Lowassa na Jakaya Kikwete ndio Maadui wakuu wa ushindi wa CCM 2015 sio CHADEMA

Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,656
Points
2,000
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,656 2,000
Pengine wana ccm wanajua ama hawajui adui yao mkuu katika kilele cha kushika dola ya nchi hii tajiri huku wakaazi wake ni MAFUKARA totoro.

Tangu rais wangu kipenzi Jakaya wa Musoga ashike hatamu za uongozi mwaka mwaka 2005, chama kilianza kupoteza umaarufu ndani na nje ya nchi, niukweli uaiopingika kuwa JK alikikuta chama kikiwa katika mwangaza mkuu wa kisiasa, chama kikijinadi chenyewe, chama kikisikika hata kwa walioenda vidatu, chama kikisikika hata kwa walio peponi.

Fikiria sana mwanaccm, nini sababu za ccm kutoweka moyoni mwa Watanzania? Jiulize sana, je Jakaya ni sababu? Tafakari zaidi mwana ccm, harakati za raisi JK za kuelekea magogoni na kampeni za urais wake wa mwaka 2005 ziliratibiwa na kufanikishwa kwa fedha kharamu, nasema kharamu kwa ukweli ulio wazi,

Labda nirejea kidogo mapito ya KAGODA=CCM, MEREMETA=CCM, DEEP GREEN=CCM nk. Hayo yote makampuni yalizaliwa kwa lengo la kufanikisha ushindi wa ccm,

Hivyo rais wa Tanzania ni moja ya maadui wa ccm kushinda 2015 kwakuwa ametokana na zao la ufisadi, kamwe hawezi kunyoshea kidole mafisadi waliomuweka madarakani, zaidi atawasamehe na kuwaambia warudishe pesa hizo huku wananchi wakishindwa kuthibitisha kama kweli zimerudi au laa, Watanzania sio wajinga, wanaelewa na wataijibu ccm 2015, na jibu litakuwa na kishindo kikuu.

Baada ya kuingia madarakani Jk alimteua SWAHIBA wake Edward Lowassa kuwa Waziri Mkuu wa Nchi, Malengo ya wawili hawa na mazingira yao ilikuwa waje wapokezane kijiti, na walikula nadhiri kabisa hata kujipambanua mbele za umma kuwa urafiki wao HAWAKUKUTANA barabarani ni (urafikimaalumu)

Mwaka 2007 tofauti za wawili waliokula nadhiri maalumu ilianza kuonekana hasa baada ya kuanza kuingizana mjini, wanaiba wote mwisho wasiku mmoja anajifanya hahusiki, Lowasa alichukia sana akawa mweusi tiiiiii, yaani kwa tuliobahatika kumtizama kupitia runinga ya TBCccm pale Dodoma siku ile nae anaamua kumwaga mboga (kujiuzuru) tulifaidi kuona hasira ya waliokula nadhiri.

Tangu siku hiyo Lowassa aliamua kuingia msituni kukivuruga chama cha mapinduzi, kuivuruga serikali na kuifanya nchi isitawalike. Katika hili amefanikiwa kwani tangu mwaka 2007 alipoachia madaraka, ndipo umaarufu wa ccm ulipoanza kuporomoka kwa kasi, makundi masilahi yakaibuka, serikali ikanza sasa kuishi kwa maruhani ya akina Mwaisapile, kila kukicha linaibuka hili mara lile, rais akaugua ghafla ugonjwa wa kusafiri hataki kabisa kuishi ikulu,
Hayo yakitendeka kwa kasi Lowasa kila siku yupo misikitini na makanisani kuwania Baraka za Muumba huku ccm na serikali yake wakiweweseka na CHADEMA, eti ndicho kinafanya nchi isitawalike? Kinaongoza migomo? Kinaiyumbisha ccm? Kinaleta makundi ndani ya ccm?USHAURI WANGU KWA JK NA CCM YAKE.

Kama kweli JK unataka kutawala kwa amani kwa mda uliosalia na kuinusuru nchi hii na machafuko ifikapo 2015, nakushauri kwa moyo mkunjufu, KAMATA Lowasa weka ndani pale Ukonga au Segerea kwa kosa la UHAINI, Likikushinda hilo mkabidhi chama kwa amani,

Hakuna njia yamkato Lowasa amejiandaa kwa vita ya kisiasa, yupo tayari nchi iingie kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ilimradi NADHIRI mliyokula pamoja inatimia.

Nawahakikishieni wanaccm, adui yenu sio CHADEMA, bali ni JAKAYA KIKWETE na EDWARD LOWASA

Mkifaulu kuwaunganisha hawa wakawa na malengo sawa hata kama hawataongea, chama kitashinda 2015,

Njia nyingine muhimu na yaharaka ni kuwanyang'anya uanachama Jakaya Kikwete na Edward Lowasa!

Muwaambie warudishe kadi zenu, wakaendelee na madili yao nje ya chama!

Kumbukeni kuwa Lowasa ana nusu ya wajumbe wa mkutano mkuu wa ccm ambao wanaishi wa PESA yake.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

IN CHADEMA WE TRUST
 
C

Che-lee

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Messages
319
Points
0
Age
57
C

Che-lee

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2011
319 0
Haitatokea hiyo kwa ccm na kwa nchi hii mkuu!
 
M

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
966
Points
250
M

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
966 250
Mkuu Yericko nyerere,
chama cha mapinduzi kilishafikia ukingoni wa mafanikia yake sasa kinashuka kwa kasi,hii ni kwasababu natural death haikwepeki kwa ccm.Kilishaondoka kwenye njia yake siku nyingi hivyo hata Kikwete na Lowasa wakiafikiana ili kujenga chama mpasuko ni dhahiri na tayari imani kwa wananchi ilishapotea siku nyingi.

Hivyo ukweli unabaki ili chama cha mapinduzi kiweze kusonga mbele lazima kiondoke madarakani ili kijipike upya na kiwe chama cha upinzani kwa muda na endapo wananchi wakiona kimekomaa kupewa majukumu basi wakipe.So wangu ushauri si tu Kikwete na Lowasa kutimiza nadhiri yao au Kikwete kumtia ndani Lowasa bali Chama cha Mapinduzi kuridhiria kwa dhati kabisa kujipanga upya.Umri pia ni tatizo kwa chama hiki kikongwe...!
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,656
Points
2,000
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,656 2,000
Haitatokea hiyo kwa ccm na kwa nchi hii mkuu!
Wataamua wao chama kife au kiendelee kuwa hai!

Pia kwa usalama wa nchi ni nivema wayatekeleze
 
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,656
Points
2,000
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,656 2,000
Mkuu Yericko nyerere,
chama cha mapinduzi kilishafikia ukingoni wa mafanikia yake sasa kinashuka kwa kasi,hii ni kwasababu natural death haikwepeki kwa ccm.Kilishaondoka kwenye njia yake siku nyingi hivyo hata Kikwete na Lowasa wakiafikiana ili kujenga chama mpasuko ni dhahiri na tayari imani kwa wananchi ilishapotea siku nyingi.

Hivyo ukweli unabaki ili chama cha mapinduzi kiweze kusonga mbele lazima kiondoke madarakani ili kijipike upya na kiwe chama cha upinzani kwa muda na endapo wananchi wakiona kimekomaa kupewa majukumu basi wakipe.So wangu ushauri si tu Kikwete na Lowasa kutimiza nadhiri yao au Kikwete kumtia ndani Lowasa bali Chama cha Mapinduzi kuridhiria kwa dhati kabisa kujipanga upya.Umri pia ni tatizo kwa chama hiki kikongwe...!
Ushauri mzuri sana, hofu yangu ni wahusika wenyewe, je wataupokea?

Wao wanaamini kuwa chama chao kimejihuisha baada ya kufanya uchaguzi wake mwezi jana!
 
Last edited by a moderator:
M

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
966
Points
250
M

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
966 250
Ushauri mzuri sana, hofu yangu ni wahusika wenyewe, je wataupokea?

Wao wanaamini kuwa chama chao kimejihuisha baada ya kufanya uchaguzi wake mwezi jana!
Kwa asili ya viongozi wa chama cha mapinduzi kwao wao kwa kila njia ya kuendelea kuwa madarakani ndio chaguo lao la kwanza hivyo hata kama mtu akija na ushauri mahususi kwa lengo la kujenga zaidi future ya chama nje ya kuwa na dola kwao ni kejeli na dhihaka kubwa.So vyovyote wawazavyo wamefika mwisho wao na hakuna njia ya mkato kwao bali kutoka nje ya mfumo.
 
M

mwinukai

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Messages
1,448
Points
1,225
Age
35
M

mwinukai

JF-Expert Member
Joined May 3, 2011
1,448 1,225
Kupata wasimamizi wapya wa mirathi, si kumfufua marehemu au kurudisha uhai wa marehemu bali ni kuendelea kugawana na mali.

Wana CCM, wamepata wasimimizi wapya wa mirathi hivyo hawapaswi kuwa na matumaini ya marehemu kufufuka bali waendelee kugawana na mali za marehemu
 
F

Fursa Pesa

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2012
Messages
2,619
Points
2,000
F

Fursa Pesa

JF-Expert Member
Joined May 30, 2012
2,619 2,000
Wewe ni greater thinker kwelix2,lakini kuna wakati 1+1 jibu si mbili bali ni moja tu.Kwa mantiki hiyo ebu jaribu kutazama na upande wa pili wa shillingi (CDM) kukoje,maana tunaweza kuwa tunapoteza muda kujadili masuala ambayo ni makubwa kuliko uwezo wetu wa kufikiri na hata tukipata majibu hayatusaidii sanax2 ni kutujaza chuki,uhasama na kufifisha ndoto/malengo yatu ya msingi.samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
 
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
7,053
Points
1,225
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
7,053 1,225
CCM imepoteza mvuto kwa wananchi kutokana na kushindwa kutatua issues mbalimbali kama mfumuko wa bei, elimu duni, umaskini uliokithiri, upendeleo kwa wawekezaji wa kigeni, ufisadi, ukosefu wa ajira, nk. Haya ndio yameipotezea CCM umaarufu na wala sio conflict ya JK na Lowassa.
 
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,656
Points
2,000
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,656 2,000
Kupata wasimamizi wapya wa mirathi, si kumfufua marehemu au kurudisha uhai wa marehemu bali ni kuendelea kugawana na mali.

Wana CCM, wamepata wasimimizi wapya wa mirathi hivyo hawapaswi kuwa na matumaini ya marehemu kufufuka bali waendelee kugawana na mali za marehemu
Hii nimeipenda mkuu, umeona mbali sana,
 
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,656
Points
2,000
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,656 2,000
Wewe ni greater thinker kwelix2,lakini kuna wakati 1+1 jibu si mbili bali ni moja tu.Kwa mantiki hiyo ebu jaribu kutazama na upande wa pili wa shillingi (CDM) kukoje,maana tunaweza kuwa tunapoteza muda kujadili masuala ambayo ni makubwa kuliko uwezo wetu wa kufikiri na hata tukipata majibu hayatusaidii sanax2 ni kutujaza chuki,uhasama na kufifisha ndoto/malengo yatu ya msingi.samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
Mimi ni mdadisi wa kimalenga ya sasa!

Ninapozitazama siasa zetu kwakiwango kikubwa itikadi yangu huificha!

Kwa macho yangu mawili naiona Chadema kama chama mbadala wa ccm, na kinajipambanua kwa sera za kitaifa, kina sura ya utaifa, na kipo tayari kushika dola!
 
F

Fursa Pesa

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2012
Messages
2,619
Points
2,000
F

Fursa Pesa

JF-Expert Member
Joined May 30, 2012
2,619 2,000
Mimi ni mdadisi wa kimalenga ya sasa!

Ninapozitazama siasa zetu kwakiwango kikubwa itikadi yangu huificha!

Kwa macho yangu mawili naiona Chadema kama chama mbadala wa ccm, na kinajipambanua kwa sera za kitaifa, kina sura ya utaifa, na kipo tayari kushika dola!

Mkuu samahani kwa usumbufu,hivi nini tofauti ya mbuyu na mgomba?
 
C

Che-lee

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Messages
319
Points
0
Age
57
C

Che-lee

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2011
319 0
Kupata wasimamizi wapya wa mirathi, si kumfufua marehemu au kurudisha uhai wa marehemu bali ni kuendelea kugawana na mali.

Wana CCM, wamepata wasimimizi wapya wa mirathi hivyo hawapaswi kuwa na matumaini ya marehemu kufufuka bali waendelee kugawana na mali za marehemu
Umeona mbali sana ndugu, kweli wewe ni GT

Lakini katika siasa huwa inaelezwa kuwa chama kinapofanya mabadiliko ya uongozi ni kuwa kinajaribu kurejesha uhai wa chama hicho!
 
C

Che-lee

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Messages
319
Points
0
Age
57
C

Che-lee

JF-Expert Member
Joined Jun 10, 2011
319 0
Mimi ni mdadisi wa kimalenga ya sasa!

Ninapozitazama siasa zetu kwakiwango kikubwa itikadi yangu huificha!

Kwa macho yangu mawili naiona Chadema kama chama mbadala wa ccm, na kinajipambanua kwa sera za kitaifa, kina sura ya utaifa, na kipo tayari kushika dola!
Chadema hakijaiva kiasi cha kushika nchi hii,

Slaa hawezi kutawala pekee yake kwakuwa wengine wote ni wahuni tu hawafai hata udc
 
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,656
Points
2,000
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,656 2,000
Chadema hakijaiva kiasi cha kushika nchi hii,

Slaa hawezi kutawala pekee yake kwakuwa wengine wote ni wahuni tu hawafai hata udc
Pole sana mkuu, usilolijua ni kama usiku wa giza,

Chadema imekomaa na ipo tayari kushika dola mkuu! Ina watu muhimu wakuweza kufanya kila idara
 
brasy coco

brasy coco

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2012
Messages
1,457
Points
2,000
brasy coco

brasy coco

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2012
1,457 2,000
Yan mwendo ulishaonekana mbaya pale Jk aliposhindwa kuwachkulia hatua mafisadi waliokula pesa za Umma hii ndo ilipunguza Imani kwa Rais huyu kipenzi cha Watanzania wengi,Jk alizidi kushusha Heshma yake aliposema mafisadi warudishe pesa, wakati Raia mwngne apofanya uharifu mfano kuiba basi inangaliwa sheria inasema nini na yule mtu ufungwa Jela lakini Jk alishindwa hili.
Jk angepata heshma kama angesema mnatakiwa kurudisha Pesa na mtapokea kifungo cha miaka 30 jela kwa kula pesa za Umma wananchi wangepiga Makofi.....Jk ni rahisi pekee aliyependwa na Wananchi wengi bila kuangalia Chama chake na kumchagua kama yeye, Lakini Jk ametuvunja moyo wananchi wake katika kushughulikia Mafisadi.
Nakubali yapo mema mengi ameyatenda Jk lakini hili la wizi amelishindwa ndomana wananchi wanaona kuwa naye ni mchafu sababu KILICHO KICHAFU HAKIWEZI KUMSAFISHA MCHAFU MWENZAKE BALI KISAFI NDO KINAMSAFISHA MCHAFU JK FANYA CHAGUO GUMU CHUKUA HATUA UTAPATA HESHMA KUBWA.
 
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
42,245
Points
2,000
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
42,245 2,000
Vipi ile thread yako uliyoanzisha kuwa mpasukuo mkubwa unakuja ndani ya CCM. imefikia wapi?
 
Forum statistics

Threads 1,284,758
Members 494,236
Posts 30,838,875
Top