NilikuWa Geneva last time ...banker mmoja akaniambia namna watoto wa Mobuto...na hata serikali ya Zaire[congo] wanavyopata taabu ku claim pesa za baba yao....wa swiss wametuibia sana ...jaamaa aliniambia pesa zilizopo kwenye mabenki yao ambazo beneficiaries wanashindwa kuzi claim ni billions of usd.....beleave me....!!! nikamuuliza ..je kuna viongozi wa kitanzania waliokufa wakaacha pesa kwenye coffers zao ...aakacheka!!!...nikamkumbuka marehemu Amir Jamal......
WA Swiss ni wasiri sana ...lakini mlolongo wa kudai pesa pale kiongozi au mwenye pesa anapofariki ni mgumu sana....akaunti nyingi za siri hazina majina wala picha ,zina password ....na funny questions and answers.....na kila mwenye secret account anakuwa assigned secret banker wa kumtafuta wakati anapotaka kufanya transaction....beleave me mapesa ya kina sadam,king hussein,bokkasas...na wote mnaowajuwa yako huko....waliopinduliwa hawakuweza ku claim pesa zao......kuna viongozi wachache ambao pale walipoona afya zinakuwa mgogoro waliweza kuhamishia pesa kwenye aakaunti za watoto wao au kuwapa access....lakini wengi wameliwa jamani!!!
Ndio maana viongozi wajanja kama kina Moi,jaramogi,kenyatta etc wakaona huu ni ujinga....wakawekeza pesa zao zote ....Kenya.......
Nawahakikishieni watanzania value ya corruption tangu uhuru ingetumika kama stimulus kwenye nchi yetu .....tungeona maajabu kabisa.....siongei haya kwa kuwa naunga mkono UFISADI....bali naongea hali halisi...wazee!!!
Jiulizeni pesa za EPA tumefaidika nini ? hazijarudi....kama ilivyoahiwa na yale majizi yamezikimbizia DUBAI ,,,...kununua majumba....tumefaidika nini??..
Umenishawishi kuchangia hoja hii.SISHANGILII UFISADI NAAMINI KUTAFUTA KWA NJIA HALALI ZISIZO NA MAKOVU YA DHULUMA,CHUKI,VISASI NA JAKAMOYO LA MAISHA SIKU ZAKO ZOTE DUNIANI.
Mara ZOTE LINAPOKUJA SWALA LA UTAJIRI WA MTU YOYOTE KWANGU UTAJIRI WAKE HUO SINA TATIZO,TATIZO LANGU UWA NI MBINU NA NJIA ZILIZOTUMIKA KUPATA UTAJIRI HUO,KWA KUWA KUWA TAJIRI SIO DHAMBI,BALI DHAMBI HIKO KWENYE NAMNA UTAJIRI HUO ULIVYOPATIKANA, JE NI KWA NJIA HALALI AU NJIA HARAMU.
HAKIKA TULIPOFIKA KAMA TAIFA NATAMANI SANA HAYA YAFANYIKE:
1: Kuundwe timu ya watu wenye UFAHAMU MKUBWA sana juu ya maswala ya UCHUMI, FEDHA, SHERIA, BIASHARA NA PSYCHOLOGY NA WAZEE WENYE KUHESHIMKA KWENYE JAMII, ambao kazi yao kuu ni kuakikisha kuwa watajibu maswali ya MASWALA LA UTAJIRI wa baadhi ya Watanzania na WAGENI WALIOKO TANZANIA [Wazungu, Waasia, Waarabu,Wasomali na wengineo ambao ni wakazi ndani ya Tanzania],ambao Watanzania wanahuoji na kutaka kufahamu juu ya UTAJIRI wao huo na hivyo basi suruhisho la majibu ya maswali ya Watanzania yapatikane, juu ya nguvu ya utajiri wao huo umepatikana kwa njia zipi, halali au halamu ?una ukubwa gani yani kutambua thamani ya Properties na Assets zake, zote?
2: Kupitia Task Force hiyo ya yatakayopatikana huko liwe jibu la TAIFA kupitia
RECONCILIATION COMMITTEE.Kwa kuwa tulipofika kama TAIFA hakika HAKUNA JIBU LAHISI LA UTATUZI HUO.Yaliyomo ndani ya maswali ya Utajiri wa baadhi ya Wanasiasa, Watendaji wa Serikali na wenzi wao yani maswahiba wao,imekuwa ni gonjwa hatari ambalo hakika tuendako kama hakuna matayarisho hakika itakuwa ni kuni mbichi kuchochewa ili kinachotakiwa kuwaka kitokeee.Ila kuna siku kuni hizo mbichi zilizoko jikoni zitakauka uko uko kwenye mafiga na moto huo utawaka kwa kasi kubwa.
3: Inajulikana kuwa kuna kuna baadhi Matajiri hao wachache wameinvest Tanzania lakini kuna wengi wamezihifadhi Pesa hizo Nje ya Nchi kama Dubai, Uswis, Uk na Kwingineko. Hakika Aliyeinvest Tanzania na Aliyeinvest nje ya Tanzania wataitaji Reconciliation tofauti sana sana. NA hatua za kudeal nao zinapaswa kuwa tofauti sana.Yatakayojili hapo ni muhimu sana na yatakayo lisaidia Taifa kuwa na kioo chema kwa kizazi kinachokuwa kwa sasa na kizazi kijacho mbele ya safari, [VISION YA WATANZANIA JUU YA SWALA LA UTAJIRI].
4: Kupitia taarifa zitakazopatikana Nchi itapata VISION na mbinu za kuunda POLICY, ambazo zitajenga na kuibua MAPOKEZI ya kulea jamii ya wanasisa, watendaji na raia wa kawaida,ikibidi Miiko mipya juu ya Wanasiasa, Watendaji wa Serikali, na Wananchi na Wageni, juu ya bidii binafsi za kujiletea mafanikio ambayo uzaa UTAJIRI.Vision hizo ambazo zitazaa Sera [POLICY] ambazo zitakuwa ni chachu za kudhibi na kupanua wigo wa umma kujitafutia mafanikio [UTAJIRI] kwa kuwa utajiri wa mtu mmoja mmoja ndio kwa ujumla uunda utajiri wa TAIFA.Lakini utajari pasipo miiko basi ni vurugu ambayo ndiyo tunayopambana nayo kama TAIFA kwa sasa.
5: Na kupitia Reconciliation Committee hiyo Wananchi watapata pia kupata viwango na ukubwa wa UTAJIRI, wa baadhi ya Watajiri.Na kupitia hapo SErikali ITATAMBUA RASMI mchango rasmi wa MATAJIRI ambao UTAJIRI wao UMEPATIKANA KWA NJIA HALALI, hivyo wao na KUTHAMINIWA RASMI na KUPEWA NISHANI RASMI ZA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAMA NAO NI SEHEMU YA VIONGOZI WALIOCHANGIA KWENYE NCHI KAMA VIONGOZI WA SERIKALI WAPEWAVYO, NISHANI YA UONGOZI ULIOTUKUKA NAO MATAJIRI WAPATE KWA KUTOA MCHANGO WA MAFANIKIO KWENYE SEKTA BINAFSI YA BIASHARA NA UCHUMI WA TAIFA.Na Taifa kuwatumia matajiri halali waliotambulika rasmi na Serikali katika kampeni rasmi za KITAIFA , kama vita dhidi ya Ukimwi, Umaskini, Magonjwa, Afya, Elimu, Ustawi wa Jamii, Makazi, Ajira, n.k.
6: Watakaobainika katika RECONCILIATION kuwa UTAJIRI WAO ni kutokana na njia sizizo sahihi, basi NENO RECONCILIATION ndio wakati wake kupewa nafasi KUFANYA KAZI katika njia sahihi.Zikiwemo mbinu kama waamue kusurrender mali zao zote kwenye umma, zikiwemo pesa walizo hifadhi kwenye mabenki ya Nje ya Nchi kama USwis na UK na kusamehewa vifungo wao na washirika wao!!!.Ama wafungwe maisha kwa kugoma kutoa ushrikiano iwapo Serikali imeridhika na ushahidi kuwa wao ndio wamilki halali wa UTAJIRI ambao Serikali kupitia TASK FORCE YA RECONCILIATION COMMITEEE imeridhika kuwa ni UTAJIRI uliopatikana kwa njia HARAMU na Wizi wa Mali ya umma.
Naamini kwenye RECONCILIATION KAMA TIBA YENYE FAIR GAME, vinginevyo jibu la UTAJIRI WA VIONGOZI, WATENDAJI WA SERIKALI NA BAADHI YA WANANCHI NA WAGENI, UTAZAA MTAFARUKU MKUBWA SANA NCHINI SIKU ZIJAZO. VINGINEVYO TAIFA LITAITAJI KIONGOZI AINA YA KAGAME KUTOA MAJIBU YA MASWALI YA UMMA JUU YA UTAJIRI WA WATUHUMIWA.NA AKIPATIKA KIONGOZI HUYO ITAKUWA IMEKULA KWAO VIONGOZI NA WASHIRIKA WAO NA VIZAZI VYAO, TOFAUTI NA WANGETUMIA RECONCILIATION COMMITTEE KAMA NJIA YA MAJIBU FAIRA NA FAIDA KWAO WAO WATUHUMIWA NA WENGINE KAMA TAIFA..