HOMOSAPIEN
JF-Expert Member
- Mar 31, 2011
- 745
- 273
Hii hoteli angeichukua kabisa au ainunue kabisa huyo mheshimiwa sijawahi kuona kanisa linafanya biashara ya hoteli,toka lini kanisa likafanya biashara? tunachohitaji waumini ni mashule,zahanati lau kama hoteli basi iwe ni hosteli na nyumba za ibada inashangaza makanisa mengine hasa masaini wanasali chini ya miti au katika vyumba vya madarasa wakati wachungaji wao wanakwenda kula kuku corridor spring,hivi kuna upako kweli hapa?haiingii akilini kabisa eti kanisa linafanya biashara kujiongezea kipato hivi ni waumini ndiyo waliamua? au wachungaji wao?hivi uamsho umeishia wapi?zamani kulikuwa na shughuli ya uamsho waumini waliweza kujenga makanisa ya gharama kubwa tena kwa kuchangia fedha nyingi sana eti siku hizi wanajenga hoteli jamani dini inafanya biashara najiuliza nakosa majibu. hata mwenyezi mungu alisema ya kaisari mpe kaisari ya mungu mpe mungu hii hoteli ni ya kaisari si ya kimungu.