga mboga (kujiuzuru) tulifaidi kuona hasira ya waliokula nadhiri.

Tangu siku hiyo Lowassa aliamua kuingia msituni kukivuruga chama cha mapinduzi, kuivuruga serikali na kuifanya nchi isitawalike. Katika hili amefanikiwa kwani tangu mwaka 2007 alipoachia madaraka, ndipo umaarufu wa ccm ulipoanza kuporomoka kwa kasi, makundi masilahi yakaibuka, serikali ikanza sasa kuishi kwa maruhani ya akina Mwaisapile, kila kukicha linaibuka hili mara lile, rais akaugua ghafla ugonjwa wa kusafiri hataki kabisa kuishi ikulu,
Hayo yakitendeka kwa kasi Lowasa kila siku yupo misikitini na makanisani kuwania Baraka za Muumba huku ccm na serikali yake wakiweweseka na CHADEMA, eti ndicho kinafanya nchi isitawalike? Kinaongoza migomo? Kinaiyumbisha ccm? Kinaleta makundi ndani ya ccm?

USHAURI WANGU KWA JK NA CCM YAKE.

Kama kweli JK unataka kutawala kwa amani kwa mda uliosalia na kuinusuru nchi hii na machafuko ifikapo 2015, nakushauri kwa moyo mkunjufu, KAMATA Lowasa weka ndani pale Ukonga au Segerea kwa kosa la UHAINI, Likikushinda hilo mkabidhi chama kwa amani,

Hakuna njia yamkato Lowasa amejiandaa kwa vita ya kisiasa, yupo tayari nchi iingie kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ilimradi NADHIRI mliyokula pamoja inatimia.

Nawahakikishieni wanaccm, adui yenu sio CHADEMA, bali ni JAKAYA KIKWETE na EDWARD LOWASA

Mkifaulu kuwaunganisha hawa wakawa na malengo sawa hata kama hawataongea, chama kitashinda 2015,

Njia nyingine muhimu na yaharaka ni kuwanyang'anya uanachama Jakaya Kikwete na Edward Lowasa!

Muwaambie warudishe kadi zenu, wakaendelee na madili yao nje ya chama!

Kumbukeni kuwa Lowasa ana nusu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa ccm ambao wanaishi wa PESA yake.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

IN CHADEMA WE TRUST
LOWASSA akamate wa nn
 
Back
Top Bottom