Lowassa, Maalim Seif waishika Zanzibar!

Lowassa, Maalim Seif waishika Zanzibar!

Nina wasiwasi wewe sio raia wa Tanzania! VITA unaijua wewe?? Unafikiri utajamba tena vita ikitokea? Huyo LOWASSA ana cheo gani cha kutoa tamko kwenye Nchi hii? Sisi tunasubiri Uchaguzi Machi 20 na mshindi atapatikana kihalali!!
Ni kweli watanzania hawajui vita hivyo nina wasiwasi wewe unaejua vita sio mtanzania, yawezekana umeexperience some where!! sasa uko TZ unaenjoy "kuj..." nchini mwetu. !! Nahisi siku ya uchaguzi utaja....sana tu!
 
Naona unaandika ukitamani machafuko yatokee na unadhani yakitokea mtakuwa mmeikomoa CCM!!!!
 
Naona unaandika ukitamani machafuko yatokee na unadhani yakitokea mtakuwa mmeikomoa CCM!!!!
Wewe ndo umemuelewa hivyo.
Mi nimemuelewa kuwa JF wasipuuze alerts zinazoletwa,maana yeye alileta alerts ikapuuzwa ila leo gazet limeripot
 
Nina wasiwasi wewe sio raia wa Tanzania! VITA unaijua wewe?? Unafikiri utajamba tena vita ikitokea? Huyo LOWASSA ana cheo gani cha kutoa tamko kwenye Nchi hii? Sisi tunasubiri Uchaguzi Machi 20 na mshindi atapatikana kihalali!!
Huu unaoludiwa ni batili ule wa mwanzo ndio ulikuwa halali.. Ccm ni wapuuzi sana huu ubabe wao una mwisho..
 
Naona unaandika ukitamani machafuko yatokee na unadhani yakitokea mtakuwa mmeikomoa CCM!!!!
ivi mkuu anaetamani machafuko ni nani kati ya huyu mtoa mada na yule anaefuta matokeo halali kirahisi tu kisa kala mweleka?
 
Naona unaandika ukitamani machafuko yatokee na unadhani yakitokea mtakuwa mmeikomoa CCM!!!!
Kwa nini serikali ya ccm haifanyi kazi kwa kufanya uchunguzi kwanza wa kina kubaini maovu ndani ya jamii bali wanatawala kwa hofu nyingi hawatumii na kuzingatia utawala wa sheria jambo hili ni baya sana..subirini
 
""moja ya faida ni kuheshimiana""
ccm wanatengeneza maandalizi ya kupigana sisi kwa sisi na si kuleta umoja na amani miongoni mwetu, uchaguzi ukishafanyika kwa amani na mmoja akaonekana ameshinda apewe haki yake yakuchaguliwa na wananchi wake lakini wao ccm hawataki wengine washinde.

mfano mzuri juzijuzi tu kulikuwa na uchaguzi wa Mameya ktk mikoa ya Kinondoni na Ilala ndugu hawa ccm walilazimisha kuleta maamluki kutoka zanzibar waje kupiga kura bila kufuata sheria za nchi ni jambo la aibu na fedheha kwa chama kinachojinasibu kwa watu kuwa ni chama kinachothamini utawala wa sheria sio kweli... uchaguzi zanzibar ulifanyika kwa utulivu mkubwa hakuna mtu wala kiongozi aliyelalamikia wakati zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura likiendelea lakini ccm baada ya kuona kwamba kulikuwa na mwelekeo wakushindwa wakasitisha kutangaza makusudi kupitia kwa mwenyekit wa uchaguzi...hiiiiii aibu na uogo wakushindwa.. ukitangaza kurudia uchaguzi march 20, 2016 Zanzibar ni uongo mkubwa.

mnadiriki kutudanganya waziwazi kwamba wawakilishi ambao wameapishwa dodoma waliotokea Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu kumalizika nakushinda wao ni halali na tena miongoni mwao wameteuliwa kuwa mawaziri na manaibu kwa nini viongozi wa ccm mnaisigina katibu ambayo mmeapa kuilinda hapo munalinda katiba ipi? ambayo sheria zake hamzifuati? ninyi ccm ni waongo wakubwa na wanafiki...
Hata Mh.Raisi Magufuli alihubiri kwa nguvu zake zote wakati wa kampeni juu ya amani ya taifa..sasa amani aliyokuwa anaihubiri kwenye majukwaa ya kampeni ilikuwa ni ya kupatia kura? leo hii sijasikia kauli yoyote amabyo Raisi amezungumzia suala la mkwamo wa kisiasa wa Zanzibar? nashangaa,..nimegundua kuwa ccm ni ile ile na watu ni wale wale hakuna mabadiliko ya kweli bali ni uongo ule ule uliodumu kwa miaka mingi katika taifa letu tulivu... ccm mnahusika na uharibifu wa amani ya taifa....
 
Katika tabia mbovu ambayo inabidi ipigwe vita kwa nguvu zote ni ile ya mtu kupenda mabaya yatokee nchini mwake. Hakuna usaliti mbaya kama ule unaofanywa dhidi ya nchi ambayo Baba yako na Mama yako wamezaliwa, nchi unayoita nyumbani. Mtu akiwa na utimamu wa akili zake anamuombea mabaya Diamond ashindwe kupata tuzo huko nje, anamuombea mabaya Mbwana Samatta asipate tuzo ya Afrika, halafu ni mtanzania kama huyo anayemuombea mabaya. Mtanzania anafurahia habari mbaya za mwenzake, hili pepo sijui limetoka wapi. Mnigeria akimkuta mwenzake nje ya nchi lazima atambeba asiadhirike, lakini kule Sweden miaka ya nyuma alikuwepo mtanzania aliyefanya kazi ya kuwachoma watanzania wenzake kwa na mamlaka za serikali. Roho mbaya inatangulizwa mbele badala ya utu. Sijui huu ukosefu wa upendo kiasi hiki umetoka wapi, labda wataalam wa saikolojia wanaweza kuwa na majibu.
 
Haiwi haiwi uvumivu sasa umefikia mwisho ,Polisi wa Muungano wapo njiani wakisaidia juhudi za mwizi kuendeleza wizi kwa maana sasa wananchi kila mmoja kwa upande wake anatoka njiani kifua mbele kupinga hatua za CCM kutaka uchaguzi urudiwe kwa kuwa ilipigwa na chini ,wanachi wakati wa kulazimishwa kuekewa utawala wasio uchagua umepitwa na wakati.

Polisi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapo njiani kupambana na wananchi wenye hasira kali ,muda huu ni mabomu kila kona na pia inasemekana zimesikika risasi za moto.
Kama huamini mpigie simu aliepo Zanzibar.
sisi kina gogo la shamba tulishaadharisha hayo mapema ila kuna mwana ccm mmoja alinishambulia sana nikamuambia aweke kumbukumbu ya taadhari yangu ili yatakapotokea akumbuke,sasa dalili zimeanza
 
Una uhakika ? Sasa nakuambia kuwa watu wameamua kufunga maduka na bomu limerushwa ndani ya nyumba ya mtu ,mwenye nyumba kawatokea wakasema wamelirusha kwa bahati mbaya ,na mabomu yanaendelea ,polisi wanasema wanafukuza jamaa eti sio waTz na jana kumeshushwa majeshi kibao ,ila watu wakiamua kufa basi hio sio dawa mtawauwa wengi tu.
Ila ulizia kati ya Mlandege na raha leo kuna nini hivi sasa !

Come on sisi tu watanganyika ndo tumebakia mazoba wa kugeuzwa hovyo kama chapati.
 
Nina wasiwasi wewe sio raia wa Tanzania! VITA unaijua wewe?? Unafikiri utajamba tena vita ikitokea? Huyo LOWASSA ana cheo gani cha kutoa tamko kwenye Nchi hii? Sisi tunasubiri Uchaguzi Machi 20 na mshindi atapatikana kihalali!!
Mimi mwenyewe naitamani maana mmezidi kututishia haya na vije kama vyaja.
 
Katika tabia mbovu ambayo inabidi ipigwe vita kwa nguvu zote ni ile ya mtu kupenda mabaya yatokee nchini mwake. Hakuna usaliti mbaya kama ule unaofanywa dhidi ya nchi ambayo Baba yako na Mama yako wamezaliwa, nchi unayoita nyumbani. Mtu akiwa na utimamu wa akili zake anamuombea mabaya Diamond ashindwe kupata tuzo huko nje, anamuombea mabaya Mbwana Samatta asipate tuzo ya Afrika, halafu ni mtanzania kama huyo anayemuombea mabaya. Mtanzania anafurahia habari mbaya za mwenzake, hili pepo sijui limetoka wapi. Mnigeria akimkuta mwenzake nje ya nchi lazima atambeba asiadhirike, lakini kule Sweden miaka ya nyuma alikuwepo mtanzania aliyefanya kazi ya kuwachoma watanzania wenzake kwa na mamlaka za serikali. Roho mbaya inatangulizwa mbele badala ya utu. Sijui huu ukosefu wa upendo kiasi hiki umetoka wapi, labda wataalam wa saikolojia wanaweza kuwa na majibu.

Haihitaji mtaalamu wa saikolojia kujua chuki miongozi mwa watanzania inapandwa na CCM na serikali yao kwa kulea na kuchochea dhuluma katika taifa.
Wakiwatendea wananchi haki wala hautakaa usikie hizi vurugu na chuki zikiendelea.
Ni hayo tu.
 
Mimi mwenyewe naitamani maana mmezidi kututishia haya na vije kama vyaja.
That is the spirit!!!
We don't show them any remorse, we take them by the throat and play their game better than them.

Maalim atangazwe rais wa Zanzibar.
Na Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, kwa hivyo watanzania wote tuna deni la kulipa Zanzibar.
Binafsi niko tayari kulilipa kwa damu yangu.

CCM amegeuka kuwa mkoloni mweusi mwenye tabia zote za kikoloni tulizopambana nazo.
CCM amekuwa eti mbaguzi wa rangi leo sijui CCM anataka rangi gani.
CCM akizidiwa kwenye ulingo wa siasa anakimbilia udini na ukabila.

Magufuli anasema anahangaika na majipu yaliyozalishwa na CCM ila nyumba yenyewe ya majipu ni CCM.

CCM ikiondoka madarakani ndio mwisho wa majipu!

Ni Maalim na Zanzibar au tukose wote.
 
Haihitaji mtaalamu wa saikolojia kujua chuki miongozi mwa watanzania inapandwa na CCM na serikali yao kwa kulea na kuchochea dhuluma katika taifa.
Wakiwatendea wananchi haki wala hautakaa usikie hizi vurugu na chuki zikiendelea.
Ni hayo tu.
CCM ina nguvu na ushawishi ndani ya Tanzania, nimeongelea mentality ya kitanzania kwa ujumla. Tabia ya mtu kufurahia kushindwa kwa mwenzake, tabia ya mtu kuwa tayari kumsaliti msanii au mwanamichezo wa Tanzania kwa faida ya yule wa Nigeria. Naongelea tabia ya wadau wa yanga na simba kuwa tayari kuzisaidia timu za nje eti ili kumkomoa mtani wa jadi!. Naongelea mambo mengi kwa wakati mmoja, naongelea kutopendana kwetu. CCM inayo madhambi yake lakini yapo mengine ambayo wataalam wa akili wanaweza kutusaidia katika kuyatatua.
 
Back
Top Bottom