Lowassa kuwa waziri mambo ya nje!?

Status
Not open for further replies.
Kama alijichagua au kujiteua katika nafasi hiyo kamwe hataondoka...

LOL! Huyo ni Mwanamtandao wa kudumu :) kwenda kokote kule ni demotion with exception ya kumrithi Mizengo Pinda au kutinga Ikulu.
 
kama huyu jamaa atarudi itabidi jamiiforums tuwe wakimbizi kwani atatutesa sana nasikia anachuki ya simba jike ukimgusa mwanawe.
 
Hii haijakaa vizuri ila kwa staili anayotumia mh kuiongoza hii nchi ya wadanganyika lolote linaweza kufanyika na sitashangaa kusikia maandamano nchi nzima ya wana CCM kupongeza hatau mh handsome boy.
 
Ni vibaya sana kutetea mafisadi! Lowasa ni moja ya mafisadi waliokwisha julikana na kuwekwa wazi hata hivyo ukweli unabaki palepale kwamba Kikwete hawezi kufanya kazi bila Lowasa. Toka Lowasa ajiuzuru kasi ya utendaji wa Serikali umepungua sana, Pinda hajaweza kabisa kutosheleza nafasi ya PM. Pinda amekuwa mwongeaji kama Kikwete tofauti na Lowasa ambaye alikuwa mtendaji. My opinion ni kumwondoa Kikwete kwasababu hawezi kazi na siyo kumwingiza Lowasa Serikalini, tutachekesha sana.

Zimwi la uwezo wa Lowasa litabaki likiigesa serikali ya JK kwa muda wote wa uongozi wa awamu hii.Pamoja na yote yanayosemwa na yaliotokea bado Lowasa atbaki kukumbukwa kwa uwezo wake wa pekee wa kufatilia ujenzi wa nchi ya Tanzania.Pinda atabaki kuwa ni waziri ambae siyo aggressive na hawezi kubadili jambo lolote.Kwanza ni muoga na hawezi kusimamia mabadiliko yoyote.hana ajenda yoyote ya ujenzi wa nchi yake.baada ya miaka mingi ukweli huu utatoka wazi na hakuna atakaebisha juu ya ukweli huu....tatizo la Pinda kubwa ni kuwa anaogopa kufanya maamuzi kwa kuwa maamuzi makubwa muda mwingine yanweza kuwa na makosa na anajua Rais wake hawezi kumlinda pale atakapotereza kiutendaji.Bora awe tu kimya kama hayupo kama Sumaye alivyokuwa.
 
Zimwi la uwezo wa Lowasa litabaki likiigesa serikali ya JK kwa muda wote wa uongozi wa awamu hii.Pamoja na yote yanayosemwa na yaliotokea bado Lowasa atbaki kukumbukwa kwa uwezo wake wa pekee wa kufatilia ujenzi wa nchi ya Tanzania.Pinda atabaki kuwa ni waziri ambae siyo aggressive na hawezi kubadili jambo lolote.Kwanza ni muoga na hawezi kusimamia mabadiliko yoyote.hana ajenda yoyote ya ujenzi wa nchi yake.baada ya miaka mingi ukweli huu utatoka wazi na hakuna atakaebisha juu ya ukweli huu....tatizo la Pinda kubwa ni kuwa anaogopa kufanya maamuzi kwa kuwa maamuzi makubwa muda mwingine yanweza kuwa na makosa na anajua Rais wake hawezi kumlinda pale atakapotereza kiutendaji.Bora awe tu kimya kama hayupo kama Sumaye alivyokuwa.

Kalamu yako imeteleza....

Recent aggressive investment and looking at aggriculture ni agenda ya Serikali lakini pia yenye msukumo mkubwa sana wa Mh. Waziri Mkuu Pinda.

Lakini pamoja na yote lazima tukubali kwamba Lowassa alikuwa analeta mabadiliko makubwa ya utendaji kwa speed... we shall remember him for this.
 
Lakini kumbukeni kuwa mbereko aliyo tumia rais kumbeba Lowasa imesha toboka akimbeba tena si atandoka pwaaaaaaaaaaaa!kisha akaumia kabisa na yeye mwenyewe JK...
 
Fisadi Mtoto,Kasheshe,Kichuguu,Bubu..,...

..nadhani tungewapima hawa Mawaziri Wakuu kwa kuangalia wali-accomplish kitu gani ktk uongozi wao.

..Mkapa na Sumaye wana mapungufu yao, lakini hii miradi[mkukuta,mkurabati,..] yote inayotekelezwa na awamu ya nne ilitokana na juhudi na vision ya hao wawili.
 
Kwani kuna tatizo gani? Uongozi wa awamu ya nne umeshathibitisha kuwa ni 'recycling' tu. Arejeshwe, asirejeshwe, sidhani kama kutakuwa na mabadiliko yoyote. wale wanaomsifia kuwa alikuwa mchapakazi, labda wanakijua kingine cha ajabu ambacho kilifanywa ambacho sisi wengine hatukifahamu
 
Haki sawa,

Mkuu unachekesha sana, naomba uache utani wa namna hii, tena haipendezi mkuu, haya umeyatoa wapi? ama ndiyo mkuu umenong'onezwa na Membe?


sasa unabisha?????? hakuna atakae fanya kitu chochote.... alishaanza kupima geji zetu kwa kumsifia kwenye hotuba yake na kutpguswa kabisa na PInda...ubabe ubabe tuu na hakuna yeyote atakae bisha
 
Bado tu hawajamaliza mazingaombwe yao?

Mpita Njia!

Mtu/Watu huwa hawamalizi kazi wanayoifanya au waliyoajiriwa nayo hadi wafukuzwe au waamue kuacha kazi hiyo.

kwa serikali ya JK (mzee wa kutalii nje ya nchi) yeye hawezi kuacha mazingaombwe kwa sababu ndiyo kazi iliyomuweka madarakani, hakuna ha zaidi. mwenzako anasogeza siku tu ziende 2010 apite tena iwe kwa halali au laa ili amalizie mazingaombwe yake na kuachia kijiti kwa mwigizaji mzwenzake.
 
Hakuna cha ajabu kama wezi wa EPA wanaendelea kuabudiwa. Ukisikiliza hotuba ya JK katika kipengele cha Richmond na ukisikiliza taarifa ya Pinda kuhusu Richmond na siku moja baada ya Pinda kampeni kamambe zikaanza, Monduli kwa kuzindua mradi wa maji kwa mwembwe nyingi na jopo la waandishi toka Dar, kabla ya kupambwa tena na sherehe za kutawazwa kuwa kiongozi wa jadi.

Lakini huu ndio mwanguko mwingine wa serikali ya Kikwete. Kwa nadharia na sanaa kubwa itaonekana kuna mafanikio makubwa na wananchi watashangilia kama wanavyoshangilia na kuandamana kwa fedha za EPE kupelekwa TIB (zilikoibwa za Inport Support) huku ndani ya mioyo ya waandamanaji na wananchi kukiwa na kutu kubwa.

Tusishangae kusikia lolote kwa serikali ya sasa, kwa kuwa wanaendelea kutuzuga na sisi tunanung'unika pembeni bila kuchukua hatua kama walivyochukua hatua wanafunzi wa Dar kuandamana kwa ongezeko la senti hamsini. Tusubiri vijana hao wa shule watakapoingia barabarani huku wazazi wao tukishangilia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom