Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu na kupata msg nyingi za hapa na pale zilizokuwa zikilenga kaniuliza mustakabali wa Zanzibar baada ya kutangazwa kurejewa kwa uchaguzi nimekuwa nikifuatilia kwa karibu nini kinaendelea na nimepata taarifa zifuatazo:
1. Kutangazwa kurejewa kwa uchaguzi kumetokana na mpango wa kutaka kuendeleza uwepo wa Dr. Shein madarakani kwani Jumatatu ya tarehe 25/01/2016 Ndio mwisho wa kuongezewa muda na Ccm wana uhakika kwamba uchaguzi hauwezi kurudiwa, hivyo inaweza kuwasaidia Wahafidhina wa Chama Tawala kubaki madarakani.
2. Wanasheria wazalendo wa Zanzibar wakiongozwa na aliekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serekali, Mr. Othman Masoud wapo kwenye hatua za mwisho za kupeleka mashtaka yetu ya kubakwa Kwa democracy kwenye mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.
3. Wanasheria wa Ukawa watapeleka hoja maalum kwenye bunge litakaloanza Jumanne tarehe 26 ili kupinga uamuzi wa kurudiwa kwa uchaguzi na ikishindikana watengue na uchaguzi wa Muungano jambo ambalo litamgusa Mh. Rais Magufuli..
Kwa hayo machache tutegemee jambo lipo insha Allah.
Ahsanteni sana..
By Mzalendo Kindaki ndaki