Kwa mujibu wa gazeti la DIRA la leo toleo la Novemba 29 - Desemba 5, 2010, waziri mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, amebomoa jengo la kihistoria la Nyumba ya Sanaa pale karibu na Movenpik Hotel Dar city centre na sasa atajenga gorofa 25 kwenye eneo hilo.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mradi huo utagharimu dola za kimarekani $45.5 million, sawa na takriban shilingi bilioni 70!.
Mradi huo wa jengo unajengwa kupitia kampuni ya Lowassa inayoitwa Integrated Property Investment (Tanzania) Limited.
Kuna tuhuma kuwa huu ni mradi wa kifisadi. Wasanii walilalamika mpaka Ikulu kwa Kikwete kujaribu kuzuia Nyumba ya Sanaa isivunjwe na kampuni ya Lowassa wakashindwa.
Kampuni hiyo ya Lowassa ndiyo iliyohusika na kashfa ya kununua nyumba huko London kwa karibu shilingi bilioni 1. Kwa mujibu wa gazeti la RAIA MWEMA la wiki iliyopita, mtoto wa Lowassa, Frederick, anachunguzwa na polisi wa Uingereza kutokana na kashfa hiyo.
* Je, Lowassa ambaye maisha yake yote amekuwa civil servant ametoa wapi 70bn/- kujenga gorofa hilo?
* TAKUKURU inasemaje kuhusu utajiri wa kutisha wa PM huyu wa zamani haswa baada ya yeye kuhusishwa na ufisadi wa Richmond na baadae TAKUKURU kumkosha?
* Huyu ndiye mtu anayetaka kuwa Rais baada ya Kikwete 2015 "by any means necessary" kwa kushirikiana na Rostam Aziz, Andrew Chenge, Nazir Karamagi, Yusuf Manji, Yusuf Makamba, Kingunge Ngombale Mwiru, etc. Nchi hii ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itapona kweli?