Lowassa na Jakaya Kikwete ndio Maadui wakuu wa ushindi wa CCM 2015 sio CHADEMA

Yan mwendo ulishaonekana mbaya pale Jk aliposhindwa kuwachkulia hatua mafisadi waliokula pesa za Umma hii ndo ilipunguza Imani kwa Rais huyu kipenzi cha Watanzania wengi,Jk alizidi kushusha Heshma yake aliposema mafisadi warudishe pesa, wakati Raia mwngne apofanya uharifu mfano kuiba basi inangaliwa sheria inasema nini na yule mtu ufungwa Jela lakini Jk alishindwa hili.
Jk angepata heshma kama angesema mnatakiwa kurudisha Pesa na mtapokea kifungo cha miaka 30 jela kwa kula pesa za Umma wananchi wangepiga Makofi.....Jk ni rahisi pekee aliyependwa na Wananchi wengi bila kuangalia Chama chake na kumchagua kama yeye, Lakini Jk ametuvunja moyo wananchi wake katika kushughulikia Mafisadi.
Nakubali yapo mema mengi ameyatenda Jk lakini hili la wizi amelishindwa ndomana wananchi wanaona kuwa naye ni mchafu sababu KILICHO KICHAFU HAKIWEZI KUMSAFISHA MCHAFU MWENZAKE BALI KISAFI NDO KINAMSAFISHA MCHAFU JK FANYA CHAGUO GUMU CHUKUA HATUA UTAPATA HESHMA KUBWA.

Umenena vema mkuu! Wadadisi tunajionea na tunazidi kuomba kifo kitakatifu kitimie
 
Naona umeamua kujiliwaza na kujifariji chama hakina hata makatibu wakuu mikoani mnawaza urais.

Kwani kwamjibu wa sheria za usajili wa vyama vya siasa na sheria ya uchaguzi, kuna kipengele kinachosema nilazima chama kiwe na makatibu mikoa yote tz ndipo kianze kugombea urais?
 
Huu ni mwendelezo mkuu, kwani huoni kuwa chama chenu kinapasuka?

Mkuu mpasuko upo Chadema kati ya Dr Slaa na Zitto Kabwe watu wa Kaskazini wameapa watafanya kila mbinu wamuangushe Zitto...na Zitto kasema lazima agombee urais kupitia Chadema.

Mkuu vipi wewe upo kambi ya nani?
 
Swali lako halina mlingano wa ccm na chadema!

Labda ungesema ipi tofauti kati ya mgomba na mpapai?
Hao ndio umeenda mbali kabisa kwani mfano wako ni sawa na CHADEMA NA CUF moja inatoa ndizi na nyingine .......
Mbuyu hata ukiwa km5O unaonekana na kwenye ardhi umejishika kabisa Yericko Nyerere leo ndio kanifurahisha kwa kuona mbali hasa nanukuu
USHAURI WANGU KWA JK NA CCM YAKE.
Kama kweli JK unataka kutawala kwa amani kwa mda uliosalia na kuinusuru nchi hii na machafuko ifikapo 2015, nakushauri kwa moyo mkunjufu, KAMATA Lowasa weka ndani pale Ukonga au Segerea kwa kosa la UHAINI, Likikushinda hilo mkabidhi chama kwa amani,
Hakuna njia yamkato Lowasa amejiandaa kwa vita ya kisiasa, yupo tayari nchi iingie kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ilimradi NADHIRI mliyokula pamoja inatimia.
Nawahakikishieni wanaccm, adui yenu sio CHADEMA, bali ni JAKAYA KIKWETE na EDWARD LOWASA

Ni kwamba kesho katika Medani za siasa Star tv msikilize Katibu waUVCCM atalizungumzia hilo la mbio za kuwania URAIS kwa mtu anayetoa mafweza jinsi akiukosa atakuwaje, na hata Kinana keshatahadharisha wanaokimbilia URAIS wajitoe
 
Last edited by a moderator:
Naona umeamua kujiliwaza na kujifariji chama hakina hata makatibu wakuu mikoani mnawaza urais.
Hii inaonesha unavyowaza ndani ya box, kama wana CCM wenzako. Kama hao makatibu wakuu wa CCM wangekuwa wanaumuhimu wowote akina KINANA na NAPE wangezunguka kuuza sura?.
 
Mkuu mpasuko upo Chadema kati ya Dr Slaa na Zitto Kabwe watu wa Kaskazini wameapa watafanya kila mbinu wamuangushe Zitto...na Zitto kasema lazima agombee urais kupitia Chadema.

Mkuu vipi wewe upo kambi ya nani?

Nakuhakikishia Chadema hakuna mpasuko, Zitto Slaa,Mbowe na wanachama wote wapo njia moja sasa kuelekea magogoni,

Chama kitaamua nani ashike bendera sio Zitto wa Slaa!

Hizo kambi unazozitaja tushazivunja na hazina madhara hata kwa mjumbe wa nyumba kumi tu!

CCM ndiko dhahama ilipo, jk anambania kwa nguvu zote Laigwanani asikanyage magogoni, huku Laigwanani kakishika chama kila upande!

JK sasa anategemea kitengo chake cha propaganda (TISS) huku mwenzie Lowasa kaishika CCM yote,

Sasa subiri utaona maajabu mapema kabla 2015
 
Hii inaonesha unavyowaza ndani ya box, kama wana CCM wenzako. Kama hao makatibu wakuu wa CCM wangekuwa wanaumuhimu wowote akina KINANA na NAPE wangezunguka kuuza sura?.

Huo ndio ukweli ambao kijana Ritz na wenzake hawauoni
 
In chadema we trust, halafu jk na EL wakiunganishwa basi ccm itashinda 2015... Tushike lipi? BTW mada yako inachangamsha
 
Hao ndio umeenda mbali kabisa kwani mfano wako ni sawa na CHADEMA NA CUF moja inatoa ndizi na nyingine .......
Mbuyu hata ukiwa km5O unaonekana na kwenye ardhi umejishika kabisa Yericko Nyerere leo ndio kanifurahisha kwa kuona mbali hasa nanukuu
USHAURI WANGU KWA JK NA CCM YAKE.
Kama kweli JK unataka kutawala kwa amani kwa mda uliosalia na kuinusuru nchi hii na machafuko ifikapo 2015, nakushauri kwa moyo mkunjufu, KAMATA Lowasa weka ndani pale Ukonga au Segerea kwa kosa la UHAINI, Likikushinda hilo mkabidhi chama kwa amani,
Hakuna njia yamkato Lowasa amejiandaa kwa vita ya kisiasa, yupo tayari nchi iingie kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ilimradi NADHIRI mliyokula pamoja inatimia.
Nawahakikishieni wanaccm, adui yenu sio CHADEMA, bali ni JAKAYA KIKWETE na EDWARD LOWASA

Ni kwamba kesho katika Medani za siasa Star tv msikilize Katibu waUVCCM atalizungumzia hilo la mbio za kuwania URAIS kwa mtu anayetoa mafweza jinsi akiukosa atakuwaje, na hata Kinana keshatahadharisha wanaokimbilia URAIS wajitoe

Sisi tunawashauri kama wadadisi wa mambo tu, lakini kama watadharau majuto ni mjukuu
 
Last edited by a moderator:
Wakati nasoma hisabati mwalimu wangu Mr Matley alisema if A=B,B=C then A=C

If the above is true then Mchawi wenu ni BW MKAPA ambaye yote hayo yalitokea chini yake.

Kwa sasa chama haikitakwa kumsaka mchawi kwakuwa alishawaloga na yeye akatokomea na kuwaachia ugonjwa,

Chama kipambane na ugonjwa ambao ni Lowasa na JK
 
Kwa sasa chama haikitakwa kumsaka mchawi kwakuwa alishawaloga na yeye akatokomea na kuwaachia ugonjwa,

Chama kipambana na ugonjwa ambao ni Lowasa na JK

Well yasingetokea hayo JK angetumia muda mwingi kuleta maendeleo kuliko kupambana na kashfa hizi za Radar,EPA,Ndege nk. Sasa unaposema yamepita nakuwa sikuelewi. Mshukuru rais wako JK aliyekuwezesha angalau ukajua madudu ya serikali kuliko hao ambao walikuaminisha mambo yanaenda vizuri kumbe huku chini nchi inatafunwa na wachache. Hata ukiangalia kushuka kwa Popularity ya JK kumechangiwa na haya haya makashfa ambayo yalitokea yeye akiwa waziri wa mambo ya nje.

Nikukumbushe kwamba kipindi cha Nyerere kilikuwa kipindi cha taabu na mashaka kiuchumi kwa wananchi wengi maana hata kuiona shati ilikuwa tabu lakini wananchi waliowengi waliona hali hii kama ya kawaida tu. Bahati nzuri kipindi hiki kulikuwa na uwajibikaji kidogo. Hayo ya uwajibikaji tulikuja kuyajua alipoingia mzee ruksa lakini pia tuliona matatizo ya hali mbaya ya uchumi ya Nyerere. Japo kipindi cha Mwinyi kilionekana kama cha neema nyingi lakini alipoingia Mkapa ndio tukagundua tatizo kubwa la mfumuko wa bei lililokuwa linatuandama.Alipoingia Kikwete tukapata kufahamu Ufisadi wa hali ya juu uliotokea kipindi cha Mkapa; EPA,Ndege,Radar n.k . Kwa sasa hamna yeyote anayejua ufisadi ,uzuri au ubaya wa serikali hii ya awamu ya nne hadi hapo JK akishaondoka tutakapopata benchmark ya awamu inayokuja.
 
Mkuu mpasuko upo Chadema kati ya Dr Slaa na Zitto Kabwe watu wa Kaskazini wameapa watafanya kila mbinu wamuangushe Zitto...na Zitto kasema lazima agombee urais kupitia Chadema.

Mkuu vipi wewe upo kambi ya nani?

Tena ni mkubwa!
 
Kwanini usiwaache tu walale ivo ivo??

Maradhi yao sisi tunayafurahia na hatutaki hata kuwahimiza dawa wala kumuona daktari ili wafe kifo chema kabisa

hawafai hawa,,waache tu wajifie zao mkuu

wabaki wa nin??tena sio heko kwa hawa kubakia kuwa wapinzani,hawa wafutike moja kwa moja wabakie tuh kwenye jumba la makumbushoo
 
Back
Top Bottom