Lowassa, Maalim Seif waishika Zanzibar!

Lowassa, Maalim Seif waishika Zanzibar!

Bunge la muungano kazi yake inapofikia swala la zanzibar kazi yao ni kushugulikia maeneo tu yale yaliyomo ndani ya katiba kwenye vipengele vya mambo ya muungano.Hata wabunge watokao Zanzibar kazi yao ni kuleta vile vihusuvyo mambo ya muungano kwenye bunge.Visivyohusu muungano vinapelekwa baraza la wawakilishi au serikali ya Zanzibar.Uchaguzi wa Raisi wa Zanzibar ni jambo ambalo liko nje kikatiba.Bunge la muungano lisithubutu kujadili hilo swala labda liwe limeletwa na na kuridhiwa na serikali ya Zanzibar na baraza la wawakilishi..

Seif kama anataka tuvunje katiba ili tuingilie mambo ya ndani ya nchi ya Zanzibar imekula kwake.Zanzibar ni nchi kamili yenye hadhi kabisa ya nch waende wakayamalize kwao hatutaki watushirikishe bara aende zake huko na Lowasa wake.

Spika awe mkali kwa UKAWA wasilete mambo yasiyo ya muungano ndani ya bunge la muungano .Kama UKAWA watazira hoja ikizimwa na kuamua kutoka na watoke.Katiba ya nchi lazima izingatiwe.Ningekuwa karibu UKAWA wakiamua kususa na kutoka ningewakimbiza na nondo ili wawahi kutoka

Wabunge wa UKAWA na LOWASA na MAALIM seif wamechoka hivi hata katiba hawasomi? Wamechanganyikiwa.HALAFU WOTE VIBABU MVI KIBAO.kUPISHA VIJANA HAWATAKI
 
sasa tufanyeje mkuu ? tupe plan B
Mlitakiwa mwende mahakamani kama mnaona mna sababu za msingi za kisheria kupinga uchaguzi kwa lolote.Matamko yenu tumeyachoka.,Kila siku maneno Jecha KACHEMKA KWA NINI MSIENDE mahakamani kutwa mko mabarabarani kutoa matamko kama vichaa.
Mahakama ziko Zanzibar hamuendi kutwa mnashinda Tanzania bara.safari hii hatubebi mzanzibari mjibebe wenyewe ile si ni nchi kamili yenye madaraka kamili .Jibebeni wenyewe
 
War is one place where there is glory enough for everyone.
Zanzibaris have nothing to fear exept fear itself.

Zanzibar politics has come to a place where civil disobedience is a civic right, even a duty for everyone who waship democracy.

Njia muafaka ilikuwa wapeleke maswala mahakamani hawakwenda.Hiyo ya kutishia nyau haisaidii kitu.Na wao wanakumbuka kile kilichowakuta 2001.Wanajua wakilianzisha watalinywa zima zima nadhani wapemba wote wanalijua hilo.
 
Vijana wa ccm.Acheni kujidhalilisha hapa kwa vitusi vyenu.Kuna njia nyingi za kutatua migogoro. Jiulize kabla hujatoa kitusi chako kama zote zimefwatwa na kushindikana.
 
Zanzibar ilitakiwa waje wasuluhishi kutoka nje ya Tanzania ili waweke mambo sawa,si swala la kutangaza tarehe ya uchaguzi wakati ulifuta kwa sababu ulishindwa.
 
Zanzibar ilitakiwa waje wasuluhishi kutoka nje ya Tanzania ili waweke mambo sawa,si swala la kutangaza tarehe ya uchaguzi wakati ulifuta kwa sababu ulishindwa.
Walitakiwa CUF waende mahakamani si kubwabwaja.Mahakama ndi chombo sahihi ambacho kingeweka mambo sawa hizo zingine ni sarakasi tu za kisiasa za Akina seif na akina lowasa
 
Wangeenda mahakama ipi wakati katiba ni mbovu???
Katiba ipi unayoongelea?

Ule uchaguzi unasimamiwa na katiba ya Zanzibar sio ya muungano.Kwenye katiba ya muungano swala la uchaguzi wa Zanzibar si la muungano.

Kuna mahakama za zanzibar wanaye kuanzia mwanasheria mkuu hadi jaji mkuu wa nchi huru ya Zanzibar huko ndiko wangepeleka
 
paul alex namfananisha na nyuki wa mashineni.huwa anatoa matamko makali saana...lakini baadae anakaa kimya.Rejea kipindi cha kifo cha mawazo.paul alex punguza jazba bro.
 
Nadhani hujanielewa matokeo yake ndiyo hayo ya kuandika ukurasa mzima kwa maelezo mafupi naelewa ulivyofikiria wewe sivyo ninavyomaanisha bunge lao si ndiyo baraza kama nilivyotaja mamlaka kamili waliyo nayo wapeleke huo mswaada kwenye baraza lao
 
paul alex namfananisha na nyuki wa mashineni.huwa anatoa matamko makali saana...lakini baadae anakaa kimya.Rejea kipindi cha kifo cha mawazo.paul alex punguza jazba bro.
Mawazo aliuawa Geita bro
Na mimi niko Geita bro
Ondoa shaka!
 
Zanzibar. Siku moja baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) kuitangaza Machi 20 kuwa siku ya marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, mgombea urais, Maalim Seif Sharif Hamad na Edward Lowassa leo wanakutana na wabunge wote kutoka vyama vinavyounda Ukawa kutoa “tamko zito” litakalotoa mwelekeo wa hali halisi ya kisiasa visiwani humo.
CUF, ambayo inapinga kurudiwa huko kwa uchaguzi, nayo imepanga kufanya vikao vyake vya juu mapema wiki ijayo kuweka msimamo wake kuhusu tangazo hilo.
Wakati hayo yakiendelea, mabomu ya machozi jana yalilipuliwa kwenye maeneo tofauti ya Zanzibar wakati askari wa Jeshi la Polisi wakitawanya watu waliokuwa wamekaa kwenye vikundi, kwa kuhofia kuwa wanaweza kutumia mwanya huo kufanya vurugu.
Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alitangaza juzi kuwa marudio ya uchaguzi hayatatanguliwa na kampeni za wagombea wa nafasi za urais, uwakilishi na udiwani na wala hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya wagombea.
Bado vyama vya upinzani havijatoa tamko kuhusu uamuzi huo wa ZEC, lakini viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa; Chadema, CUF, NLD na NCCR Mageuzi wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa African Dream.
Habari zilizolifikia gazeti zinaeleza kuwa awali katika kikao hicho Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ulipanga kujadili mkwamo wa kisiasa na jinsi ya kupata suluhu, lakini baada ya ZEC kutangazaa kurudiwa kwa uchaguzi huo, ajenda imebadilika na sasa umoja huo utatoa msimamo wake wa mwisho kuhusu Zanzibar.
Msemaji wa Lowassa, Aboubakar Liongo na Ismail Jussa walithibitisha viongozi hao kutua Dodoma jana jioni tayari kwa kikao hicho ambacho kitaanza asubuhi.
Habari zaidi zinaeleza kuwa awali, Maalim Seif na Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu na ambaye mwaka jana aligombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, watakutana na viongozi wakuu wa Ukawa na baadaye na wabunge wote na kisha kutoa maazimio.
“Ni maazimio ambayo yanalenga kueleza ukweli kuhusu kinachotaka kufanyika Zanzibar. Yatakuwa maazimio mazito,” alisema mpashaji habari wetu.
Januari 20, wabunge wa Ukawa walifanya kikao cha ndani kwenye ukumbi wa Pius Msekwa uliopo viwanja vya Bunge kuhusu hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na kutangaziwa kuwa wataelezwa msimamo wa umoja huo leo.
“Watapewa mrejesho wa kikao cha mwisho kati ya Maalim Seif na (Rais wa Zanzibar) Dk Ali Mohamed Shein. (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman) Mbowe na mwanasheria wa Chadema (Tundu Lissu) nao wataeleza masuala mbalimbali kuhusu Zanzibar,” alisema mtoaji habari huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema licha ya kuwapo kwa mazungumzo hayo, msimamo wa Ukawa na CUF wa kupinga uchaguzi huo kurudiwa, upo palepale.
“Kesho (leo) tunazungumza kuhusu Zanzibar. Pamoja na mambo mengine tutatafakari hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na nchi kwa ujumla na baada ya hapo tutatoa maazimio yetu,” alisema Mbatia.
Alisema lengo la kikao hicho ni kuelezana kwa kina lilipo tatizo, kupewa taarifa na takwimu sahihi.
“Hatuko tayari kurudiwa kwa uchaguzi Zanzibar, Watanzania lazima wakumbuke kuwa ukitenda haki, amani ndipo hupatikana,” alisema.
Alisema kutokana na kufutwa kwa uchaguzi huo, Tanzania imetengwa pamoja na kunyimwa fedha za maendeleo kutoka mataifa makubwa.
“Ole wao wanaofanya mambo haya. Yakisababisha umwagaji damu yatawagharimu na wapo watakaokamatwa na kufikishwa Mahakama ya Kimataifa kwa kusababisha mauaji,” alisema Mbatia.
“Suala la Zanzibar hatukubaliani nalo kwa sababu ukishawekwa utaratibu, halafu ukauvuruga ni fujo. Na duniani kote dola na taasisi huundwa kwa njia ya maridhiano,” alisema.
“Mwaka 1995 na 2000 mauaji yalitokea Zanzibar lakini mwaka 2010 hayakutokea kwa sababu ya maridhiano ya CCM na CUF.
“Leo hii Zanzibar wanarudi kulekule kwa kuwa CCM wasiposhinda inakuwa nongwa. Wanataka wao ndiyo washinde tu na wanadhani wao ndiyo wenye fikra na haki tu. Kama ni hivyo kwa nini mfumo wa demokrasia uwepo?”
Wakati mkutano huo ukiandaliwa, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa CUF, Jussa, ambaye amelielezea tamko la Jecha kuwa halizingatii Katiba wala sheria.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Jussa amelielezea tamko hilo kuwa “la kihuni lisilozingatia Katiba wala sheria” na kwamba vikao vya juu vya chama hicho vitafanyika mapema wiki ijayo kufanya uamuzi.
“Kamati ya Utendaji ya Taifa itakutana tarehe 27 Januari, 2016 na kufuatiwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokutana Alhamisi, tarehe 28 Januari, 2016,” inaeleza taarifa hiyo iliyotolewa na Jussa akiongeza kuwa vikao hivyo vitafanyika kwenye ofisi za makao makuu ya CUF zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo inawataka wananchi ambao kinasema “waliikataa CCM kwa kishindo Oktoba 25”, kuendelea kutunza amani na kuwa watulivu “katika kipindi hiki kigumu na kusubiri maamuzi ya chama chao wanachokiamini”.
Akitangaza tarehe ya kurudia uchaguzi huo juzi kupitia kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ambako pia Januari 28, 2015 alitangaza kuufuta, Jussa alisema kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.
Alisema uchaguzi huo utarudiwa ndani ya siku 90. Juhudi za kutafuta suluhisho la kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huo zilizomshirikisha Dk Shein na Maalim Seif zimegonga mwamba baada ya kufanya vikao tisa bila kuafikiana.
Tayari Maalim Seif ameshajitoa kwenye mazungumzo hayo yaliyohusisha vikao tisa.
Mitaani Zanzibar
Mapema jana hali ilikuwa shwari mitaani wakati watu wakiendelea na shughuli zao za kila siku, lakini ilibadilika jioni wakati polisi walipotumia mabomu ya machozi kutawanya watu waliokuwa wamekusanyika nje ya nyumba zao wakinywa kahawa kwa maelezo kuwa mikusanyiko hairuhusiwi.
Maeneo hayo ni pamoja na Kundemba, Kwa Haji Tumbo na Kinuni na watu kadhaa wanadaiwa kupigwa kabla ya kutawanywa.
Wakizungumza na gazeti hili, mashuhuda wa tukio hilo walisema hakukuwa na sababu yoyote ya polisi kufanya jambo hilo kwa kuwa ni kawaida vijana na wazee kukusanyika maeneo hayo kwa ajili ya kunywa kahawa na kucheza keramu.
Eneo la Haji Tumbo, kijana mmoja alitolewa ndani ya duka la simu na kupigwa kisha polisi kuondoka naye pamoja na pikipiki yake aina ya Vespa.
“Wamekuja wakaingia kwenye duka la simu kwanza wakapiga mabomu kama mlivyosikia ule mlio, kisha wakamchukua. Lakini kwanza wamempiga,” alisema Mahmoud Ali, mkazi wa eneo hilo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mukadam Khamis Mkadam hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo.
Wakati wanaingia kwenye uchaguzi Oktoba 2015, CUF walijua ZEC ipo. Walitambua mwenyekiti wa ZEC Jecha Salimu Jecha yupo. Walitambua pia madaraka yake katika kuandaa daftari la wapiga kura hadi kutangaza matokeo ya uchaguzi. Namini kama Jecha Mwenyekiti wa ZEC angalimtangaza Maalim Seif kuwa mshindi matokeo hayo wangeyaheshimu bila shaka yoyote. Shida inakuja pale Jecha anapoenda kinyume na matarajio ya wana CUF. Hapo sasa Jecha anaonekana kuwa ni CCM. Ni lini Jecha amekuwa CCM? Kama walijua hivyo tangu mwanzo kwa nini hawakumkataa?
Mahakamani kuna haki ya kumkataa hakimu kama huna imani kama haki itatendeka. Uchaguzi urudiwe, ndiyo lakini Jecha maadam ametiliwa shaka na CUF, atafutwe Mwenyekiti mwingine neutral mwenye historia ya kutenda haki bila upendeleo wowote. Kukataa kushiriki uchaguzi kutawafanya CUF pia wasieleweke. Shida siyo uchaguzi, shida ni Mwenyekiti anayedhaniwa kuwa anapokea maelekezo kutoka CCM. Tanzania haijaishiwa watu waaminifu, inao wengi lukuki. Kama CCM watang'ang'ani awe huyo huyo Jecha, hapo pana shida na kama CUF watakataa kushiriki uchaguzi hata baada ya kumtoa Jecha napo hapo patakuwa na shida.
Si busara hata kidogo nchi kuingia kwenye mgogoro wa kisasa kwa sababu ya vikundi viwili CCM na CUF tu. Kuna watanzania wengi tusi wanachama wa vyama hivi viwli, kwa nini waumie kwa sababu ya vikundi vwili tu tena wanachama wao hawafiki hata nusu ya watanzania wote? Nashangaa watu wazima kama akina James Mbatia wanazunguzia vurugu kana kwamba ni jambo rahisi, wanazungumzia watu kwenda The Hegue kwa gharama ya maisha ya watu, watanzania waliozoea amani tangu enzi za baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kuna watu hawawezi kuishi bila migogoro. Mbatia alifukuzwa Chuo kikuu sababu ya migomo, Seif Sharif Hamad zaid ya nuru karne anapambana tangu akiwa kijana hadi leo ni mzee bado anapambana tu.
CCM pia wamekuwa wakilazimisha ushind hata waliposhindwa. Tanzania ni nchi ya demokrasia siyo ya kisultani. Ukikubali kuwa nchiya kidemokrasia lazima ukubali matokeo upende usipende lazima uongozwe kwa misingi y kidemokrasia na siyo kwa matakwa yao. Dr. Shein siyo demokrasia. Dmokrasia ndiyo iliyomuwepa pale kama inamtoa, atoke tu. Mtu au chama hakiwezi kuwa kikubwa kuliko demokrasia kwa sababu wote wameikuta demokrasia ipo siyo wao wameiweka demokrasia
 
Mlitakiwa mwende mahakamani kama mnaona mna sababu za msingi za kisheria kupinga uchaguzi kwa lolote.Matamko yenu tumeyachoka.,Kila siku maneno Jecha KACHEMKA KWA NINI MSIENDE mahakamani kutwa mko mabarabarani kutoa matamko kama vichaa.
Mahakama ziko Zanzibar hamuendi kutwa mnashinda Tanzania bara.safari hii hatubebi mzanzibari mjibebe wenyewe ile si ni nchi kamili yenye madaraka kamili .Jibebeni wenyewe
kama zanzibar kuna mahakama mbona uamsho wameshitakiwa Tanganyika ?
 
Ngoja tuone watasema nini ila hata taahira anajua CCM wapo tayari damu imwagike kuliko kuachia madaraka Zanzibar...
 
Mara nyingi linapokuja swala la uchaguzi CCM hupenda kukimbilia kwenye ukingo wa mto wa vita wakiamini majeshi ya ulinzi na usalama ya Tanzania yako kwaajili ya maslahi yao.

Mimi nataka CCM wajue kwamba unapopenda kucheza pembeni ya ukingo wa mto basi ujue kuna hatari ya kuangukia mtoni.

Hii ni risk ambayo CCM wameamua kuichukua kwa kuamini kama watanzania wataogopeshwa na haka kamchezo kao ka kurushia watu mawe na kukimbilia nyuma ya wanajeshi na FFU.
Lazima tuwaonyeshe CCM kama na sisi tunaweza kuchukua hii risk ya kucheza kwenye ukingo wa mto wa vita.
Basi kama wote tukidondokea itakuwa kwa faida ya demokrasia.

But we must show them that we are ready to play brinkmanship.That is the only way to deal with them
 
Jana niliandika habari ya Zanzibar ,nilikuwa nazungumza na mtu na ukasikika mshindo nje alitoka na kunipasha na hapo hapo kurusha JF,wakaruka watu hapa na kudai chanzo na wapi na wapi ,jamani wengine huwa hatuokoti okoti ,ona sasa magazeti yameandika kitu ambacho newz alati tuliiweka hapa JF ,hatukurupuki kwa habari zinazohusu maisha ya mtu na watu na wananchi kwa ujumla. Inamaana hata kama tumevamiwa na nchi jirani na ulichonacho ni Jf wakati unatumia simu za satalite ,wacheni zarau.
Haya gazeti hili hapa limeandika hali ya jana jioni Zanzibar shindaneni nalo basi !


By Waandishi Wetu
Sunday, January 24, 2016
Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha kuitangaza Machi 20 kuwa siku ya marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, mgombea urais, Maalim Seif Sharif Hamad na Edward Lowassa leo wanakutana na wabunge wote kutoka vyama vinavyounda Ukawa kutoa “tamko zito” litakalotoa mwelekeo wa hali halisi ya kisiasa Zanzibar.
CUF, ambayo inapinga kurudiwa huko kwa uchaguzi, nayo imepanga kufanya vikao vyake vya juu mapema wiki ijayo kuweka msimamo wake kuhusu tangazo hilo.
Wakati hayo yakiendelea, mabomu ya machozi jana yalilipuliwa kwenye maeneo tofauti ya Zanzibar wakati askari wa Jeshi la Polisi wakitawanya watu waliokuwa wamekaa kwenye vikundi, kwa kuhofia kuwa wanaweza kutumia mwanya huo kufanya vurugu.

Mitaani Zanzibar
Mapema jana hali ilikuwa shwari katika mitaa ya Zanzibar, huku watu wakiendelea na shughuli zao za kawaida, lakini hali hiyo ilibadilika jioni wakati polisi walipotumia mabomu ya machozi kutawanya watu waliokuwa wamekunsanyika wakinywa kahawa kwa maelezo kuwa mikusanyiko hairuhusiwi.
Mitaa iliyokumbwa na kasheshe hiyo ya polisi ni pamoja na Kundemba, Kwa Haji-Tumbo na Kinuni, ambako watu kadhaa wanadaiwa kupigwa kabla ya polisi kuwatawanya.
Wakizungumza na gazeti hili, watu waliyoshuhudia tukio hilo walisema hakukuwa na sababu yoyote polisi kuchukua hatua hizo kwa kuwa ni kawaida vijana na wazee kukusanyika maeneo hayo kwa ajili ya kunywa kahawa na kucheza keram.
Eneo la Kwa Haji-Tumbo, kijana mmoja alitolewa ndani ya duka la simu na kupigwa kisha polisi kuondoka naye pamoja na pikipiki yake aina ya Vespa.
“Wamekuja wakaingia kwenye duka la simu kwanza wakapiga mabomu kama mlivyosikia ule mlio, kisha wakamchukua. Lakini kwanza wamempiga,” alisema Mahmoud Ali, mkazi wa eneo hilo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini/Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam hakupatikana jana kuzungumzia matukio hayo.
Imeandikwa na Fidelis Butahe, Hassan Ali, Kalunde Jamal na Salma Said
 
Back
Top Bottom