Lowassa kuongea na Wananchi 14/05/2015 kupitia Clouds FM

Lowassa kuongea na Wananchi 14/05/2015 kupitia Clouds FM

Nitamuuliza maswali matatu tu.akijibu aende Kuchukuwa fomu kwa upande wangu nitaridhika labda kwa watanzania wengine.
 
leo katika kipindi cha clouds fm asubuhi,watangazaji wa kipindi hicho wamesema mbunge wa monduli,ndugu edward ngoyai lowassa atatangaza maamuzi magumu na mazito kuhusu hatma yake ndani ya chama na uamuzi wake wa kutangaza nia ya urais kuelekea october 2015

katika kipindi hicho lowassa atajibu maswali yote yanayoelekezwa kwake,kashfa na sintofahamu mbalimbali dhidi yake.

Qitakumbukwa toka kashfa ya richmond iliyomuondoa madarakani mwaka 2008,mh.lowassa hakuwahi kuongea rasmi na vyombo vya habari kuhusu yeye,mambo yake ya richmond na nia yake kuelekea magogoni 2015.

Mara zote alipokuwa akiulizwa swali la kutaka urais,lowassa amekuwa akijibu "we will cross the brigde when we reach there"

nafasi hii inawapa wananchi fursa ya kumuuliza na kupata ufafanuzi wa mambo yenye utata kumuhusu yeye na hasa ktk nia ya kuelekea magogoni 2015...watu wana maswali mengi,hasa kuhusu afya yake,matumizi makubwa ya pesa kuelekea magogoni,msimamo wake kuhusu rushwa na makundi ndani ya chama n.k

ningeomba wadau na hasa mods, pengine kuanzisha uzi maalumu ambao wadau mbalimbali wangetupia maswali ili hata watangazaji wa clouds fm kupitia kipindi cha power breakfast hiyo kesho kutwa.

Kupata maswali ya ziada ya kumuuliza yanayotokana na sintofahamu za wananchi wa kawaida wasio na nafasi ya kuonana na e.n. Lowassa
kulekea magogoni 2015 ni kishindo kikuu
breaking newzzz!!!!.
Kwa wote marafiki wa lowassa ambao mnahitaji kwenda arusha.muda ni saa kumi na moja jioni.
Leo tunakikao cha maandalizi pale dodoma carnival..karibia na stand ya mkoa.
Unakaribishwa sana kwani ni mhimu kufika kwako.ukipata ujumbe huu mjulishe na mwingine ambaye ni friend of lowassa.
Ahsanteni
 
Hakika Lowassa akiukosa urais .............
 
Huu ndo mwaka kusikia watu wanazimia kwa presha za ghafla .EL anataka kutangaza maamuzi magumu ya kumfuata yule aliyemkaribisha tayari?
 
Leo katika kipindi cha Clouds Fm asubuhi,watangazaji wa kipindi hicho wamesema Mbunge wa Monduli,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa atatangaza maamuzi magumu na mazito kuhusu hatma yake ndani ya chama na uamuzi wake wa kutangaza nia ya urais kuelekea October 2015

Katika kipindi hicho Lowassa atajibu maswali yote yanayoelekezwa kwake,kashfa na sintofahamu mbalimbali dhidi yake.

QItakumbukwa toka kashfa ya Richmond iliyomuondoa madarakani mwaka 2008,Mh.Lowassa hakuwahi kuongea rasmi na vyombo vya habari kuhusu yeye,mambo yake ya richmond na nia yake kuelekea Magogoni 2015.

Mara zote alipokuwa akiulizwa swali la kutaka urais,Lowassa amekuwa akijibu "We will cross the brigde when we reach there"

Nafasi hii inawapa wananchi fursa ya kumuuliza na kupata ufafanuzi wa mambo yenye utata kumuhusu yeye na hasa ktk nia ya kuelekea Magogoni 2015...watu wana maswali mengi,hasa kuhusu afya yake,matumizi makubwa ya pesa kuelekea Magogoni,msimamo wake kuhusu rushwa na makundi ndani ya chama n.k

Ningeomba wadau na hasa Mods, pengine kuanzisha uzi maalumu ambao wadau mbalimbali wangetupia maswali ili hata watangazaji wa Clouds Fm kupitia kipindi cha Power Breakfast hiyo kesho kutwa.

Kupata maswali ya ziada ya kumuuliza yanayotokana na sintofahamu za wananchi wa kawaida wasio na nafasi ya kuonana na E.N. Lowassa
Kulekea Magogoni 2015 ni kishindo kikuu

KWA HISANI YA GAZETI LA MUHIMILI TULIPATA MASWALI HAYA- TUNAYAWEKA HAPA KAMA AKIPATA NAFASI AYAJIBU

[h=2]1. Kupitia ukurasa huu wa “KIZIMBA CHA MUHIMILI” tunataka Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowasa apande kwenye kizimba hiki ilia je atujibu maswali haya kabla ya kutuomba kura za kuwa raisi wetu. Lowasa simama hapo kizimbani,tujibu maswali haya yafuatayo:[/h] [h=2]2. -Ndugu Edward Lowasa,hebu tuambie wewe ulihusika vipi katika sakata la Richmond lililokufanya kujiuzulu nafasi nzito ya Waziri Mkuu huku ukilalama kuwa ulifanya hivyo kwa ajili ya kulinda Chama chako cha CCM?[/h] [h=2]3. -Je kwa kujiuzulu kwako kutokana na sakata la Richmond ulikisaidiaje chako,na je hicho chama chako nacho kilikuwa mmoja ya washirika wa lile kashfa ya Richmond?[/h] [h=2]4. -Ndugu Edward Lowasa; kumbukumbu zinaonyesha kuwa kabla na baada ya kuwa Waziri Mkuu hujawahi kusikika ukiikemea rushwa na ufisadi,ni kwanini?[/h] [h=2]5. -Ndugu Edward Lowasa; kuna tuhuma ambazo hujawahi kuzikanusha mpaka leo za kuwa ulipokuwa Waziri wa Ardhi ulijinyakulia ranchi za Taifa huko Misenyi na kuwa uliziandikisha kwa majina ya wanao ili kukwepa kuwajibika,je unaweza kutupa ufafanuzi wake?[/h] [h=2]6. -Edward Lowasa; kuna minong’ono ya chini kwa chini kuwa mwaka 2004 ulipokuwa Waziri wa Ardhi ulijinyakulia nyumba mbili (2) za Serikali maeneo ya Mikocheni na kuzikarabati kwa kutumia mabilioni ya pesa za Umma ,kwamba hizo nyumba zilikuja kuzinduliwa na aliyekuwa Raisi wa Afrika Kusini wakati huo Mheshimiwa Thabo Mbeki na kuwa hizo nyumba ukaja kuzipangisha kuwa ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini ambao ni wapangaji wako mpaka leo huku ukijipatia mamilioni ya dola za kimarekani kama kodi ya nyumba hizo,je ni kweli?? Na kama ni kweli huoni kama huo ni mpwayo wa maaadili ya Utumishi wa Umma?[/h] [h=2]7. -Edward Lowasa kuna habari kuwa wakati wa Utumishi wako wa uwaziri wa kawaida na hata ulipokuwa Waziri Mkuu kuwa hukuwahi kutembelea Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka hivi majuzi ulipokwenda kutafuta kuungwa mkono kwa ajili ya mbio za kuusaka uraisi,ni kwa vipi unaweza kututhibitishia kuwa wewe ni mpenzi wa huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo ni moja ya takwa la chama chako cha CCM?[/h] [h=2]8. -Edward Lowasa; kuna habari iliwahi kuandikwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa wewe unamiliki nyumba nchini Uingereza,jijini London,mtaa wa Churchil ambayo inasemekana uliinunua ukiwa ni Mtumishi wa Umma,vipi hiyo nyumba imo kwenye fomu ya Maadili ya Watumishi wa Umma na kwanini viongozi wa Uingereza walitilia shaka ununuzi huo?[/h] [h=2]9. -Edward Lowasa unasifika kwa kaulimbiu ya ”maamuzi magumu”. Katika moja ya maamzi yako yanayoitwa “maamuzi magumu” ukiwa Waziri Mkuu uliwahi kuamuru matumizi ya njia tatu barabarani huku ukijua kuwa ni unavunjifu wa Sheria ya Usalama Barabarani (The Roard Traffic Act),ambapo wananchi wengi walikufa kwa kugongwa hovyo na magari na baadaye kusitishwa kwa hizo njia tatu ili kuokoa maisha ya wananchi. Je unatuthibitishiaje umakini wako katika kutoa hayo maamuzi magumu? Na je una lipi la kusema kwa ndugu wa wale watu waliopoteza maisha kwa vifo vya ajali zilizotokana na maamuzi yako “magumu”?[/h] [h=2]10.-Edward Lowasa; ukiachana na ubunge wewe hauna kazi nyingine kwa sasa. Ninakuuliza huo ukwasi wa haya mamilioni mengi ya pesa unayoyatoa sehemu mbalimbali kwenye zinazoitwa harambee zinatoka kwenye mfuko upi?[/h] [h=2][/h] [h=2][/h]
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Picha sasa ndio linaanza rasmi trela zimeisha!

Kumekucha mkuu, Wakati umefika tutajua nani Rais wa wasafi na yupi wa Akudo. Vijana tunamtaka Lowassa Full stop
 
breaking newzzz!!!!.
Kwa wote marafiki wa lowassa ambao mnahitaji kwenda arusha.muda ni saa kumi na moja jioni.
Leo tunakikao cha maandalizi pale dodoma carnival..karibia na stand ya mkoa.
Unakaribishwa sana kwani ni mhimu kufika kwako.ukipata ujumbe huu mjulishe na mwingine ambaye ni friend of lowassa.
Ahsanteni
Mkuu nitumieni nauli kama laki tano tu itanifikisha dodoma.
 
Maswaliii yapi mkuu share apa nasubiri kumsikia jamaa
Maswali yanahusu maadili,ufisadi na utajiri alionao ambao kaupata kutokana na nafasi yake kama kiongozi wa umma,kutoa rushwa ili apitishwe kugombea urais.akiweza kujibu haya maswali kwa ufasaha watanzania wakamwelewa ruksa kugombea uongozi wa nchi hii.
 
mtu anayetaka kujisafisha kwa kutumia redio isiyo aminika na ambayo tetesi zinadokeza kwamba imenunuliwa na fisadi sana , ni kujishusha zaidi .
 
Back
Top Bottom