Lowassa mbioni kuinusuru Hoteli ya KKT, Corridor Spring

Lowassa mbioni kuinusuru Hoteli ya KKT, Corridor Spring

Wana bodi!!
Hatimaye lile jembe la kaskazini Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli mh. Edward Lowassa aingilia kati mgogoro wa hotel ya KKKT corridor spring isiuzwe.

Hili limejitokeza baada ya hotel hiyo kukopa fedha katika benki ya CRDB na kushindwa kulipa,ina sadikika hotel hiyo miaka ya nyuma ilichukua kiasi kikubwa cha hela na kushindwa kurudisha na kupelekea deni kufikia zaidi ya bilioni moja.

Jana mh. Lowassa alifnya kikao kikubwa na wafanyabiashara wakubwa kuhakikisha wanainusuru hoteli hiyo ambayo iko mbioni kuuzwa.

Katika kikao hicho ambacho kiliongozwa na mh. Lowassa walikubaliana watafanya harambee kubwa ya kufunga mwaka ambayo itakuwa ya kihistoria lengo ni kuhakikisha fedha hizo zinapatikana kuhakikisha hoteli inarudi mikononi mwa KKKT jimbo la Arusha.

Wakazi wa Arusha wamepokea kwa shangwe kubwa na kumpongeza kwa nguvu zote mh Edward Lowassa,wakazi hao wa Arusha hatimaye wamefikia maamuzi ya kutenga siku kwaajili ya kumwombea mbunge wa Monduli ili Mungu aendelee kumpa moyo wa huruma.

Wakaz hao wanasema walishakata tamaa na hawakuwa tena na matumaini kama hoteli ingebaki tena mikononi mwa KKKT.

Wanasema kiasi cha fedha ambacho hotel hiyo ilikuwa ikidaiwa kutokna na mkpo walio chukuwa hakuna mtu mwingine ambaye angeweza kuinusuru hoteli zaidi ya Lowassa kwani amekuwa na ushawishi mkubwa sana wa kushawishi wafanyabishara wakubwa kuchangia michango mbali mbali ya kimaendeleo.

Hii hotel inaaiwa zaidi ya 10 billion bro sio bilion 1, tumeshaendesha harambee za ndani kwa dayosisi mzima zaidi mara 2 kwa kila mkristo kutoa shs 30,000/= kwa dayosisi mzima, mie mwenyewe nimechangia sana tu, kiukweli kanisani nako kuna ufisadi tena mwingi tu na ninajua hata kama sie tutaunyamazia watoto wetu wa vizazi vijavyo watakuja kuwapiga wachungaji na maaskofu mawe! halafu nasikitika kwa system ya kkkt askofu akimess up hawezi kuwajibishwa, ingekuwa ni roma askofu lazima alishawajibishwa!! ila all in all makanisa tena yote kuna ufisadi mwing sana unafanyika
 
Juzi tu tulilipa riba peke yake milioni 600, bado awamu nyingine.

Hoteli ya kanisa hairuhusu wazinzi, walevi, wavuta sigara kulala pale, na hakuna lounge kwa ajili ya kupata vinywaji vikali ndiyo maana hoteli haifanyi vizuri.

USHAURI WANGU;
Hoteli ya Corridor Spring iuzwe, fedha zitakazopatikana zielekezwe kujenga shule au hospitali ya kanisa
Mungi umesema neno.
Kanisa limeingia kufanya biashara ambayo wao wenyewe wamejiwekea barrier ktk mambo fulani.
Walishashauriwa muda mrefu waikodishe kwa makampuni yanayo-deal na mambo ya hotel kama Serena n.k hawakutaka.

Uongozi wa kanisa ulichokuwa unafanya ni kufisadi kila kilichokuwa kinafanyika ktk hoteli hiyo Karyongi akiwa kinara mkuu.

Kwa wanaomjua meneja mkenya aliyeletwa na Karyongi watakuwa wanaelewa ufisadi uliokuwa unafanyika.

Waumini wameshaambiwa mara nyingi tu wachange na wakachanga lkn bado deni haliishi.
 
Last edited by a moderator:
Poor management why mnajiingiza kwny biashara msizoweza kizisimamia na kuanza kutembeza bakuri la ombaomba. It's much better kufocus ktk ujenzi wa matawi mengine ya kanisa na kuvuna waumini wengi zaidi ili kueneza injiri mana hiyo ndo main theme ya kanisa kuliko kujiingiza kwny biashara kwa manufaa ya wachache na kuleta aibu na usumbufu kwa waumini.!!
si afadhali hao wanaojaribu wanapata hasara,muda mwingne wakirudia tena wanafaulu kwasabu washajuwa jinsi ya manage,kuliko nyie mmebakia kununuwa suruali na kuzikata na vibarakashee
 
Wakati mwingine Viongozi wakiLUTHERI wanawafanya waumini wao km CCM inavyosulubisha waTZ nakuwaona maBWEGE! kuna Usharika DAR ilikuwa inajengwa HOSTEL watu 2kahoji Waumini watanufaikaje nahiyo HOSTEL? hakukuwa na majibu nnavyokwambia HOSTEL ina DENI hata haiujulikani latalipwaje! Miradi mingi yakiLUTHERI cjui haifanyiwi uchambuzi wakutosha kabla yakuanzishwa au vp DAR kuna RADIO UPENDO lkn kila mwaka Sharika zinaichangia ss hv wamefungua BANK ctashangaa waumini wakiambiwa wachangie uendeshaj fuly uBABAISHAJ
 
si afadhali hao wanaojaribu wanapata hasara,muda mwingne wakirudia tena wanafaulu kwasabu washajuwa jinsi ya manage,kuliko nyie mmebakia kununuwa suruali na kuzikata na vibarakashee

Ndg unakosea kusema namna hiyo KKKT ni 1 ya Dhehebu lenye waumini wengi na wataalam kwenye Sector mbali mbali kuniambia kuwa wanajaribu cdhani km ni sahihi! Tatizo wanaonufaika ni wachache na mradi ukitaka kufilisiwa wataletwa waHUBIRI mbali mbali kuja kufundisha UTOAJI hii nikuwadharau waumini!
 
Juzi tu tulilipa riba peke yake milioni 600, bado awamu nyingine.

Hoteli ya kanisa hairuhusu wazinzi, walevi, wavuta sigara kulala pale, na hakuna lounge kwa ajili ya kupata vinywaji vikali ndiyo maana hoteli haifanyi vizuri.

USHAURI WANGU;
Hoteli ya Corridor Spring iuzwe, fedha zitakazopatikana zielekezwe kujenga shule au hospitali ya kanisa

wajenge chuo kabisa
 
Wana bodi!!
Hatimaye lile jembe la kaskazini Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli mh. Edward Lowassa aingilia kati mgogoro wa hotel ya KKKT corridor spring isiuzwe.

.
Rekebisha hapo kwenye red tafadhali.
 
Wewe Bw.Karyongi Bw.John Njoroge yupo wapi? Karyongi_1.jpg
 
ila kama kweli watamalza den la hyo hotel,wahakikishe viongoz wa dini wanakaa mbali na hoteli hii,watakuw wanapew taarifa tu
 
Lowassa ana haki kabisa ya kufanya hivyo;
yeye anajua utamu wa maeneo ya kanisa hasa hilo hilo la kkkt.
 
Pesa ya kujenga hoteli watoe waumini (na zilipatikana pesa za kutosha floor 6), njama ya kukopa aianzishe yeye na askofu Rafiki yake, wale wao pesa iliyokopwa leo hii mtu huyo huyo eti anashangiliwa kuwa kaiokoa hoteli isiuzwe!!! Kweli aliewaloga Watanzania kafa!

Mnamshangilia mwizi???!!!!!???
 
Hakika umesomeka na umenena Mungi.

Juzi tu tulilipa riba peke yake milioni 600, bado awamu nyingine.

Hoteli ya kanisa hairuhusu wazinzi, walevi, wavuta sigara kulala pale, na hakuna lounge kwa ajili ya kupata vinywaji vikali ndiyo maana hoteli haifanyi vizuri.

USHAURI WANGU;
Hoteli ya Corridor Spring iuzwe, fedha zitakazopatikana zielekezwe kujenga shule au hospitali ya kanisa
 
Last edited by a moderator:
Pesa ya kujenga hoteli watoe waumini (na zilipatikana pesa za kutosha floor 6), njama ya kukopa aianzishe yeye na askofu Rafiki yake, wale wao pesa iliyokopwa leo hii mtu huyo huyo eti anashangiliwa kuwa kaiokoa hoteli isiuzwe!!! Kweli aliewaloga Watanzania kafa!

Mnamshangilia mwizi???!!!!!???

Nina wasiwasi kama ww utakuwa siyo kariongi anayetuhumiwa kuifilisi hotel ya corridor spring,bas kariongi ni baba yako
 
Back
Top Bottom